Bongo movie mko vizuri ila...

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,491
8,301
Heshima kwenu wanajamvi.
Nimesikia kilio cha waigizaji Bongo na jitihada zao za kutawala soko na kujipatia riziki halali. Kwanza poleni sana.

Pili ni ushauri tu,kama wewe ni muigizaji mzuri na wala siyo muuza sura inabidi ulitambue hili. Kitu gani hadhira inataka? Jifunzeni kwa taarab na dansi,kufanya maonyesho hai hii itapembua pumba na mchele na waigizaji wa kweli tu ndiyo watabakia kwenye soko.

Teknolojia inakimbia sana,hata TV karibuni zitapotea,hivo mauzo ya cd hayatakuwa na maana sana.Lakini kama unajua kuperform live utasurvive tu. Na pia watu wanapenda kusikia visa vinavyogusa maisha yao ya kila siku huku vikiwaelimisha/burudisha/asa. Muda wa kuishi dunia ya kufikirika umeshapita.
 
Hawa tusiwalaumu wala hayo maisha wamependa wenyewe baada ya kuisogelea siasa na kuanza kutumika majukwaani.

Wenzao wakina Rambo wamefanya kazi hadi sasa hawajachuja kwa sababu wanajua ubunifu wa kazi na hawahusiki na kitu kingine tofauti na sanaa yao kila kukicha wanawaza watatoa nini kipya cha kuteka fahamu za watu, leo b-movie anawaza ataitwa kwenye mkutano wa kisiasa saa ngapi.

Samahanini kumtolea mfano Rambo
 
Azam, Simba na Yanga mbona wako kimya? Game zao zilichezwa na zikiwa mubashara kwa TV huku game ya Maniyu na Chesii ikipigwa hawatulazimishagi kuangalia ya kwao bana.
 
Ni sawa sana,ila wakipotea itakuwa kero nyingine,jaribu kupitia profile zao kwenye fb uone maelimu wanayojipa,wakati wengi tunawajua ni std 7,sasa wasiponoa vipaji kuna mawili tu,1.kuongezeka vyangudoa,2, kuongezeka majambazi. Tuwape nasaha wakomae kwa faida yao kwanza,na taifa pia.
 
Back
Top Bottom