orangutan
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 757
- 773
Asalaam Alaykum,
Mwanaume ukishafikia rika la umri wa makamo ndipo utakuja kugundua kwamba ulifanya jambo la msingi sana kumuoa mwanamke mwenye akili ya darasani na maisha kuliko mwanamke mwenye uzuri wa sura na muonekano tu.
Hii inakuja kudhihirika pale familia inapokuwa kubwa au ongezeko la majukumu ndani ya nyumba kiasi cha kukufanya wewe mwanaume kuelemewa na majukumu yako. Na hapo ndipo utakapoona umuhimu wa mwanamke huyu mwenye kujielewa kichwani.
Inaweza ikatokea mwanaume ukaumwa ghafla, ukapata udhuru wa safari ya muda mrefu mbali na familia na biashara zako, au wakati mwingine ushauri tu kutoka kwa mwenza wako kuhusiana na namna ya kuyaendesha mambo ya kifamilia.
Tafuta mwanamke anaweza kukushauri biashara zako, kupangilia familia, kusimamia baadhi ya miradi midogomidogo ya familia na mwanamke mwenye uwezo wa kufanya maamuzi mengi bila kusimamiwa au kuelekezwa na mume.
Ukifanya hivyo ndipo utakaposhuhudia firsthand ile kauli ya kwamba 'kwa kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke nyuma yake.' Ukifanya viceversa- ukaamua kumuoa mwanamke mwenye makalio makubwa, mwenye muonekano mzuri na uwezo wa kujiremba huku ukipuuzia reasoning yake na akili yake kimaisha- basi mpendwa jiandae tu kisaikolojia kuishi maisha yenye stress za kutosha na kesi zisizoisha ndani ya nyumba.
NB: Sijasema kwamba tusioe wanawake warembo, ila nimeshauri kigezo cha uwezo wa akili ya mwenza wako iwe kigezo cha kwanza kuamua kumfanya mwanamke huyo awe mkeo wa maisha. If she is beautiful and intelligent the better.