Buddha 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Buddha 2

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Dec 2, 2009.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  .ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}

  .ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;} Tulimalizia asubuhi hii kwa kusema kwamba Gautama aliacha maisha katika Kasri,na kusema kwamba ataendelea maisha yake kutafuta Kweli. Sasa,tuendelee.

  "" Gautama alipoondoka kutoka kwenye Kasri ya baba yake,mfalme,akili yake ilikuwa imejaa mawazo mengi.Alistushwa sana kuona ugonjwa wakati yeye alikuwa hafahamu kuhusu ugonjwa,aliona kifo,wakati yeye alikuwa hajui kifo,na kuona amani kubwa,utulivu mkubwa,na kutosheka. Mawazo yake yalikuwa kwamba kwa vile yule aliyekuwa na hali ya kutosheka alikua amevaa nguo ya mtawa,basi kutosheka na amani ya ndani itapatikana kwa kuvaa magwanda ya mtawa,kwa hiyo akaondoka kutafuta utulivu wa ndani,katika lengo lake la kutafuta maana ya maisha.

  . ''Alikwenda mwendo wa mbali sana,mpaka kuvuka maeneo ambayo baba yake alikuwa anatawala,akazidi kwenda mbele kufuatia uvumi kuhusu wamonaki,na watawa waliokuwa wanaishi peke yao.[hermits]. Alijifunza kutoka kwa walimu bora kuliko wote alioweza kuwapata,alikuwa akisoma wakati wowote kulipokuwa na chochote cha kujifunza. Baada ya kujifunza kwa mwalimu mmoja yote ambayo yule mwalimu angeweza kumfundisha alisonga mbele,daima alisonga mbele,kila mara anatafuta kile kitu ambacho ni kigumu sana kutapikana katika Dunia hii-amani ya akili,utulivu.

  ''Gautama alikuwa mwanafunzi mwenye bidii. Alikuwa amebarikiwa katika maisha yake, amejaliwa kuwa na akili makini na ufahamu mkubwa. Aliweza kukusanya habari na kuzichambua katika akili yake na kubakiza mambo yale tu yalikokuwa na faida na thamani. Mmoja wa Walimu Wakubwa,ambaye alipendezwa na ari ya Gautama na akili yake makini,alimuomba abaki na kufundisha. Lakini hili lilikuwa ni jambo ambalo likuwa kinyume kabisa na imani ya Gautama kwa sababu-akafikiria-ataweza vipi kufundisha mambo ambayo yeye mwenyewe alikuwa hayaelewi vizuri?Anaweza vipi kuwafundisha wengine wakati yeye bado alikuwa anaitafuta Kweli ?Aliifahamu Misahafu na Commentaries za Misahafu,lakini,ingawa Misahafu ilileta amani kiasi fulani[a certain degree of peace],lakini bado kulikuwa na maswali na matatizo yalioiondoa amani aliyokuwa anaitafuta,kwa hiyo Gautama akaendea na safari yake.

  ''Alikuwa mtu amepagawa,mtu mwenye ari kubwa ambayo haikumruhusu kupumzika,inamsukuma zaidi na zaidi kutafuta elimu,kutafuta Kweli. Hermit mmoja akamfanya kuamini maisha ya kujitesa tu ndiyo yanayoweza kumletea amani[ascetic life].,kwa hiyo,kwa ajili ya utundu wake,Gautama akajaribu maisha ya kujitesa. Tokea zamani alikuwa ameshaacha vitu vyote alivyokuwa navyo,alikuwa hana starehe za mwili,aliishi tu na kutafuta maana iliyopo nyuma ya maisha. Lakini sasa akajilazimisha kula chakula kidogo zaidi na zaidi,na,kama zinavyosema hadithi za zamani,zamani sana,mwisho wake akaweza kuishi kwa punje moja ya mchele kwa siku.

  ''Muda wake wote aliutumia kufanya tafakari ya kina sana. Lakini mwishowe kula kwake kidogo kukaanza kumdhuru,afya yake iliporomoka,kwa ajili ya njaa na utapiamlo,na kukosa matunzo ya msingi. Kwa muda mrefu alidumu ukingoni mwa maisha,lakini hakuna ufahamu ulimjia,alikuwa bado hajaipata siri ya utulivu,alikuwa bado hajaipata siri ya kitu kigumu kabisa kupatikana Duniani-amani ya akili,shwari.

  '''''Rafiki' fulani walikuwa wamejikusanya mbele yake katika siku zile alizokuwa anaishi maisha ya njaa,wakafikiria kwamba hapa kuna jambo la kusisimua,kuna mtawa anaishi kwa punje moja ya mchele kwa siku. Walikuwa wanafikiria kwamba watapata faida nyingi kuhusiana na mtu mwenye vituko kama huyu. Lakini,kama 'rafiki' duniani kote,hawa walimuacha katika wakati wake wa shida. Gautama alipolala pale amekaribia kufa kwa ajili ya njaa rafiki zake wakamuacha mmoja baada ya mwingine. Gautama akawa peke yake tena,bila usumbufu unaotokana na marafiki,bila kusumbuliwa na wafuasi,alikuwa huru tena kuanza tena kufikiria upya kuhusu maana iliyopo nyuma ya maisha.

  Tukio hili ndilo lililofanya Gauatama abadilishe mwelekeo wake. Kwa miaka mingi alikuwa anafanya mazoezi ya yoga,ili,kwa kuutesa mwili,aweze kuifanya roho iwe huru kutokana na kifungo cha mwili,lakini sasa aliona kwamba yoga haina faida yoyote kwake,yoga ilikuwa ni njia tu ya kupata nidhamu kidogo juu ya mwili wenye ubishi,lakini ilikuwa haina faida kubwa sana ya kumsaidia mtu katika mambo ya kiroho. Pia aligundua kwamba kulikuwa hakuna faida kubwa kuishi maisha ya kujitesa vikali kwa vile kuendeleza mateso kutasababisha tu kufa kwake na maswali yake hayajajibiwa na kutafuta kwake hakujaisha. Akalifikiria hilo swala pia,na akaamua kwamba alichokuwa anafanya ilikuwa ni sawa na kujaribu kutoa maji kutoka kwenye Mto Ganges kwa kutumia ungo,au kutoa maji katika Mto Ruvuma kwa kutumia ungo,au kufunga mafundo katika hewa.

  '' Kwa mara nyingine tena Gautama akafikiria,akakaa chini ya mti,mdhaifu huku anatetemeka,na udhaifu unaowajia wale ambao wamekaa njaa mda mrefu sana na ambao wameponea chupu chupu kufa. Akakaa chini ya mti na kutafakari kwa kina kuhusu matatizo ya kukosa furaha na kuhusu mateso. Akadhamiria kwamba kwa vile tayari alikuwa ameshatumia miaka sita kutafuta elimu bila kupata jibu,atakaa na kutafakari na hatainuka mpaka apate jibu la tatizo lake.

  '' Gautama akakaa na jua likazama,na giza likashuka katika nchi,na ndege wa usiku wakaanza kuita kwao na wanyama wakaanza kuranda katika mawindo. Gautama akakaa. Saa ndefu za usiku zikajikokota na punde mionzi ya kwanza ya mwangaza ilianza kutokea katika anga,alfajiri ilikuwa inakaribia. Gautama alikaa na kutafakari

  '' Viumbe wote wa porini walishuhudia mateso ya Gautama alivyochoka siku iliyopita kabla hajakaa peke yake chini ya mti mkubwa. Alikuwa na huruma zao,na uelewa wao,na viumbe wote porini wakafikiria katika akili zao jinsi ya kumsaidia binadamu kutoka katika matatizo makubwa aliyotumbukia.

  ''Tigers wakaacha kuunguruma ili miimbo yao na kuita kwao kusimsumbue Gautama aliyekuwa anatafakari;nyani wakaacha kelele zao,wakaacha kuruka kutoka tawi moja kwenda tawi jingine;badala yake wakakaa kimya wanatumaini,wanatumaini. Ndege wakaacha nyimbo yao,wakaacha makelele yao,na badale yake,wakakaa,nakupigapiga mabawa yao kwa matumaini ya kuweza kumsaidia Gautama kwa kumpelekea mawimbi ya mapendo na mawimbi ya hewa ya kumpooza. Mbwa,ambao kwa kawaida walikuwa wanabweka na kukimbia kila pahali,waliacha kelele zao na wakaenda na kujificha ambapo mionzi ya jua isiwafikie. Mfalme wa konokono,alipotazama na kuona kwamba mbwa wametoweka na kwenda kivulini,akafikiria jinsi yeye na watu wake wanavyoweza kuwasaidia binadamu kwa kupitia Gautama. Mfalme wa konokono akawaita watu wake na pole pole akaongoza njia kwenda kwenye mgongo wa Gautama,wakapanda shingo lake,na pole pole wakakusanyika katika kichwa chake ambacho kilikuwa chekundu kwa ajili ya jua,kile kichwa ambacho kilikuwa katika tafakari ya kina,kile kichwa ambacho kilikuwa kimeunguzwa na mionzi mikali ya jua;wale kono kono walikusanyika na miili yao iliyopoa walimkinga Gautama kutokana na jua la mchana,na nani anajua,hao konokono kwa kukipooza kichwa cha Gautama labda walimsaidia katika kufanikiwa kwake. Watu wa porini wakati fulani walikuwa rafiki wa Binadamu,hawakumwogopa Binadamu,na kabla ya Binadamu walipowasaliti,watu wa porini waliwasaidia Binadamu
  .ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;}
  Siku ikaendelea,ikaendelea na Gautama alikaa bila kutingishika,bila kutingishika kama sanamu ya kuchongwa. Kwa mara nyingine tena usiku ukafika,giza likafika,na mara nyingine tena alfajiri ilipokaribia ikatokea mionzi katika anga,halafu jua likafika katika horizon. Lakini wakati huu jua likamletea Gautama ufahamu. Kama vile amepigwa na radi,wazo likamjia Gautama,alikuwa na jibu,au jibu nusu kwa matatizo aliyokuwa nayo. Alipata ufahamu kwa kupata habari mpya,alikuwa ''Aliyeamka',ambayo kwa Kihindi inaitwa ''Buddha''

  ''Roho yake iliangazwa kwa kwa kile kilichotokea wakati wa kutafakari kwake katika ulimwengu wa roho[astral plane],alipata ufahamu na alikumbuka mambo aliyoyaona katika ulimwengu wa roho. Sasa,kama alivyoelewa,atakuwa huru kutokana na karaha za maisha ya dunia,atakuwa huru kutokana na kurudi dauniani tena na tena katika mzunguko usiokuwa na mwisho wa kuzaliwa,kufa,na kuzaliwa tena. Alipata elimu kuhusu kwa nini binadamu lazima ateseke,ilisababishwa na nini, kiini chake ni nini,na jinsi ya kuyamaliza.

  ''Kutokea wakati ule Gautama akawa Gautama Aliyeamka,au ,kuisema Kihindi,Gautama Buddha. Sasa akafikiria tena afanye nini. Aliteseka na alijifunza,kwa hiyo,awafundishe wengine au awaachie wengine wagundue kwa njia zile zile alizotumia kugundua?Alikuwa na wasiwasi,kuna mtu mwingine yeyote ataamini mambo yaliyomfika? Lakini akaamua kwamba njia pekee ya kufahamu jibu la swali hili ni kwenda kuongea na wengine ,na kuwaeleza habari njema ya ufahamu uliomfikia

  '' Akanyanyuka,na baada ya kula chakula kidogo na kunywa maji,akaondoka kueleka Benares ambako alitumaini kuwaona rafiki zake watano kati ya wale waliomuacha alipokuwa anahitaji msaada mkubwa-ambao walimuacha alipoamua kula chakula tena.
  '' Baada ya safari iliyochukua muda mrefu kiasi,kwa sababu Gautama alikuwa bado mdhaifu kwa ajili ya maisha yake ya kukosa mahitaji ya msingi,akafika Benares na kuwakuta wale rafiki zake aliokuwa anawatafuta. Akaongea nao,na akawaelezea ile ambayo iimefahamika katika historia kama ,'' Khutba kuhusu Kuzungusha Gurudumu la Sheria' Akawaambia waliokuwa wanamsikiliza chanzo cha mateso,kiini cha mateso,na akawaeleza jinsi wanavyoweza kuyashinda mateso;akawaeleza juu ya dini mpya ambayo sasa tunaifahamu kama Dini ya Buddha. ' Dini ya Buddha ina maana kwamba ni dini ya wale ambao wanataka kuamka upya.''

  Kwa hiyo Gautama aliifahamu njaa,nikafikiria? Mimi pia nilikuwa naifahamu njaa!Nilitamani kwamba huyu mwalimu angekuwa na huruma zaidi,kwetu sisi watoto,kwa sababu hatukuwa na chakula kingi cha kula,hatukuwa na muda mwingi wa ziada,na yeye alivyokuwa anaongea bila kuchoka,anaendelea tu kuongea na kuvuka muda uliopangwa,sisi tulikuwa na njaa,tumechoka,na hatukuwa na uwezo wa kuelewa umuhimu wa mambo aliyokuwa anazungumza.

  Yule kijana aliyechelewa kufika kwenye masomo alikuwa bado anaiuguza pua yake ameishikilia pua yake isitoke damu ili asimuudhi zaidi Mwalimu. Na nikafikiria wakati ule,hii ina madhumini gani,kwa nini mateso mengi namna hii,kwa nini wale ambao ipo katika uwezo wao kuonyesha huruma,imani,na ufahamu-kwa nini wao,badale yake,wanatenda mambo ya ukatili? Niliamua kwamba mara mwalimu wangu atakaporudi itabidi nichunguze kwa kina kuhusu haya matatiozo ambayo kwa kweli yalikuwa yananihangaisha sana. Lakini nikaona kwa furaha kubwa kwamba yule Mwalimu wa Kihindi alikuwa anaonekana amechoka kidogo,alikuwa anaonekana ana njaa kidogo na kiu,alikuwa mara anasimama na mguu huu,mara anasimama na mguu mwingine. Sisi watoto wote tulikuwa tumekaa chini kwenye sakafu tumekunja miguu,wote isipokuwa mimi,na ilibidi nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kutulia ili nisionekane. Wengine walikaa wamekunja miguu,wamekaa kwa safu,na yule Mwalimu kwa akawaida alizunguka nyuma yetu anafanya patrol na tulikuwa hatujui yupo wapi,lakini huyu mtu,yule Mwalimu wa Kihindi,alikuwa anasimama mara mguu huu,mara mguu huu,alikuwa anatazama nje ya dirisha kutazama jinsi kivuli kilivyokuwa kinakwenda juu ya ardhi,na saa zilivyokuwa zinakwenda. Mwishowe akafikia uamuzi. Akajiinyoosha na kusema,''Sasa,tutapumzika.,mawazo yenu yanakwenda huko na huko,hamyasikilizi maneno yangu,maneno ambayo yanaweza kuathiri maisha yenu yote,na maisha yenu mengine katika miaka mingi ijayo. Tutapumzika kwa nusu saa. Mko huru kwenda kula,halafu mrudi kimya na nitaendelea kuongea kwangu.''
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ganesh,

  Ingekuwa vyema kama ungeziunganisha ili kuwe na flow.
   
Loading...