bongo fleva ziinaboa sana



Asante KOKU kwa maelezo yako mazuri, ninachofanya ndo hicho unachosema, ninajaribu kuchangia katika kuboresha vya kwetu kwa kutoa maoni yangu kama hivi, kama kuna mahala vya 'wenzangu' vimesifiwa humu labda ni kwa dhumuni la kutolea mifano tu.

Nakubali kwamba huwezi kumpendezesha kila mtu, lakini naamini pia kwamba watanzania huwa tunapokea kila kitu wheather ni kizuri au kibaya, kwa mfano ni kwa nini wasanii wa bongo star search hushinda baada ya kupigiwa kura na watanzania na baada ya hapo huwa hawasikiki tena, mara nyingine wale ambao hawakushinda ndio huendelea zaidi, kwa mfano Peter Msechu.

Nataka wa tz tuanze kuchagua, sio kukubalia kila kitu kwa kigezo eti ni cha kwetu, tuanze ku demand quality.

Kwa ujumla bongo fleva ni sanaa iliyolala, haina ubunifu isipokuwa kwa wasanii wachache sana na baadhi ya kazi zao.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…