Bora angekufa baba kuliko mama

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,729
[N]Naileta kama nilivyoipata ili kuwakumbusha wanaume wenye tabia za kuwanyanyasa wake zao kuwa hawana nguvu kuliko MUNGU na ipo siku watafika huko.[/B]

"Juzi nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja na mkewe. Yeye na mkewe walifariki kwa ajali ya gari, wameacha watoto wawili mmoja wa miaka kumi na mwingine wa miaka minne wakike, mkubwa ni wakiume.

Sasa tukiwa kwenye ule msiba, mimi kama rafiki nilikua karibu sana na wale watoto kwani wananifahamu kama Baba mdogo, kusema kweli nilichokishuhudia kilinifanya nije nimpende mke wangu mara mia zaidi.

Kweli nampenda sana mke wangu lakini kuna wakati namchukuliaga poa nikiwa na mambo yangu najifanya kidume na ninamuudhi. Kwa siku tatu zote nilikua karibu na ile familia tukimalizia msiba, katika kipindi chote hicho watoto walikua wakimlilia Mama yao.

Yaani wakilala wakiamka ni kuniuliza, wananiita anko, Mama yuko wapi (Mara nyingi wnaaniita anko), wanamauuliza Bibi yao Mama yuko wapi. Sasa kilichonifanya nilie nipale ambapo mtoto mkubwa wa miaka kumi ambaye anaelewa kitu kidogo alikua anampembeleza mdogo wake alikua anamuambia.

“Usilie Mama kaenda sehemu nzuri, kaenda kupumzika kwa Mungu na Malaika…” Mdogo wake ndipo alipouliza Baba na yeye, akasema “Amemsindikiza Mama watakaa huko na mimi ndiyo nitakulinda, usiogope nipo hapa. Unakumbuka siku ile Mama alivyotuambia twende kwa Bibi kukaa wenyewe…”

Alimuuliza… “Mimi si nilikulinda…nitakulinda na sasa…Mama anatuangalia lakini sisi hatumuoni….” Kama hapo umelia basi subiri majibu ya yule mdogo wake. Huku akijaribu kujizuia kulia alimuuliza Kaka yake.

“Sasa kama Baba ameenda na Mama si atampiga tena, mimi sitaki Mama apigwe, kwanini asingeenda baba peke yake….???”

Nilianza kuwaza namna ambavyo rafiki yangu yule alikua akimnyanyasa mkewe, namna alivyokua akimpiga na kumsimanga, nilishaongea naye mara nyingi lakini hakujali.

Lakini alikua anawapenda watoto wake na kila siku aliwadekeza ila hawakumkumbuka. Jibu la kijana wake ndiyo lilinifanya niamini kuwa wanadamu si chochote. “Huko hawezi kumpiga, Mama ameenda kwa Mungu, huyo ana nguvu zaidi kuliko Baba. Akimsogelea tu atamchanachana kamakaratasi! Mungu ana upendo hapigi watu wema kama Mama!”

Hapo yule mtoto alikua akiongea kwa uchungu lakini kwa hasira na kwa imani kabisa. Sikuweza kuendelea kuvumilia kuwasikiliza, niliwaacha na kwenda kumuangalia mke wangu, nilimkumbatia na kumuuliza “Mke wangu hivi na mimi nakunyanyasa?”

Aliniangalia kwa mshanagao, aliniuliza kwanini unasema hivyo, nilimuambia hapana niambie tu. Niambie kama kuna kitu nakifanya kinakukwaza ambacho watoto wangu watakiona. Nilimuambia

“Nataka wanangu waniulizie nikifa, sitaki wanangu wafurahie kifo changu.”

Mke wangu alinikumbatia huku akitokwa na machozi aliniambia “Hakuna mume wangu, wewe ni mume bora, sema uache tu kuweka soksi kwenye makochi na kuacha sahani kitandani.” Nilijikuta natabasmau kidogo, kwani mke wangu alikua na furaha.

Sasa hivi najifunza nisiache soksi kwenye makochi wala sahani kitandani. Najua alikua anatania ila kama kinamkera nitaacha, maisha hapa duniani ni mafupi, watoto ndiyo kitu tunaacha kwaajili ya kututambulisha, sitaki wnaangu wanaitambue kama Baba mkatili."
 

Hahahaahahahaha!!!
 
Mkuu umenikumbusha mengi,duniani ni mapito ila tusiache mabaya kwa watoto wetu.
 
Aisee inauma na inafundisha ni ukweli kabisa watoto wanajenga sana chuki
Nina mdogo wangu hampendi baba yetu ingawa ameshafariki zaidi ya miaka 10 sasa hivi ni binti mkubwa karibia miaka 25
 
Umenitoa machozi....!!
 
kweli mkuu kuna familia nafahamu watoto wanaomba baba yao afariki kila siku lakini afi zaidi sasa mama yao kapata sukari na presha kisa huyo baba yao chuki imezidi mara 100 na wanaona kabisa mama yao atafariki lakini baba atabaki wapo kama wamejipanga kumyanyasa baba yao...

nyingine mama kafariki watu wazima kila mtu na falimia yao ilibidi ukoo ukae usuluhishe baba apewe matunzo sababu wanadai baba yao ndiyo sababu ya mama kufa mapema kisa mateso aliyokuwa anampa....

nyingine baba alifariki kiukoo wetu watoto ndiyo wanatakiwa watoe sanduku kama heshima kwa mzazi walikuwa wanabisha na kutaka wao watoe chakula sanduku watoe wanaukoo ilibidi msiba uchukue wiki mama yao akijidai alishamsamehe mumewe na ana amani kabisa japo ule msiba sikusikia hata mtu anakohoa .. mkewe mwenyewe akulia alikuwa anatoa maelekezo tu azikwe wapi na avae nini? anatumbukizwa kaburini watu hulia yani akatokea mbibi huko hakuna anayemjua akapiga ukunga pale ndiyo tulisikia kilio kama igizo vile...

watoto wanagundua mapema sana pale nyumba inapokosa amani na hujenga chuki hata wakiwa watu wazima vipi hili nimeliona usiombe kisasi cha watoto........

nb: hata wamama wapo watesaji
 
Umenitoa machozi....!!
Pole sana Msweet! Swali la kujiuliza "Ni nini nafasi ya wanaume katika familia ya ulimwengu wa kileo"?

Wewe mwanaume utasubiri hadi lini, nawe wanao wakutambue kuwa upo, kwa wakati wote maishani mwao, au unabaki tu na kuishi katika dhana hasi kwamba wewe ni kichwa cha familia!.

WAKATI NDIO HUU WANAUME KUBADILIKA
 
Tuwapende wake zetu jamani.
Ila tatizo la wake wa kitanzania ukiwapenda na kuwaheshimu wanacheza hadi kichwani kwako,
Wanakuona ndondocha wa kushikwa pembe, kwamba amekupata, kaishika akili yako.
Yaani ukiwa mkali TZ wewe ndo baba, ukiwa mpole babu, tuheshimiane tafadhali.



$ Binadamu ukimwambia usipite huko kuna kinyesi mbele, atapita tu, akikutana na kinyesi ndo atajikuta kubadili njia, kutema mate na kukunja uso..
 
Ndo hivo wazazi wana impact kubwa sn kwenye maisha ya mtoto na ndo wanaongoza kuharibu maisha ya watoto...wazungu wenzetu wanajitahidi sn watoto wasione tofauti zao

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbaya zaidi unakuta wazazi wamekushape kwa maisha fulani ile time wanakuja kugundua hawakua fair wanaanza kukulinganisha na watoto wa wazazi wenzao.(et mbona flan yupo hivi ww sijui ukoje...kuwa kama fulani...)
Hii kitu ni mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…