Bugando hospital siwaelewi

BOFREE

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
1,032
1,402
Jamani ndugu zangu wa jamiiforum mimi nina mgonjwa hospitali ya Bugando anatakiwa afanyiwe uchunguzi na mashine ya CT Scan. Cha kushangaza nimeambiwa kuwa mashine ya CT Scan imeharibika ina miezi mingi haifanyi kazi.

Hivi hospitali kubwa tena ya rufaa wanashindwa kununua hiyo mashine?, na cha kushangaza madaktari wananiambia kwamba mashine kama hiyo ipo Isamilo kuna kitengo cha mtu binafsi anayo na gharama yake ni laki tatu na kwavile mgonjwa hayuko vizuri kiafya inabidi nikodi na gari kutoka Bugando hadi kwenye hicho kitengo.

Sasa iweje mtu binafsi anayo halafu hospitali ya rufaa mnashindwa kununua? Hapa napata wasiwasi kwamba inawezekana hawanunui makusudi ili wagonjwa wawe wanapelekwa kwenye hicho kitengo kwa gharama kubwa na inawezekana mwenye hicho kitengo ni muhusika mkubwa wa hospitali ya Bugando.

Hivyo rai yangu nawaomba viongozi wa hospitali ya Bugando waweze kununua iyo mashine ili wananchi tuepuke gharama za kukodi gari la wagonjwa na natumaini gharama zitapungua kama CT Scan ikipatikana hospitali ya Bugando.
 
Back
Top Bottom