PreGE2025 Buchosa wakataa pesa za mgombea, 'hatutaki rushwa'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Buchosa, Mwanza Tukio la kushangaza linalodaiwa kukiuka taratibu na maadili ya uchaguzi limeibuka katika Jimbo la Buchosa, ambapo mtia nia wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Charles Tizeba, anaripotiwa kuwapatia wajumbe wa CCM kiasi cha shilingi elfu ishirini (20,000/=) kwa wajumbe jimbo zima, akidai hawezi kufanywa kitu sababu yeye ametumwa na Rais kuja kugombea na kuwashawishi wamchague katika kura za maoni zitakazofanyika Agosti 2, 2025.

Hata hivyo, wajumbe wa Kata ya Katwe wameibua mshangao kwa kukataa kupokea fedha hizo na kuzirejesha kwa msambazaji, wakidai kuwa hawako tayari kuuza dhamira yao kwa pesa, bali wanahitaji maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Buchosa.

“Hatutaki pesa ya masimango! Tunataka maendeleo ya kweli, na maendeleo hayo tunayayaona kwa Mbunge wetu Eric Shigongo na Diwani wetu Max Mkungu,” alisema mmoja wa wajumbe hao kwa msisitizo.

Wajumbe hao wamesema wanataka kiongozi mwenye dira ya kweli ya maendeleo, si mtu anayetumia fedha kama nyenzo ya kupata uongozi

Juhudi za kumpata Dkt. Charles Tizeba ili atoe ufafanuzi kuhusu tuhuma za kugawa fedha kwa wajumbe zilifanikiwa, ambapo alipokea simu ya mwandishi wetu. Hata hivyo, mara baada ya kusikia swali kuhusu madai hayo, alikata simu ghafla na kui block namba ya mwandishi wetu, hakutaka kuendelea na mahojiano. Jitihada za kumfikia tena hazikufua dafu, kwani hakupokea simu zilizofuata wala kujibu ujumbe wa maandishi aliotumiwa.​

chanzo: Mwanahabari​
 
Shigongo akikumbuka alipita kwa mgongo wa mwendazake anatamani akatambike kwenye kaburi lake mizimu impitishe tena😂 yeye si amegawa tisheti sasa anaogopa nini mwenzie kugawa fwedha
 
Unakaa elfu ishirini Ila maisha yako magumu unapewa basikeli na tisheti

Wakipewa hela kuleni Ila chagueni kiongozi mnayemtaka kwakuwa siasa hazina maana Tanzania
 
Mbona ni kama tukio limetengenezwa, kwanini hawakuzikataa huko walikozipokelea?
 
Kuleni hela na kura msiwape kama wajumbe wa chadema walivyomfanya Mbowe,Ili wajue pesa ni muhimu lakini siyo kila kitu
 
Hai ni mazezeta unakataa hela ila unakubali tishezi za kijani😀
 
Buchosa, Mwanza Tukio la kushangaza linalodaiwa kukiuka taratibu na maadili ya uchaguzi limeibuka katika Jimbo la Buchosa, ambapo mtia nia wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Charles Tizeba, anaripotiwa kuwapatia wajumbe wa CCM kiasi cha shilingi elfu ishirini (20,000/=) kwa wajumbe jimbo zima, akidai hawezi kufanywa kitu sababu yeye ametumwa na Rais kuja kugombea na kuwashawishi wamchague katika kura za maoni zitakazofanyika Agosti 2, 2025.

Hata hivyo, wajumbe wa Kata ya Katwe wameibua mshangao kwa kukataa kupokea fedha hizo na kuzirejesha kwa msambazaji, wakidai kuwa hawako tayari kuuza dhamira yao kwa pesa, bali wanahitaji maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Buchosa.

“Hatutaki pesa ya masimango! Tunataka maendeleo ya kweli, na maendeleo hayo tunayayaona kwa Mbunge wetu Eric Shigongo na Diwani wetu Max Mkungu,” alisema mmoja wa wajumbe hao kwa msisitizo.

Wajumbe hao wamesema wanataka kiongozi mwenye dira ya kweli ya maendeleo, si mtu anayetumia fedha kama nyenzo ya kupata uongozi

Juhudi za kumpata Dkt. Charles Tizeba ili atoe ufafanuzi kuhusu tuhuma za kugawa fedha kwa wajumbe zilifanikiwa, ambapo alipokea simu ya mwandishi wetu. Hata hivyo, mara baada ya kusikia swali kuhusu madai hayo, alikata simu ghafla na kui block namba ya mwandishi wetu, hakutaka kuendelea na mahojiano. Jitihada za kumfikia tena hazikufua dafu, kwani hakupokea simu zilizofuata wala kujibu ujumbe wa maandishi aliotumiwa.​
View attachment 3388435
chanzo: Mwanahabari​
Sema ccm buchosha wamekataa rushwa
 
Elfu ishirini tu wakati rais katoa pikipiki,baiskeli,milioni kumi Kwa Kila goli,na rushwa zingine nyingi ambazo siwezi kuzimaliza kuzitaja
 
Wanao mchafua raisi ni wengi ila hatochukuliwa hatua, ila sema no reform no election, unaondoka usiku usiku
 
Mbona hamjatuletea huku visiwani hizo pesa, mkiniletea pesa nakula kura ni siri yangu. Hao wabunge wa Buchosa tunapo wachagua tu, kuwaona tena ni hadi baada ya miaka mitano tena. No Reform no Election.
 
CCM wakatae rushwa. Nitakua w mwisho kuamini
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom