Waungwana, niwashirikishe kwenye jambo ambalo huwa linanikera. Mara nyingi ninasoma watu wanabadilishana matusi makali hata ya nguoni kuhusu mambo mbalimbali. Aghalabu, wengi hujitambulisha kwamba wanajua zaidi na kuanza kwa kudai "wewe hujui."
Mtu atang'ang'ania jambo utadhani kwamba amelifanyia utafiti, kumbe kalisikia tu kwenye vijiwe. Na akisha lishika hivyo, huwezi kumwonesha ukweli akaukubali. Kwa mfano, nilienda ughaibuni, na niliporudi nilisimulia mambo fulani, na jamaa alinibishia wakati yeye huko hajawahi hata kwenda. Nikaambiwa pia kwamba sijui kitu.
Nilishuhudia pia siku moja mtu mmoja mwenye maneno mengi akiwaelezea watu kwamba mabanda tuliyoyaona karibu na barabara ni mabanda ya kufugia mbu wa utafiti. Lakini kijana wa kutoka kijiji kile aliposahihisha kwamba kwa hakika mabanda yale ni ya kuoteshea mimea maarufu kama greenhouses, jamaa aling'aka kwamba si kweli. Yeye anajua kwamba ni mabanda ya mbu.
Ushawishi wa vijiweni umekuwa tatizo kubwa sana hapa. Badala ya watu kuhoji mambo na kufanya makini kutafuta habari katika vyombo mbalimbali, wanapenda kurukia sifa za mitaani.
Tulipata kushuhudia sehemu kubwa tu ya wananchi wakifunga safari kwenda kwa Babu. Nakumbuka waandishi fulani walihoji busara na ukweli wa uganga huo. Walitukanwa vibaya. Washawishi wa vijiweni walishasema kwamba kuna uganga, basi hakuna kuhoji wala ubishi. Upepo sasa hivi umebadilika juu ya jambo hili.
Kutokuwa makini ndiko kunakoua upinzani wa kisiasa nchini. Watu badala ya kuhoji mambo, wanakimbilia ushabiki kulingana na mwenye kupiga kelele zaidi. Na kuna kautamaduni kanakokua ka kutotaka kuhojiwa. Mwaka jana ndiyo nilishuhudia kilele cha tatizo hili. Yeyote aliyehoji busara ya ubadilishaji wa gia angani aliandamwa kwa matusi na si hoja hata kidogo.
Matokeo yake sauti za busara na zenye kuhoji mambo zilizimwa. Wale waliotabiri kwamba CCM itarudishwa madarakani kwa sababu ya makosa hayo, walitukanwa vibaya na walipuuzwa kuwa au wametumwa na CCM au wafuasi wa mtu fulani. Na hatimaye tumeshuhudia tena yale yaliyotabiriwa ya ushindi wa CCM.
Demokrasi haiwezi kukua kwa ushabiki tu wa kikasuku. Demokrasia ya kweli inastawi katika mazingira ambapo watu wanakuwa na uelewa mzuri, wanajihabarisha vema na zinapopambanishwa hoja za pande mbalimbali.
Nawasilisha.