VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Wakili Msomi Tundu Antipas Mughwai Lissu ameacha mwangwi kwenye Mkutano wa Mawakili-AICC Arusha. Ameonesha jinsi asivyotetereka na kusimamia anachokiamini. Amethubutu kusema na kuwaita Mawakili 'waoga' na watetezi wa vibovu.
Katika moja ya michango yake,Wakili Lissu alimuumbua Jaji Dr.Feuz Twaib(ambaye pia Mwalimu Shule ya Sheria ya Tanzania na Wakili) kwa kumwambia kuwa punde tu,miezi michache iliyopita,aliandika hukumu 'mbovu' na isiyostahili ambayo 'imechanwachanwa' na Majaji wa Mahakama wa Rufani na kutupiliwa mbali.Hukumu a Jaji Twaib ilikuwa ni kwenye kesi ya Yusuph Manji dhidi ya Kampuni moja ya Saudi Arabia.
Uchunguzi wa nyaraka za Wakili Tundu Lissu unaonesha kuwa katika kesi hiyo iliyokuwa mbele ya Jaji Rugazia wa Mahakama Kuu,pande husika za kesi zilikubaliana nje ya Mahakama( Settlement out of Court) na Jaji Rugazia akaridhia makubaliano hayo na kuyafanya Amri ya Mahakama. Ni utaratibu unaokubalika kisheria.
Siku si nyingi,Wakili Majura Magafu alijitokeza Mahakamani,kwa niaba ya Manji kuomba Marejeo(Review) ya Makubaliano hayo. Kisheria, Marejeo hufanywa na Jaji aliyeamua kesi husika.Jaji Twaib anajua hilo fika. Jaji Twaib,akiwa hausiki na Amri ya mwanzoni,alitengua Makubaliano ya pande za kesi. Akafanya 'blanda'. Akafanya jambo haramu kisheria.
Wakili Lissu hakuogopa uwepo wa Majaji na Mawakili Waandamizi kama vile Jaji Dr.Feuz Twaib,Prof. M.K.Wambali,Jaji Joseph Sinde Warioba,Jaji Mstaafu Thomas Mihayo,Jaji Victor Makaramba,Wakili na Rais wa Mawakili Tanganyika Francis Stolla na wengineo. Mkutano ukageuzwa Semina. Lissu akatoa mafunzo thabiti.
Aliposimama Jaji Twaib, ambaye alionekana mnyonge, aliwaomba Mawakili waende wakaisome hukumu husika na kujiridhisha na tuhuma za Lissu.Katika siku nilizojiona sina maana katika jamii hii,siku hii ya Lissu inaoongoza. Wakili Lissu akanifanya nirudi Dar kwa basi badala ya ndege kama nilivyopanga.