Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,554
- 2,161
Taarifa zinazosambaa kwa kasi kwenye Mitandao ya kijamii ni kuhusu taarifa za ajali mbaya sana ya basi tajwa linalofanya safari zake kati ya Dar na Karagwe Kagera.
RPC Tabora amesema ajali ni Mbaya vifo kadhaa vimetokea.Basi limegongana na Lori.
Haya Mabasi ya City Boy yalishawahi kufungiwa.
Habari zaidi, soma=>SUMATRA yaifungia kampuni ya mabasi ya City Boy ambayo mabasi yake mawili yalisababisha ajali jana
Habari zaidi..
Taarifa zilizotufikia usiku huu zinaeleza kuna ajali mbaya sana ya basi la City Boy linalofanya safari zake kati ya Dar na Karagwe Kagera limegongana na Fuso huko Igunga mkoani Singida
Taarifa zaidi zinasema ajali hiyo imesababisha vifo kadhaa (idadi kamili bado haijafahamika)
Tunaendelea kufuatilia kwa kina ajali hii na tutawajuza zaidi..
======
TAARIFA YA AWALI YA AJALI YA CITY BOY NA FUSO KUTOKA TRAFFIC TABORA.
Nimefika eneo la tukio SAA 2330hrs toka Tabora mjini 200kms. Eneo ni Makomero tarafa na wilaya Igunga mkoa wa TABORA.
Gari T486 ARB FUSO ikiwa na mzigo wa viazi ikitokea Singida kuelekea Igunga tairi ya kulia litumbukia katika mashimo mawili barabarani kisha kupasua tairi na rim kupinda & mfumo wa usukani kukatika maungio ya steering rod na steering box kisha gari kukosa uelekeo na kugonga basi la abiria T983 DCE Scania kampuni ya City boy.
Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha , 10 eneo la tukio, 2 wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Wilaya Igunga. Jumla ya majeruhi 46 wamefikishwa Hospitali ya Wilaya Igunga kwa matibabu, kati yao 3 ni mahututi ambapo ME 02 wamepelekwa Bugando Mwanza na KE 01 amepelekwa Nkinga usiku huu.
Dereva wa basi amefariki papo hapo. Wahusika wa FUSO kwa taarifa za awali inasemekana wamekimbia baada ya ajali hii.
Toka kwa Insp Hardson Kaimu RTO Tabora.
UPDATES:
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa amethibitisha watu 12 kupoteza maisha na wengine 46 kujeruhiwa baada ya basi la City Boy kugongana uso kwa uso na fuso lililokuwa limebeba viazi katika kijiji cha Makomero, wilayani Igunga jana usiku.
Habari zaidi, soma=>Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi