Wilfred Lwakatare
Member
- Dec 10, 2015
- 22
- 70
Sawa Mbunge, Lakini Mbona Inasemekana Huko Nyuma Ziliwahi Kuchangwa Pesa Alafu Zikapotelea Mikononi Mwako? . Mbona naona kama siku moja haitoshi, kwanini msingefanya tarehe 22 na tarehe 27 ili kujadiri kwa umakini, upana na mkaweza kuandaa vitu madhubuti?
Nimejisahihisha, zilikuwa za Abaana bashome. Niliumia sana kusikia kuwa zimepotea kwenye mikono ya mh mbunge wangu japo kuwa miaka ile nilikuwa bado dogo. Nikawaza mh. kashindwa kulitendea haki jina lake la Muganyizi.
Program ya Abaana Bashome ilikuwa chini ya Halmashauri ya Bukoba Mjini 2000-2005 mimi nikiwa Mbunge. Pesa zilizochangwa zilitumika katika kuboresha shule za serikali na kununua nyenzo zake. hakuna pesa iliyopokelewa na mikono yangu, zote zilielekezwa Halmashauri na records zipo. usipotoshwe na propaganda za kisiasa.
Tarehe 27 itakuwa ni fursa ya kujadili kwa umakini na upana agenda nilizoeleza hapo juu. pia tutatoa fursa ya ushiriki kwa mtandao na njia mbalimbali.
Karibu sana Tuijenge Bukoba kwa pamoja. SHUKRAN
Kazi nzur km litafanikiwa. Ila watu bado watu wana mashaka na hilo kongamano maana uliwahi kuchangisha hela za Abana Bashome zikaliwa.
Tokea umepata ubunge hujawahi kuonekana jmboni. Umeshndwa hata kuandaa mkutano wa kuwashukuru wananchi. Ss tuliokuwa washabiki wako ndo tunapgwa vjembe maana tunaambiwa tumemchagua mtu kapotea jimboni. Jirekebshe mzee kuwa karbu na wananchi wako ili ujue matatzo yao vngnevyo 2020 utapgwa chini. Nakutakia majukumu mema.
Kama ana makazi ya kudumu Kimara,watoto wote wamesoma Dar,mke yuko Dar naye anasoma mzumbe mbeya unategemea kweli aonekane Bukoba?
Kazi nzur km litafanikiwa. Ila watu bado watu wana mashaka na hilo kongamano maana uliwahi kuchangisha hela za Abana Bashome zikaliwa.
Tokea umepata ubunge hujawahi kuonekana jmboni. Umeshndwa hata kuandaa mkutano wa kuwashukuru wananchi. Ss tuliokuwa washabiki wako ndo tunapgwa vjembe maana tunaambiwa tumemchagua mtu kapotea jimboni. Jirekebshe mzee kuwa karbu na wananchi wako ili ujue matatzo yao vngnevyo 2020 utapgwa chini. Nakutakia majukumu mema.
ukiishi kwa propaganda utapata taabu sana. sherehe ya ushindi waulize wananchi waliokesha nyumbani kwangu Kibeta na kung'oa mahindi, maharagwe na mikungu ya ndizi. waulize wananchi tuliofanya nao usafi 9 Disemba 2015. Kaniulizie ofisi ya Mbunge Rwabizi. kaniulizie Ofisi za Halmashauri. na hivi sasa niko Bukoba tukijipanga na uchaguzi wa Mayor kesho Asubuhi.
siasa uchwara zinakwamisha maendeleo.
Kweli kabisa. Huu ni muda wa kurudsha heshima ya Bukoba kwmb ni "abashomi". Maana nshomile ni wengi lakn wameshndwa kuijenga Bukoba yao kutokana na tabia ulizozitaja. Mungu atutangulie. Mbunge wetu inabd awaunganishe watu wa Bukoba ili kufuta yale makundi ya siasa ili twende sawa kimaendeleo.Mh. nimekuelewa kama hivyo ndivyo. Sasa mkishaandaa agenda za mkutano mtufahamishe ili tuweze nasi kuchangia hizo ajenda. Tunaelewa ishu ni maendeleo lakini naamini mkishaiweka vizuri itatuwia rahisi. Ni jambo jema ila niwasihi wenzangu kwenye mambo haya tuachane na "emize" na "kabambone", okugaya, okushonesangana, okwanjalana na kamunobere haya mambo si ya kuchekea na kukumbatia. Ni bora sana wakati mwingine tukaukosa mchango wako kuliko kutumia lugha za hivi.
Mzee tatzo sio sherehe, nisome vzuri! Ulipaswa kuweka mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi km mbunge. Sijaongelea sherehe hzo. Hata madiwani wengi baada ya kushnda walifanya sherehe lakn hilo halikuwazuia kupita kwa wananchi kuwashukuru.
Mbunge wangu usipokuwa mtu wa kupokea maoni ya watu wako mbeleni kuna tabu. Kagasheki kilichomuangusha ni hayo hayo ya kuamini kila anachofanya yy ni sahihi na hakuna mtu wa kumshauri.