Bongo Flava mkimaliza kum-copy Davido mtam-copy nani

Bongo Flava mkimaliza kum-copy Davido mtam-copy nani

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
58,053
Reaction score
134,365
Kiukweli vijana wetu wameishiwa ubunifu kiasi cha kutia mashaka makubwa sana.Elimu yetu imetujenga kutokuwa wabunifu.Ni masikitiko makubwa kabisa kuona mitoto hii inaiga kila kitu toka west africa, sijui kama wanapata kufikiri wenzao kina davido wanaiga kwa nani.

Mbaya zaidi hata ujumbe hakuna ni mikelelee tuuuh hakuna cha maana tena.Watu wa kulaumiwa pia ni hawa wanaojiita wadau wa music hasa Clouds ent.Kina Sugu. Jay Moh, Watengwa, japo waliiga toka Marekani lakini kuna kitu walijitahidi kuifundisha jamii.

Waliitia jamii ujasiri sasa nyie mitoto muwaambie kabisa mashabiki wenu mkitoka kumuiga Davido mtamuiga nani,ili waanze kabisa kumsikiliza mtakaye muiga ili kupima kama mtamuiga vizuri
 
Hivi kumbe huwa unasikiliza bongo fleva!!!! ndo maaaaaaana................ovyo.
 
Yaani umenena.

Mie kuna nyimbo beats zake uwa nasema si bora nisikilize za west.

Inabidi wawe wabunifu kwa kweli hata kuwa na bendi zao.

Kwani kuna shule ya muziki Tanzania? Kama zipo ni ngapi?
 
Back
Top Bottom