Boss mpya wa microsoft africa mashariki

Joined
Jun 3, 2014
Posts
28
Reaction score
16

​

Kampuni ya Microsoft imemteua Ms Mariam Abdullahi kuwa meneja wake wa Africa Mashariki kwa upande wa vifaa vya mobile. Sehemu kubwa ya idara ya vifaa vya mobile ya Microsoft inatokana na kampuni ya Nokia ambayo Microsoft iliinunua. Vifaa vya mobile vinavyouzwa na Microsoft ni pamoja na: simu za Nokia kama smartphones za Lumia, Nokia Asha na nyinginezo, vifaa vya michezo ya video (Xbox), na accessories zingine mbalimbali. Ms Abdullahi ataongoza timu za mauzo na matangazo ya bidhaa za Microsoft nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia. Anatarajiwa kuongoza jitihada za bidhaa za Nokia kupambana na washindani walioteka soko la Africa mashariki kwa sasa kama Tecno, Huawei na Samsung.

Ms Abdullahi ni mhitimu wa shahada ya sayansi ya kompyuta toka chuko kikuu cha Brunei Uingereza, mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 kwenye sekta ya ICT.

chanzo: http://www.bofyatz.com/2014/10/boss-mpya-wa-microsoft-afrika-mashariki.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ