Bomu la tatu tanzania lalipuka

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
814
380
Wana jamvi, nimekuwa nafuatilia kwa makini sana siasa za nchi yetu na hasa mwenendo wa Serikali ambayo ndiyo kimbilio la wanyonge na watanzania waliowengi, lakini matokeo yake imekuwa ni kupigwa mabomu tu, kama yanavyojieleza hapa chini.

1. BOMU LA 1 - Tumeona Serikali yetu ikipoteza uwajibikaji uliotukuka, watendaji wakuu na wasaidizi wao na wale wa kawaida, wamegeuza serikali kama ni kijiwe cha kujipatia mali na ni kwa ajili ya kundi fulani la watu. Hii imetuingiza ktk mtikisiko mkubwa wa kiutendaji na kiuwajibikaji, ambapo, matokeo yake ni kuwa na Serikali isiyowajibika. Serikali imegeuzwa kuwa shamba la bibi. Sasa kama tunaserikali isiyowajibika, ni sisi wanyonge tunakimbilia wapi? Yapo mengi ktk hili, tunaweza kuyaongezea.

2. BOMU LA 2 - Matokeo ya BOMU la kwanza, yametrigger na kufyatua bomu la pili ambapo Jeshi letu la Polisi, limepoteza weledi. Kwa kiasi kikubwa sana jeshi limekuwa si la kulinda usalama wa raia na mali zao tena badala yake limegeuka kuwa kijiwe cha watu kujipatia pesa na mali zilizochafu, kunyanyasa wanyonge na hasa wanaodai haki zao za msingi, limenunuliwa na kundi la wahalifu (Mafisadi) na kutekelezza matakwa yao, kusaidia biashara haramu, na kushirikiana na makundi ya (ki-mafia), Tanzania ya leo, imekuwa ya kiujanjaujanja tu, yaani wale ambao ni wahuni na washenzi ndio wanaonekana watu wa maana na kutukuzwa na jeshi letu la polisi, lakini wale wenye busara zao wamekuwa maadui wa polisi. Polisi imegeuka kuwa kama soko, ambapo wanyonge wanaenda kununua haki zao. Kama huna pesa, hupati huduma stahili ktk jeshi letu la polisi. Sasa wanyonge tukimbilie wapi? Nafahamu si askari wote ktk jeshi hilo la polisi wako hivyo, ila hao baadhi wamechafua taswira nzima ya jeshi la Polisi, narudia wanyonge tukimbilie wapi? Unaweza ukajua mengine na kuongezea hapa.

3. BOMU LA 3 - Bomu la tatu ambalo ndilo lilibaki kuwa tegemeo la mwisho la mlalahoi, ni Mahakama zetu. Siku hizi mahakama ipo ktk sydicate ya mradi wa watu kutengeneza pesa, haki haipatikani mpaka kwa pesa, baadhi ya mawakili, mahakimu, majudge na ma broker, wametengeneza mtandao wao wa kupata pesa katika haki halali za mlalahoi mnyonge mtanzania. Mahakama zimeanza kuonyesha waziwazi kutumiwa na Serikali iliyoshindwa kuwajibika kwa watanzani kukandamiza haki ya wanyonge. Ikiwa kama mahali tulipopategemea patatoa haki ya msingi kwa raia mnyonge wa Tanzania pamebadilika na kutumiwa kwa maslahi ya kundi fulani na kutumika kama mahali pa kuchumia pesa, nauliza tena wanyonge walalahoi watanzania tukimbilie wapi?

Wanyonge tumebanwa kila mahali, hatuna pa kukimbilia, ni kama vile umefunga milango na madirisha ya chumba unaanza kumpiga Paka, nadhani jibu lake kila mtu analifahamu na hata viongozi wetu wanalifahamu.......Nauliza tena, Serikali, Polisi na Mahakama, mmetutosa wanyonge watanzania tukimbilie wapi??? Tunaomba majibu yaliyojitosheleza na mjipime wenye dhamana hizo.

 
Back
Top Bottom