'Brazamen, Bitoz, sista du'

'Brazamen, Bitoz, sista du'

Kuvaa raba za rojamila, maradona, ziko na DH na kaunda za mchelemchele. Wadada walikua nacraba flani nyeusi zina shingo kidogo zinaitwa Loso, basi nikiwa std 4 nikaiba za sister nikaenda kuchezea mpira. Kwa kuwa ni kijijini na almost watoto wote mnacheza peku, nilikamua sana siku hiyo tukashinda 5-2 na mi nilifunga matatu. Sasa kw kuwa raba zilikuwa laini sana na watoto wa kijiji wako sugu zilichanika vibaya mno. Kilichonikuta huko home sina hamu ya kusimulia leo aisee

Haha. Hilo janga la loso lilishanikuta...na nilivaa za bibi...wee!!
 
suruali michael jackson au zico,kuna viatu vya kina dada vya mpira vina matundu mengi,tuliviita saa nane utanikoma.

Mkuu sio vya kiume kweli vile. Vyeusi vimechorwa kimtu kinaendesha baiskeli!!
 
Mi naona hawa watoto wa siku hizi kupata div 5 na div 4 za point 40 kuna mambo mengi yanachangia. Kwa mfano hata michezo ya watoto ya asili imepungua sana ukikompea na sisi wa enzi hizo. Mambo ya kombolela, mdako, nage, kuwinda kw manati. Kuendesha ma-ringi, baiskeli za miti, nyumba za udongo, magari ya mabati na maboksi n.k. vyote hivi vilikuwa brain activators. sasa siku hizi ni tamthiliya, bongo movie, play station n.k. eti kuna hadi tuition za chekechea. Nadhan I consider myself privillaged to be born by that time...

Hapo kwenye maringi sasa!! Tena unalifunga kamba kwenye kimti kisha mbio zinaanza!! Nakuunga mkono..maisha yale yametengeneza watu bora na sharp.
 
Mi nakumbuka viatu fulani hivi vyeusi vya plastiki almaarufu kama mwisho saa sita. Kama hukuvaa hivyo basi uliruka steji ya maisha. Pila kulikuwa na viatu vya gogo... Dah!
 
hapanaM.E.M.A vilikuwa vya kike rangi nyeupe na blue bahari vina matundu madogo madogo.
 
Wale wenye hizo title hapo juu waliozaliwa miaka ya 1978-84..walikuwa wana sifa za pekee ambazo ukiziona tu unawajua. Yaani zile za kumfanya aonekane mtu 'mjanja'. Mi nitataja baadhi kisha endelezeni.
Wanaume:
1. Kuvaa suruali za 'Tokyo, Van Basten'
2. Kubeba mabegi ya 'Montana'
3. Kutembea na 'walkman'
4. Kuchomeka t shirt au shati kwenye mkanda.
5. Kuvaa raba oversize
6. Kunyoa kwa kuchonga nywele za pembeni tuu.
7. Endeleza...

Wanawake:
1. Kuchoma nywele kwa kifuu/kigae
2. Kuvaa magauni/sketi za ngazi 3 na kuendelea.
3. Endelezeni nimezisahau ghafla nyingine.

Watoto wachanga mmeingilia historia msioijua.
Waulizeni baba zenu!
Hiyo miaka ya 78-84 ubrazzamen, sista do ubitozz nk ndio ulikuwa inakwisha tena.
Wakati huo BUDDY GUY keshakuja na kuondoka Dar, baada ya show kabambe Mnazi Mmoja gardens.... Ndio Mnazi mmoja ilikuwa budtani na mandhari safi kabisa.
The Beatles walikuwa tayari na hits kadhaa..... hadj 84 tayari watu wesha retire u brazzaman!!
 
Raba za DH, almaarufu, Dunia hadaa/Daud hana uwezo.
Viatu vya chacha.
 
duh mambo ya kunfuu shuzi(shoes)halafu unatembea na cheni(chain)unajifanya bruce lee.
 
kuvaa chupi za VIP na kuzikuta kifuani

hahaaahahaaa...uuuuwiiiii..oooooh.....ni kweli kabisaaaaa...kitu cha VIP ukikitupia kikipata tu joto hichooo kinapanda kifuani au kama umevaa bukta basi utakuta kime-over take bukta mpaka magotini....duuuuuh....asante sana Catherini
 
kuvaa chupi za VIP na kuzikuta kifuani

hahaaahahaaa...uuuuwiiiii..oooooh.....ni kweli kabisaaaaa...kitu cha VIP ukikitupia kikipata tu joto hichooo kinapanda kifuani au kama umevaa bukta basi utakuta kime-over take bukta mpaka magotini....duuuuuh....asante sana Catherini
 
Back
Top Bottom