Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,431
- 73,078
Kwa mara ya kwanza katika historia, Budget ya serikali iliyopitishwa na bunge imeonekana na mkanganyo na mapungufu siku ya kwanza kuanza kutumika.
Ongezeko la VAT 18% katika miamala ya kibenki imeleta mkanganyo kati ya BOT, TRA na Mabenki katika kutafsiri sheria iliyopitishwa kutokana na mapungufu yake na kuleta shida kwa wananchi.
Ikumbukwe budget hii na sheria zake zimepitishwa kwa kishindo na wabunge wa CCM kwa kishindo bila tafakari ya kina huku wapinzani wakiwa nje kwa kufukuzwa na wengine wote kususia.
Sasa ndio pengo la kutokuwepo bungeni wale wabunge wanaohoji kipengele kwa kipengele ndio linaonekana. Tulikuwa tunaona watu kama Lissu,Zitto, Mnyika nk wakionekana kama wabishi kwa kuhoji na kufanya marekebisho ya msingi kumbe hilo ndio lilikuwa linaepusha aibu kama hii ya SIKU YA KWANZA kuchanganyana BOT, TRA ,mabenki na wananchi.
Jee ni mapungufu mangapi yataibuka jinsi siku zinavyoenda? Hii ni kwamba Naibu Spika Tulia amesababisha kuwa na mitafaruku ya budget 2016/17 kwa kutokuwepo watetezi makini na wenye weledi kujadili katiba.