balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 16,868
- 15,735
Shule hii iko Kimara _Suka Dar Es Salaam,shule iko hovyo sana,hakuna utaratibu unaoeleweka.Ada zinapandishwa muda wowote wakijisikia,Wakifunga shule hawatoi report za matokeo ya mitihani na hata taarifa ya kwamba ada kiasi gani inayotakiwa kulipwa,siku ya kufungua watoto wanabughudhiwa,wananyanyaswa maana kama mzazi anadaiwa,mtoto atatengwa,atakalishwa chini kwenye madarasa yasiyo na sakafu akirudi nyumbani mchafuuu.Hiyo shule inamilikiwa na akina Meena,usafiri hovyo,wakuu wa shule wanabadirika kila kukicha.Ni shule vituko sana,mamlaka zifuatilie,wanabambika madeni na siyo waelewa kabisa.Ni shule ya kijinga sana.