Bora ukawa waliotoka kuliko waliobaki

Bora ukawa waliotoka kuliko waliobaki

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,408
Kwanza naomba samahani nafikiri mtandao uko chini nimeshindwa kuweka haya katika maandishi yangu lakini nadhani ujumbe utafika.

kwa mchakato wa katiba unavyoenda nawapongeza sana UKAWA ingawa nao siwaungi mkono kwa asilimia zote kuliko waliobaki wanaojaribu kupotosha mfumo wa utawala wa nchi ili watanzania wachache waendelee kuwa mafisadi na kupora rasilimali za nchi, ili viongozi waendelee kutokuwa na maadili, ili wananchi waendelee kukosa haki mbele ya vyombo vyao. wapo mafisadi wakuu wanaowadanganya wananchi kuwa hatuwezi kupoteza mda kujadili mihimili ya utawala wa nchi kwa na kudai ni kupoteza kodi za wananchi na kudai wananchi wanataka kusikia ardhi, kusikia uchumi na mengine yanayowagusa.

Jambo la msingi hapa ni kujua kuwa hata ukiwa na mipango mizuri ya kiuchumi, afya na mengine lakini kama mfumo wa utawala ni mbaya mwananchi hawezi kupata lolote. Kwa mfumo tulio nao wa raisi kuteua kila kitu unasababisha wahuni kuunda vikundi vya kuatafuta madaraka na kumchagua mmoja wao akawanie nafasi ya juu. Akipata anawaleta wahuni wenzake kwa kuwateua kushika nyadhifa muhimu zote na nchi inaendeshwa kihuni. bila kuondoa mifumo hii Tanzania hata tupate kiongozi gani mzuri hawezi kutuletea maendeleo kwani vikundi hivi vya kihuni vinavyojulikana kama mitandao na majina mengine vina nguvu kuliko mtu mmoja hata kama ni kiongozi wa nchi.

Vikundi hivi ndivyo vinavyovuruga katika yetu kwa kujaribu kuzuia mifumo ya uwajibikaji, usawa na mifumo ya viongozi kuwatumikia wananchi isiwekwe katika katiba. Mambo muhimu katika katiba yetu ni swala la muungano lazima tuangalie ni mfumo gani unaokubalika kwa watanzania wa muungano. Kiongozi asiye na busara ndiye anayeweza kuingiza nchi katika machafuko kisa ni kutetea kile anachokiamini yeye. kama wananchi hawapendi muungano hata kama muungano unafaida nyingi kiasi gani faida hizo haziwezi kupatikana kwa watu wasioukubali. lakini jambo la pili ni kutenganisha mihimili ya utawala wa nchi kwa maana mahakama, serikali na bunge na kisha ukimaliza kuvitenganisha kwa kuondoa ushawishi wa chombo kimoja katika chombo kingine kufanya kazi zake (ushawishi huu unaweza kupitia upatikanaji wa fedha za kuendesha chombo au upatikanaji wa watumimishi na mambo mengine ikiwemo maslahi binafsi).

Tunatakiwa kubalansi nguvu za vyombo vya usalama. hapa vipo vyombo ambavyo lazima vitoke katika mikono ya serikali vyombo kama takukuru, tume ya maadili ya watumishi wa umma na ikiwezekana uongozi wa jeshi usiwe unateuliwa na raisi bali raisi yeye anaweza kuwa anamuapisha tu lakini viongozi wa mihimili ya nchi wanakutana kujadili mapendekezo ambayo kila chombo kinajadili na kupeleka mapendekezo na kufikia maamuzi ya pamoja na hivyo mkuu wa majeshi kuwa anapatikana kwa kuteliwa na vyombo vyote na si mmoja hivyo kutumia nguvu ya jeshi kulinda kiongozi mmoja anayemteua hata kama anafanya maasi kwa wananchi. mimi nafikiri ukimchukua mtu mwenye uzoefu akutengenezee kitu anatengeneza kwa uzoefu wake na uzoefu unaweza kuwa umejikita katika "corruption" na hili ndilo linalowakumba watanzania walio wengi wana uzoefu lakini hawana uzoefu katika kulisaidia taifa bali uzoefu katika kutumia fitina kupata madaraka, uzoefu katika kutumia ujanja kupora rasilimali za taifa, uzoefu katika kufoji matokeo sasa unawachukua watu hawa wakutengenezee katiba mpya unafikiri watafanya nini kama sio kutumia uzoefu wao huo tena wakiangalia kujiandalia makao.

Wengi wao hawana sifa bali wameingizwa wengine kwa rushwa zisizo za fedha, wengine kwa kujuana na makundi na kuweka mifumo mizuri ya utawala na uwajibikaji ni sawa na kukata matawi waliyoyakalia je ni nani yuko tayari kujiondoa mwenyewe katika mrija anaoutumia kunyonya taifa kama siyo kuondolewa.

Hatuwezi kupata katiba kwa mfumo huu bali katiba inaweza kutengenezwa na wataalamu na sio wanasheria tu bali kundi la wataalamu wa fani zote kukaa pamoja kusikiliza matakwa ya wananchi na kuiandika katiba kitaalamu kuweka mifumo ya kuwasaidia wananchi kupata kile wanachokitaka. mfano wananchi wanaweza kudai maswala ya uchumi yaingie katika katiba, ukimchukua mbumbumbu atapendekeza kuwepo na kifungu kinachozungumzia uchumi katika katiba lakini kwa mtaalamu ataangalia jinsi gani mfumo wa serikali unaathili uchumi, ataangalia ushiriki wa wananchi na wataweka mifumo ya kuwezesha uchumi kukua bila hata kutaja uchumi katika katiba.

Mbumbumbu anaweza kuweka kifungu cha kuzungumzia uchumi huku mfumo wa utawala unamuweka fisadi katika kuongoza kitengo cha uchumi au vyombo vya usalama vinafungwa na mifumo ya kiutawala ukimkata kigogo unaletewa memo au kufukuzwa kazi na hakuna chombo hata kimoja kinaweza kunyanyua mdomo kuhoji sasa kinachotakiwa katika katiba ni kutaja neon uchumi au ni kuweka mifumo ya kumuwezesha hata yule mdogo katika chombo cha usalama anaweza kumninginiza kigogo kama ana hatia na hakuna mpuuzi anaweza kuandika vikaratsi kutishia wala kunyanyua mdomo wote wakiogopana kulingana na mfumo ulivyo. tusitegemee mafisadi walioshikilia mifumo (bila kujali upande walipo) watuwekee mifumo mizuri bali katiba mpya ni wakati sasa wa kuweka mifumo ya utawala ambayo inafanya vyombo kutumikia wananchi na si matajiri wanaowapa sapoti viongozi au nafsi zao au mitandao yao
 
Lakini pia, muundo wa serikali ndiyo MOYO wa rasimu ya pili ya katiba, kama muundo unavurugwa, ni dhahiri kuwa rasimu nzima inakuwa haipo,
 
Lakini pia, muundo wa serikali ndiyo MOYO wa rasimu ya pili ya katiba, kama muundo unavurugwa, ni dhahiri kuwa rasimu nzima inakuwa haipo,

Si muundo wa serikali tu bali muundo wa vyombo vyote vitatu vya utawala wa nchi ni muhimu, mfano kwa nini wabunge na madiwani wasiwe chini ya chombo kimoja kinachoitwa bunge huku bunge likifanya kazi ngazi ya taifa na balaza la madiwani likifanya kazi ngazi ya wilaya. hapa namaanisha kuwa mbunge ndiye anakuwa msimazi mkuu wa serikali kwa ngazi ya wilaya lakini usimamizi huu una mwakilishi kwa kila kata. majumuisho ya vikao vyao katika wilaya ndio hoja ya wilaya katika bunge la taifa na sio mtu kutoka kwenye biashara zake anaenda kujadili mawazo yake. mbunge awe na ofisi na awe mkazi wa kufanya shughuli za kila siku katika wilaya. kwa serikali jambo la msingi mimi naona ni marekebisho ni mengi lakini muhimu kwangu kwa leo ni swala la kuunda MAMLAKA YA MIPANGO ambayo kwa mtizamo wangu hii inatakiwa kuwa kuwa ni malaka pacha na mamlaka ya kukusanya mapato (TRA). taasisi hizi mbili zinatakiwa ziwekwe chini ya waziri mkuu kwa maana waziri mkuu anatakiwa kuongoza wizara inayopanga mipango ya maendeleo ya kitaifa na kutoa mipango ya maendeleo ya mda mfupi na mda mrefu kwa taifa. taifa litekeleze program yake ya maendeleo na ilani za vyama ziwe ni kufafanua jinsi gani chama Fulani kinaweza kutufikisha katika malengo Fulani tuliyoyapanga. waziri apewe malengo ya kutimiza na sio kila waziri anapanga mipango ya kwake na anatekeleza ya kwake na kibaya zaidi watu wenyewe wanaangalia kupigiwa kura. Tunataka wataalamu wanakaa chini wanaangalia mwelekeo wa mapato ya nchi wanaweka mipango ya mda mrefu, fupi na kati ya miundo mbinu, huduma za jamii, kukuza uchumi na waziri husika anatengeneza mpango wa kutimiza unaurudisha kwa waziri mkuu na vitengo huko unachambuliwa na kuboreshwa na ukipishwa au waziri mkuu anaangalia mipango yote ya taifa kwa pamoja kwa kuangalia mapato na matumizi katika mda husika. mimi ningekuwa waziri mkuu mfano mwaka 2015 ningeagiza wizara kama ifuatavyo wizara ya miundo mbinu kufikia mwaka 2020 tunataka Tanzania iwe na master plan ya usafirishaji wa reli na meli inayounganisha kila kanda ya Tanzania na inayorahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria kutoka kanda moja kwenda nyingine na inayoweza kuchochea ukuaji wa utalii wa ndani na nje. kufikia mwaka 2025 tunataka Tanzania iwe imepunguza usafirisha wa mizigo na abiria wa safari ndefu kutoka usafiri wa barabara kwenda usafiri wa treni zinazokwenda kwa mwendo kasi kwa asilimia 60. Wizara ya makazi na ...... tunataka kufikia mwaka 2025 Tanzania iwe imeondokana na makazi holela kwa kuhakikisha kila mwananchi anajenga katika eneo lililopimwa kwa maana ya kuwa na ukubwa unaokubalika, kuwepo kwa mipango ya huduma ya jamii kwa maana barabara inafamika itapita wapi, umeme wapi, maji wapi, maeneo ya hospital na shule yanatengwa kwa kila eneo lenye ukubwa Fulani. (hapa nakuwa nategemea sio lazima wananchi waambiwe walipe milioni ngapi ili wapimiwe bali kwa kila kata inaweza kuandaa vijana ambao wanaweza kupewa mafunzo na halmashauri ambao wanaweza kushirikiana na serikali za viji au mitaa au kata kubainisha maeneo ya barabara kutenga maeneo ya viwanja katika kata kwa mpangilio na kwa ukubwa unaokubalika) lakini kwa wale wanaokuwa wana uwezo wanaweza kushughulikia kupima kupitia wataalamu wa halmashauri na halmashauri kuendesha program za upimaji. lengo tunataka miji iliyopangiliwa vizuri hata kama wananachi hawana hati lakini tuondokane na makazi holela na sio mpango wa sasa wa kuhalalisha makazi holela kwa kuwapa wananchi hati katika maeneo yasiyo na barabara au huduma za jamii lengo likiwa ni kuangalia kodi tu bila kuangalia maendeleo ya jamii kwa ujumla. kwa kifupi muundo wa serikali unaofanya viongozi kupanga majukumu na malengo na kuwa na nguvu ya kusimamia malengo hayo unahitajika sio unapewa uwaziri kwa sababu wewe ni rafiki wa raisi alafu kwenye wizara kuna taasisi ambayo raisi anateua rafiki yake mwingine kuwa chini yako unashindwa kumsimamia kwanza kwa sababu wewe hukupata kazi hiyo kwa sababu wewe ni bora bali kwa sababu ya urafiki hivyo lazima ulinde urafiki na si kutafuta ubora pili kwa sababu huyo mkuregenzi hakuletwa kwa sababu yeye anauwezo wa kuongoza taasisi vizuri bali raisi alimsaidia apate pa kulia sasa ukimuwajibisha unamchokoza raisi unabaki kimya hata kama unauwezo na unaona makosa. lazima tuondoe mazingira haya.
 
Back
Top Bottom