kalamu na karatasi
Member
- Jul 26, 2015
- 49
- 30
Habari Wakuu
Katika maisha tunafanya mengi kwa kila mmoja kuamini ni haki yake kufanya afanyavo.
Kwa upeo makini wa mwanadamu akaenda mbali kwa kujiwekea miongozo mbalimbali.
Akaiita haki na wajibu,Kwa maana Yale anayopaswa kufanya kwenda kwa mwengine, na Yale anayopaswa kufanyiwa toka sehemu nyingine kuja kwake.
Lakini Mungu alietuumba nae hakuwa mbali katika kutupa miongozo ya kufuata katika Maisha.
Bora ya mambo kati na kati,Kwani hatuwezi sema usimkere mwezako kabisa maishani,ila isiwe ni kupitiliza.
Wakati unalia kudai haki yako ilio upande Fulani,Jiulize ni kwa kiasi gani nawe umetimiza wajibu wako?.
Tuna mifano dhahri juu ya hili hata kupitia vitu vituzungukavyo Maishani.
Leo chumvi n muhimu lakn ikizidi ni hatare,Maji yakikosa kwenye rejeta ya gari kila mmoja anajua nn kitatokea.
Basi vivo hivyo wastani katika kila jambo ni muhimu,Usiishie kusisitiza umuhimu wa heshma ilihali we mwenyewe hufanani na unachokihubiri.
Usitumie udhaifu wa upande mmoja kama fimbo ya kuchapia wengine.Bali weka mambo kati na kati.
Hili lijikite hata kwetu watumiaji wa mitandao ya kijamii,Tuna Uhuru wa kuandika na kushare fikra zetu lakini ni ule wenye mipaka.
Tukijikita kwenye kujibidiisha katika kujifunza juu ya Yale yenye natija nasi,Natumai itakua fursa kwetu kuakisi umaana wa bora ya jambo ni kati kwa kati.
Tusome na kutafakari vema kabla ya kufanya jambo lolote.
Tusisite kuuliza katika wale wenye dhamana juu ya jambo husika.
Na katika hili hatujachelewa,Kwani ni suala la kujipa muda na umuhimu zaidi.
Kalamu na Karatasi
(Chanzo cha Maarifa)