Botswana waichana live USA

Botswana waichana live USA

hans2014

Senior Member
Joined
Oct 4, 2014
Posts
112
Reaction score
99
8aba582885e0617792a3b6e467b47f52.jpg


Kungekua na maraisi watano kama wa botswana TRUMP angonyooka na kuona waafrika wa sasa sio wale waliochukuliwa utumwa

Huwezi kuziita Africana country "shithole" halafu baadhi ya maraisi wanakaa kimya yaani kwa kiswahili cha kawaida "nchi za africa ni shimo la choo" huyu TRUMP lazima apimwe akili


=======

Serikali ya Botswana imemshutumu Rais wa Marekani kwa kusema mataifa ya Afrika ni "machafu" na kusema tamko lake rais huyo ni la kukosa kuwajibika, la kukera na "ubaguzi wa rangi".

Bw Trump alisema hayo alipokuwa akizungumzia sera ya uhamiaji ya Marekani, ambapo alisema anafikiti watu kutoka Haiti, El Salvador na nchi za Afrika hawafai kuruhusiwa kuingia kama wahamiaji Marekani.

Botswana imesema kupitia taarifa kwamba imemwita balozi wa Marekani nchini humo kufafanua iwapo Marekani inachukulia taifa hilo la kusini mwa Afrika kama "taifa chafu" na taifa la mabwege.

Taarifa hiyo ya Botswana imesema tamko la Trump ni la kukosea heshima taifa ambalo lina urafiki wa kufana na uhusiano wa kibalozi.

Botswana imeitaka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika Sadc pamoja na Umoja wa Afrika kushutumu tamko hilo la Trump.

Bw Trump kwenye Twitter hata hivyo amejitetea na kusema hakutumia maneno hayo, lakini akasema aliyoyasema yalikuwa na "lugha kali".

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema tamko hilo la Trump ni la kushangaza, la aibu na la ubaguzi wa rangi.

Rupert Colville amesema: "Iwapo yatathibitishwa, matamshi haya ni ya kushangaza na ya aibu sana kutoka wka rais wa Marekani, nasikitika kwamba hakuna maneno mengine ya kueleza hili ila kusema kwamba ni ubaguzi wa rangi.

Bw Colville amezungumzia hotuba ya Trump wakati wa kampeni 2016 ambapo alisema wahamiaji kutoka Mexico ni wahalifu na wabakaji.

Na pia, amerejelea tamko lake akijibu maandamano ya waandamanaji watetezi wa ubabe wa Wazungu mwaka jana yaliyokumbwa na vurugu Charlottesville, Virginia walipokabiliana na waandamanaji waliokuwa wanawapinga.

Trump wakati huo alisema "pande zote" zilifaa kulaumiwa.

Afisa huyo wa UN amesema tamko hilo la Trump linaenda "kinyume na maadili ambayo ulimwengu umekuwa ukiazimia kufikia" tangu mwisho wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, na kufungua "mlango wa kuonyesha ukatili zaidi wa binadamu".

Trump alikuwa akizungumza na wabunge siku ya Alhamisi katika afisi yake ndani ya Ikulu ya Whitehouse kulingana na gazeti la The Washington Post.

Image captionWaandamanaji wanaopinga chuki ya rais Donald Trump dhidi ya wahamiaji

Alisema: ''Kwa nini tunawaruhusu watu hawa kutoka mataifa 'machafu'"?

Tamko hilo lilidaiwa kuwalenga watu kutoka Afrika, Haiti na El Salvador.

Ikulu ya Whitehouse haikukana tamko hilo ambalo lilithibitishwa na vyombo vyengine vya habari.

''Wanasiasa fulani wa Washington hupendelea kupigania mataifa ya kigeni, lakini rais Trump atawapigania raia wa M arekani pekee,taarifa iliotoka katika msemaji wa Ikulu Raj Sha ilisema.

Iliendelea: „Kama mataifa mengine ambayo yana wahamiaji wanaofaa kuwa nchini humo, rais Trump anapigania suluhu ya kudumu inazofanya taifa hilo kuwa thabiti kwa kuwakaribisha wale ambao wana mchango katika jamii ,hukuza uchumi wetu na kuingiliana na raia wa taifa letu.

„Kamwe hatakubali mkakati wa muda mfupi ulio hafifu na hatari ambao unahatarisha maisha ya raia wa Marekani, mbali na kutowaruhusu wahamiaji wanaotaka maisha mazuri Marekani ijapokuwa kupitia njia halali."

Matamshi hayo ya rais Trump yanajiri huku wabunge kutika vyama vyote wakimtembelea kupendekeza mpango wa wahamaiji usiopendelea upande wowote.

Seneta wa Democrat Richard Durbin alikuwa akizungumza kuhusu vibali vya muda wa kuishi vinavyotolewa kwa raia wanaotoka katika mataifa yaliokumbwa na majanga, vita ama milipuko ya magonjwa, vilisema vyombi vya habari.

Kulingana gazeti la Washington Post , bwana Trump aliwaambia wabunge kwamba Marekani badala yake inachukua wahamiaji kutoka Norway, ambayo waziri wake mkuu alimtembelea rais Trump siku ya Jumatano.

Seneta Lindsey Graham, ambaye ni mwanachama wa chama cha Republian kutoka Carolina Kusini pia alikuwa katika mkutano huo lakini hakuweza kuzungumzia kuhusu matusi hayo yaliotolewa na rais Trum.

Gazeti la The New York Times liliripoti miaka mitatu iliopita kwamba bwana Trump alisema kuwa raia wa Haiti wote wana ''ukimwi'' wakati wa mkutano wa mwezi Juni kuhusu wahamiaji.

Na kufuatia matamshi hayo rais Trump hakusazwa katika mitandao ya kijamii.

Elijah Cummings, mbunge wa Democrat katika eneo la Maryland alichapisha ujumbe katika mtandao wa twitter akisema: Nayashutumu matamshi hayo yasiosameheka na yanayoshusha hadhi ya afisi ya rais.

Mbunge mwengine mweusi kutoka chama cha Democrat. Cedric Richmond, alisema matamshi ya bwana Trump ni dhihirisho tosha kwamba sera yake ya kuliimarisha taifa la Marekani ni sawa na kulifanya taifa la Marekani kuwa la watu weupe pekee.

Mia Love, raia wa chama cha Republican katika eneo la Utah ambaye pia ni mbunge wa pekee mwenye mizizi ya Haiti nchini Marekani amemtaka rais Trump kuomba msamaha kwa maneno hayo yalio na chuki na yenye kugawanya watu.

Muungano unaopigania haki za watu weusi NAACP ulimshutumu rais Trump kwa kuzidi kuegemea katika ubaguzi wa rangi.

Lakini Ikulu ya Whitehouse imepuuzilia mbalia shutuma hizo zinazomkabili rais.

Afisa mmoja wa Trump alinukuliwa na chombo cha habari cha CNN akisema: Ijapokuwa hili litawakasirisha watu wa Washington, wafanyikazi wanadhani kwamba matamshi hayo yanatokana na mizizi yake, sawa na matamshi yake dhidi ya wachezaji wa NFL waliopiga goti wakati wa kuimbwa kwa wimbo wa taifa.

Msemaji wa ubalozi wa El Salvador mjini Washington alikataa kuzungumzia kuhusu matamshi hayo.

Chanzo: BBC
 
Kwani amekosea wapi?

Nchi za Afrika ni shimo la choo.

Kama unaweza kupita barabarani na kuona vinyesi vikitapakaa barabarani na mitaroni baada ya chemba kutibuliwa kuna tofauti ipi na shimo la Choo?

Mfano mzuri ni jiji la Dar es Salaam.

Kuhusu Waafrika kuwa Watumwa, bado Waafrika ni Watumwa, ila utumwa wa leo si wa kutobolewa miguu na kuvishwa minyororo.

Tuna utumwa binafsi wa fikra, kisha vijana na wazee wa kiafrika ni Watumwa mpaka katika makampuni na viwanda vya wahindi.

Kama watu wanatoil asubuhi mpaka jioni na kusweat haswa katika kiwanda cha nguo cha muhindi na kulipwa sh. Elfu 80 kwa mwezi si utumwa?
 
8aba582885e0617792a3b6e467b47f52.jpg


Kungekua na maraisi watano kama wa botswana TRUMP angonyooka na kuona waafrika wa sasa sio wale waliochukuliwa utumwa

Huwezi kuziita Africana country "shithole" halafu baadhi ya maraisi wanakaa kimya yaani kwa kiswahili cha kawaida "nchi za africa ni shimo la choo" huyu TRUMP lazima apimwe akili

trump yupo sahihi, mmezoe maneno yakulembwa

trump anasea ukweli kama unahasira ni wewe na mkeo mkalie chumbani kwenu

msubiri utawala democratic watawaficha, fyuuuuuuuuu
 
mbona mwaka 2015 mliitwa MALOFA mkanywea tena hapahapa nyumbani kwenu.Je Trump mtamfanya nini.Africans should be recolonizes for another 100 years aisee ile tujirekebishe.
Ni mim SHITHOLE (DODOMA)
Kwa sasa Zanzibar
 
8aba582885e0617792a3b6e467b47f52.jpg


Kungekua na maraisi watano kama wa botswana TRUMP angonyooka na kuona waafrika wa sasa sio wale waliochukuliwa utumwa

Huwezi kuziita Africana country "shithole" halafu baadhi ya maraisi wanakaa kimya yaani kwa kiswahili cha kawaida "nchi za africa ni shimo la choo" huyu TRUMP lazima apimwe akili




Mambo ya kipuuzi mashithole wanatoa tamko, vipi kuhusu Waafrika kuuzwa kama bidhaa karne ya 21? Kumlaumu Trump hakutufikishi popote, tudili na kwa nini Dunia nzima inatuona mashithole!
 
Trump ni mgonjwa kumbuka Ronald Regan
 
8aba582885e0617792a3b6e467b47f52.jpg


Kungekua na maraisi watano kama wa botswana TRUMP angonyooka na kuona waafrika wa sasa sio wale waliochukuliwa utumwa

Huwezi kuziita Africana country "shithole" halafu baadhi ya maraisi wanakaa kimya yaani kwa kiswahili cha kawaida "nchi za africa ni shimo la choo" huyu TRUMP lazima apimwe akili
hongera sana kwa kutafsiri yawezekana hawajui maana si unajua lugha hii........sasa wataweza nao kujibu to that extent
 
namuunga mkono trump maana mambo mengine hakuna namna...we fikili kuna watu hata mitaji ya laki moja tu, wanakosa lakini bajeti ya kuchaugua upya madiwani na wabunge wanao muunga mkono mtukufu ipo sasa kwa mambo kama haya trump asemeje sasa....hizi pesa za marudio ya uchaguzi wangepewa wajane na yatima si tungekuwa mbali sana
 
Trump yuko sahihi kabisa.nchi za Africa wanapenda mtelemko.badala ya kubaki Africa na kujenga nchi zetu watu wanaenda kujazana ulaya marekani.ndio maana south Africa na msumbiji walianza kuwatimua wahamiaji kwa mapanga.pia maneno ya trump ya kawaida sana.mbona sisi wenyewe Mara tunaitana wapumbuvu Mara karai.Mara nyumbu Mara malofa Hawa.
 
Botswana wananifurahisha sana.

Nimetoka kusema kwenye thread nyingine, nchi za Afrika zinatakiwa kufukuza hawa mabalozi wa Marekani na kuvunja uhusiano wa kibalozi na Marekani mpaka rais wa Marekani aombe radhi.

Aone kwamba Marekani hata kama ina nguvu vipi, nayo pia inategemea ushirikiano na nchi za ki Afrika katika vita dhidi ya ugaidi, biashara etc.

Afrika kwa sasa inaweza kirahisi sana kuamua kufanya biashara na Ulaya na China, ikaipotezea Marekani.
 
Back
Top Bottom