Brainstorming

Brainstorming

SMB Group

New Member
Joined
Apr 13, 2019
Posts
4
Reaction score
0
UJUMBE WA TANO.

Na Saidi Mbondela.

Ankara/Turkey

13/04/19.

Habari,

Ujumbe wangu wa leo utakua unakamilisha awamu ya kwanza ya jumbe zangu kwa vijana. Awamu hii nilijikita kutoa maelekezo kuhusu namna ya kuweza kuajirika kwa urahisi katika zama hizi zilizojaa mabadiliko ya kila namna katika mifumo ya kazi. Kwa msomaji makini atakua tayari kashaanza kuchuka hatua za kuweza kujijenga ili ajiuze kwa haraka katika soko la ajira. Lengo langu kubwa kukushauri uanze kwa kuajiriwa ni kutaka upate nafasi ya kujifunza kazi, vilevile nilitaka ujue uchungu wa kuajiriwa ili uweze kupata maarifa ya kuja na wazo lako la kujiajiri.

Awamu ya pili ya jumbe zangu nitaelekeza nguvu kuzungumzia kuhusu kujiajiri na nitaanza kutoa maelezo kuanzia hatua za awali kabisa kuanzia namna ya kuweza kuzitambua fursa mbalimbali za kibiashara katika mazingira yako, vipi utaweza kupata mtaji, mbinu za kimasoko, namna ya kusimamia kazi yako ili uweze kufikia malengo na mengine mengi. Jiweke tayari kusoma.

Tumalizie ujumbe huu kwa kuendelea kutokea pale tulipoishia katika ujumbe wa nne.

Ujumbe wa nne niliumalizia kwa kukuonesha umuhimu wa kua na uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali katika kazi ili uweze kufanikiwa sokoni. Katika uwanja uliojaa upinzani lazima uwe na mbinu kabambe za kukusaidia kuwashinda wapinzani wako kinyume na hivyo hutoweza kuumudu ushindani.


Katika Ushindani inabidi uzingatie matokeo ya maamuzi yako pamoja na ya mpinzani wako. Kitaalam tunasema Payoffs, Payoffs ndio muongozo wako katika kukusaidia kufanya maamuzi. Ili uwe na Payoffs lazima ubaini mpinzani wako atafanya maamuzi gani ili wewe uje na maamuzi ambayo yakikabiliana na maamuzi yake utamshinda. Hapa nazungumzia uwezo wa kuona kupitia macho ya mpinzani wako we say Seeing through your rival’s strategies. Wakati unafikiria haya inabidi ukumbuke kua mpinzani wako naye anapiga mahesabu sawa na unayopiga wewe hivyo lazima ujitahidi kutotabirika, kama unakumbuka katika ujumbe wangu wa tatu nilikwambia avoid to be predictable.

Nivipi mtu atakua predictable?

Jibu ni kwamba utakua predictable kama utatumia strategies zinazofanana kila kukicha, na ndio maana nilikushauri katika ujumbe wangu wa tatu uwe unamix strategies zako ili mpinzani asikuotee in your next move.

Katika strategies zako zipo ambazo kila ukilinganisha na strategies zingine ili kukabliana na mpinzani zenyewe zinaleta payoff ndogo, Strategies hizo tunaziita Dominated strategies, hizo hazifai kutumika katika soko la upinzani. Kinyume chake zipo strategies ambazo kila ukilinganisha na zengine ili kukabiliana na mpinzani zenyewe huleta payoff kubwa hizo tunaziita Dominant Strategies.

Turudi kwenye Mchuano wetu kutokea Ujumbe wa Nne. Tuchukulie kwamba 30% ya wasomaji(hawa ni wale wenye kununua kulingana na habari iliyopo kurasa ya mbele, they are not loyal readers) wanavutiwa na habari ya Mh. Lowasa Kurudi CCM na asilimia 70% wanavutiwa na habari kuhusu mapokezi ya mwili wa Ruge.

Hivyo Wahariri wa magezti yote mawili wanaweza wakafikiri kama ifuatavyo lakini kila mmoja kivyake, wakiwa wamejificha katika vyumba vyao vya siri.


“Ikiwa tatuweka habari ya Lowasa Kurudi CCM na wapinzani wakaweka habari kuhusu mapolezi ya mwili wa Ruge ina maana tutapata 30% zote za wataovutiwa na Habari ya Lowasa kurudi CCM. Wao wakiweka ya Mapokezi ya Mwili wa Ruge watapata 70% zote. Ikiwa tutaweka habari Lowasa kurudi CCM na wapinzani nao wakaweka habari hiyo hiyo tutagawana shea iliyopo sokoni hivyo tutapata 15% na wao asilimia 15%.


Pia, ikiwa tutaweka habari ya Mwili w Ruge na wapinzani wakweka habari ya Lowasa kurudi CCM tutapata 70% zote za wanaovutiwana habari ya mwl wa Ruge. Safari hii wao watapta 30% zote kuhusu Lowasa kurudi CCM. Ikiwa wapinzani wetu nao wataweka habari kuhusu Mwili wa Ruge tutagawana shea iliyopo Sokoni hivyo tutapata 35% na wa asilimia 35%.”

Katika payoffs hizi tunaona habari kuhusu mapokezi ya mwili wa Ruge ina payoff kubwa zaidi bila kujali mpinzani ataweka habari gani. Ni 70% zote au 35% ambayo ni zaidi ya 30% au 15% kwa habari ya Lowasa kurudi CCM. Hivyo habari kuhusu mwili wa Ruge na mapokezi yake itakua ni Dominant strategy na habari kuhusu Lowasa itakua ni Dominated Strategy.

Kwakua magazeti yote mawili yanataka faida hivyo habari kuhusu mapokeziya mwili wa Ruge ndiyo itayotamba zaidi katika kurasa za mbele za magazeti hayo. Huo ni mfano mmoja mdogo unaotaka mtu awe na uwezo wa kubaini mbinu gani ya kutumia katika changamoto flani hasa katika soko lililojaa upinzani kwa ajili ya faida kadha wakadha kwa Kampuni.





You are ready know how much Complex problem solving skills and Decision Making skills are important. The same applies for the rest mentioned skills in my 4th Article.



Katika ujumbe huu tunaona umuhimu wa kuwa na Big Data( kubaini shea ya yako na ya mpinzani wako sokoni inabidi uwe na data za kutosha) vilevile umuhimu wa kuwa na Data Scientists watu ambao wanalipwa vizuri sana duniani kwa sasa, hawa ni watu wanaowexa kizichambua data zetu kinagaubana zinakaleta maana kwetu.

Kumbuka huu ni ujumbe wa mwisho katika awamu hii ya kwanza. Awamu ya pili itaanza wiki kadhaa zijazo panapomajaaliwa.

Ili kujihakikishia kutokukosa mfululizo wa Makala hizi niandikie kupitia email yangu smbondela@hotmail.com kwa ajili ya kukuweka katika Database yangu ya wasomaji wa Makala zangu. Hivyo utakua miongoni mwa watu wa kwanza kupata Makala mpya inayotoka kila wiki siku ya jumamosi. Na kama ulikosa jumbe za mwanzo usisite kunijulisha ili nikutumie ujue wapi tulipotokea katika safari yetu hii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
UJUMBE WA NNE
06/04/2019
Ankara-Turkey.
Na Saidi Mbondela.

Salaam.

Karibu tena katika Makala zangu, leo tupo wiki ya nne na nilikuahidi kua siku ya leo nitakutajia juzi unazohitajika kua nazo nje ya fani yako unayosomea/uliyosomea chuo kikuu. Juzi hizo zitakuongezea sifa za kuweza kuajirika lakini pia kama upo kazini zitakufanya uwe katika ufanisi wa hali ya juu hivyo kukufanya uendelee kubaki kwenye ajira tena kwa kulipwa mshahara mzuri na mwajiri wako.
Utakubaliana na mimi kwamba mazingira ya kazi ya sasa yanabadilika kwa kasi ya ajabu kushinda wakati wowote hapo awali, kama ulitoka katika mfumo wa kazi kwa mwaka mmoja kisha ukarudi tena unaweza kukuta ujuzi ulikua nao mwaka jana hauhitajiki tena kazini au ukakuta kuna juzi zingine zinazohitajika na wewe hauko nazo. Naam hali ipo hivyo.
Msingi mkubwa hapa ambao ningependa utoke nao katika ujumbe huu ni swala zima la kuweza kujifunza kwa urahisi na haraka ili uendeane na kasi ya mabadiliko. Neno fupi na fasaha zaidi la kingereza naloweza kulitumia hapa ni Learnability.
World Economic Forum wametaja juzi kumi zitazoweza kukusadia kubakia ndani ya mfumo wa kikazi lakini pia zitakusaidia kuingia katika mfumo ikiwa ndo kwaanza unatafuta kazi. Ni hizi zifuatazo
Complex problem solving
Critical thinking
Creativity
People management
Working with others
Emotional intelligence
Judgment and decision making
Service orientation
Negotiation
Cognitive flexibility
Kwa mazingira yetu ya kitanzania unatakiwa uwaze nje ya box namna ya kuweza kuzikusanya juzi hizi kwani unaweza usikutane nazo katika masomo yako ya kila siku. Tumia muda wako kujiongeza wewe mwenyewe kwa ajili ya manufaa yako.
Hao ni World Economic Forum wametaja hizo kwa kuzingatia hali ya kiujumla duniani lakini tukirudi bongo naweza kusema hizo ni skills za mbali sana. Kuna jamaa zetu bado hawawezi kutumia Computer kwa kufanya kazi rahisi kabisa katika; kwa mfano kuchapa. Zaidi ya hilo zile zinazoitwa office programs yani Ms word, Ms Excell Ms Access na Power Point bado ni changamoto kwa vijana wengi. Katika dunia hii ya sasa dunia ya Big Data unaachaje kujifunza Excell kwa mfano? Unaweza kufanya maamuzi sahihi kama unashindwa kuandaa data zako katika mpangilio unaoleta maana?
Wapo jamaa hata kuandika CVs zao mpaka watazamie kwa wengine, wapo jamaa kujieleza walau kwa lugha ya taifa nako mtihani sikwambii kingereza. Wapo jamaa bado wajui official way ya kuandika emails, kwa kifupi soft skills hatujazipa kipaumbele. Jaribu kujitofautisha, zikusanye sifa zitazakufanya ujiuze kwa haraka kwa muajiri.
Tukirudi kwenye skills zetu 10 hapo juu tujaribu kidogo kuangalia Complex problem solving iliyochanganyika na Judgement and Decision Making skills.
Leo katika mazingira ya kazi zetu kuna changamoto mbalimbali zinazojitokeza, changamoto hizo zinanafasi ya kuipa kampuni faida na kuipandisha sokoni au ikawa kinyume chake. Hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kua na misingi na mikakati imara ya kuweza kupambunua changamoto hizo na kuitumia kwa ajili ya faida ya kampuni yenu. Nina kitabu kinaitwa Thinking Strategically kilichoandikwa na Avinash K.Dixit na Barry J. Nalebuff, jamaa wamejitahidi sana kuelezea kuhusu Strategic Moves katika kuziendea changamoto mbalimbali hasa katika soko lenye ushindani. Napendekeza ukitafute ili uweze kunufaika nacho.
Labda nikupe mfano moja katika sekta ya habari utaoweza kukuonesha umuhimu wa strategic moves. Wahariri wa magazeti hutumia muda mwingi sana katika vyumba vyao vya siri kujadili habari gani ya kuiweka katika kurasa ya mbele ya magaazeti yao ili kuvutia wasomaji. Wanafanya hivyo wakijua kwamba habari itayokuwepo katika kurasa ya mbele inaushawishi mkubwa kumvutia msomaji kununua gazeti lao. Wanafanya hivyo wakijua kabisa wapinzani wao nao wafanya kitu kama hiko japo hawajui habari gani wapinzani wao watakuja nayo. Hivyo kuna mambo kadhaa ya kuzingatia ili kujihakikishia gazeti lao litauzika kwa wingi na mwisho wa siku wapate mapato ya kutosha. Tuyaite magazeti yetu mawili maarufu yanayoshiriki ushindani huu majina yafuatayo; Nipashe na Mwananchi.
Tuanze kwa kuzingatia kwamba kila moja kati ya magazeti haya yana loyal readers ambao wao hawawezi kununua gazeti tofauti na moja kati ya haya. Yani wapo wasomaji ambao wao lazima wanunue Nipashe na si vinginevyo na wengine wao ni wasomaji wa Mwananchi pekee na si vinginevyo. Hivyo ushindani hapa utakua kuwapata wasomaji ambao watanunua kulingana na habari itayowavutia zaidi katika ukurasa wa mbele.
Unakumbuka siku mwili wa Ruge ulipotua Bongo?
Unakumbuka pia hiyo ndio ilikua siku Mhe Lowasa kurudi CCM?
Gazeti gani kati ya Mwananchi na Nipashe liliuza zaidi kwa kutanguliza habari moja kati ya hizo mbili ikizingatia kuwavutia zaidi wasomaji wake?
It was not a randomly selection, but it was a strategic selection after considering the move of competitors, but how?
Ili kujihakikishia kutokukosa mfululizo wa Makala hizi niandikie kupitia email yangu smbondela@hotmail.com kwa ajili ya kukuweka katika Database yangu ya wasomaji wa Makala zangu. Hivyo utakua miongoni mwa watu wa kwanza kupata Makala mpya inayotoka kila wiki siku ya jumamosi. Na kama ulikosa jumbe za mwanzo usisite kunijulisha ili nikutumie ujue wapi tulipotokea katika safari yetu hii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
UJUMBE WA TATU

Na Saidi Mbondela.

Salaam,

Shukrani kwa mara nyingine tena kwa kutumia muda wako kusoma ujumbe wangu, wewe ni mtu muhimu sana kwangu na nayathamini sana maoni yako. Wapo wadau wanaoshauri niandike kuhusu kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine kutokana na haja iliyokuwepo. Lakini niseme tu, Huu ni mfululizo na muda wa kuelezea kuhusu kujiajiri na kutengeneza ajira utafika. Tunahitaji kujenga uzoefu wa kazi kwanza kabla ya kujiajiri hivyo ni vizuri kuanza kwa kuajiriwa tena na bosi mzuri atayekua tayrai kushea uzoefu wake wa kazi nawewe ili ujiimarishe zaidi kisha baada ya hapo ndipo utaweza kujiajri kwani utakua tayari ushajua kazi inafanywa vipi pia utajua soko lipoje na linataraji nini kutoka kwako kama mjasiriamali.

Katika ujumbe wangu wa pili nilijaribu kuelezea negative attitudes za baadhi ya vijana wanaodhani wanastahiki kipato kikubwa mwanzoni kabisa mwa ajira zao kabla ya kupanda mbegu ya vipato hivyo. Hatua za awali kabisa kabla ya kuonesha ufanisi wake kazini anahitaji alipwe 1M+ in my opinion it’s ridiculous na atapata tabu sana kumpata mwajiri atayekua tayari kumlipa kiasi hiko kabla ya kuhakikisha kama kweli anastahiki. Zingatia kua hapa naongela ile hali ya kawaida katika soko letu la ajira.



Tayari tushalijua tatizo , je tunalitatuaje?

David Schwartz, PhD katika kitabu chake The Magic of Thinking Big ameelezea namna Service first attitude inavyoweza kukusaidia kupata pay raise ikiwa ni mfanyakazi au ongezeko katika faida ikiwa wewe ni mjasiriamali.



Elewa ya kua kabla hujaanza kuvuna pesa lazima kwanza upande mbegu zake na kwa hapa mbegu ni huduma utazoweza kuzitoa kwa weteja wako. Pesa zipo mifukoni mwa watu na ili mtu akupe pesa yake inabidi apokee huduma/bidhaa yako kama alivyoitaraji au zaidi ya matarajio yake. People are willing to pay for a product or service as long as it satisfy their needs, customer satisfaction is the key here. Let satisfaction exceed the cost incurred. Let him/her feel that he/she deserves to pay you more for what he/she has received.



Panda mbegu kwanza; boresha huduma yako, onesha umuhimu wako katika kampuni kwa kutoa huduma bora kwa wateja wenu ili bosi wako aone kweli unastahiki kuongezewa mshahara kwani utakua unamtengenezea mapato ya kutosha hivyo bila shaka utafanikiwa kuufikia mshahara uliokua ukiuhitaji bila ya kutumia nguvu. Lakini ikiwa hufanyi kampuni ipate mapato zaidi vipi wewe ulipwe zaidi? Let service first attitude be your policy on everything you do. Definitely it will pay you sooner or later.



David Schwartz ametoa mfano halisi aliowahi kuushuhudia unaotia nguvu dhana ya huduma kwanza pesa baadae; wakati alipokua akifanya safari zake kwenda mji flani nje kidogo ya alipokua akiishi, njiani husimama katika moja ya sheli miongoni mwa nyingi zilizopo pembezoni mwa barabara kwa ajili ya kujaza mafuta. Tofauti ya sheli hiyo na zingine ni kwamba kila mara anapofika hapo lazima akute magari mengi yamepanga foleni yakingojea huduma wakati zipo sheli nyingine pembezoni mwa barabara hiyohiyo ambazo zinaonekana hazina wateja kabisa.

Huduma gani ya tofauti wanayotoa hawa jamaa inayowatofautisha na wengine?



Alipochunguza akagundua hawa jamaa wanatoa huduma bora na zaidi ya matarajio ya wateja wao. Ilipofika zamu yake kujaziwa mafuta, mmhudumu alimuomba amsafishie gari yake sehemu ya ndani huku kusafisha nje ikiwa ni kama sheria kwa kila mteja wao. Hivyo gari litalojaza mafuta katika sheli hii linapata huduma zaidi ya ile iliyokusudiwa na hili ndilo lililokua likiwavutia wengi pamoja na kua wanatumia muda mrefu kwenye foleni. Siku zijazo kwenye darasa za marketing nitakwambia kwanini walikua tayari kusubiri kwenye foleni wakati sheli zingine zilikua tupu.

Jamaa wamepanda mbegu; huduma bora kwanza, kisha pesa baadae, Schwartz anasema alikua kila mara apitapo kwenye barabara hiyo lazima asimame katika sheli hiyo kwa ajili ya kupata huduma, tena hupata huduma zaidi ya alivyotarajia. Bila shaka katika hali kama hii mavuno yake huo ni maradufu. Customer satisfaction must be your policy. Put Service first attitude and money will take care of itself.



Kwa mfanyakazi anaetaka kuongezewa mshahara, fanya kazi kwa bidii, boresha huduma za kampuni yako, wafanye wateja wenu wapate zaidi ya wanavyotaraji kutoka kwenu. Wafanye wapende kununua bidhaa zenu zaidi kushinda mapenzi yenu ya kuwauzia wao. Na kwa Dear Arafat Abdallah,Dear Arafat Abdallah,Dear Arafat Abdallah,ArafatDear Arafat Abdallah,kufanya hivyo bila shaka utakua umepanda mbegu, mbegu ambayo kesho itazaa matunda, mteja huyu kesho atarudi lakini safari hii hatorudi peke yake atakuletea na mteja mwingine na mwisho wa siku mapato ya kampuni yenu yataongezeka na hapo your bargain position with your boss will become stronger. Hapa pia ninalakukwambia kuhusu bargaining. Endelea kusoma maandiko yangu. Kila siku wateja wenu wanapokuja wape huduma ya ziada tofauti na ya jana. Avoid to be predictable, remember your competitors are always watching your strategies and they will try emulate your strategies.

Nisirefushe sana maneno katika hili, muda utafakia wa kuyazungumza haya kwa urefu sasa tuendelee na kujifunza skills muhimu zitazokufanya uajirike kirahisi baada ya kuhitimu.







Kama ulisoma vizuri ujumbe wangu wa kwanza nilisema kabla ya kuhitimu tazama soko linahitaji watu wa aina gani ili uanze kujiandaa mapema kwa kuzijenga juzi hizo ili uweze kujiuza kwa haraka mara tu utapohitimu.

Katika Makala ya wiki inayokuja nitaanza kukutajia ujuzi wa aina gani na kwa sababu ipi utahitajika kua nao ili uendane na soko la ajira la sasa.

Nafanyia kazi maombi yenu ya kutoandika ujumbe mrefu utaowachosha kusoma.

Your gratification is my pride.

I’m trying to be lucid and eloquent just for you my reader.



Ili kujihakikishia kutokukosa mfululizo wa Makala hizi niandikie kupitia email yangu smbondela@hotmail.com kwa ajili ya kukuweka katika Database yangu ya wasomaji wa Makala zangu. Hivyo utakua miongoni mwa watu wa kwanza kupata Makala mpya inayotoka kila wiki siku ya jumamosi. Na kama ulikosa jumbe za mwanzo usisite kunijulisha ili nikutumie ujue wapi tulipotokea katika safari yetu hii.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom