Bomu la elimu limeshalipuka bado la afya

Bomu la elimu limeshalipuka bado la afya

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
6,067
Reaction score
2,229
Katika moja ya sababu za msingi ambazo hazijatajwa kuchangia mporomoko wa elimu ni hili la walimu wa vodafasta.
Tukiamua kuanisha kiwango cha ufaulu wa walimu wanaotufundishia vijana wetu tutaona ni kwa jinsi gani tulijitegea bomu hili lililolipuka hivi karibuni.kiukweli walimu wetu hasa zile shule za st kayumba ni failures wa form six au hata form four.
Sekta ya elimu imekuwa kimbilio la ajira za waliokosa muelekeo badala ya vipanga.

Kwa sasa serikali ina kampango cha kuweka dispensary kila kata huku ikisahau kuboresha miundo mbinu na utaalamu katika hospitali ngazi za wilaya.
Sasahivi tunashuhudia maelfu ya ajira kwa wizara ya afya huku wengi wa waajiriwa wakienda huko bila vigezo kama ilivyo katika elimu.hii asilimia 26 ya form four waliopata daraja la nne utaikuta imeingizwa kwenye sekta hizi mbili baada ya miaka miwili hivi.

Ni swala la muda tu tutashuhudia maafa ya sekta ya afya halafu tutaanza kutafuta visingizio!
 
marekani wakisitisha uhisani tutaona vifo vya wachanga na kina mama kwa kasi,nguvu na ari zaidi.
 
Afu litafuata la Ajira kwa vijana, hili ndo litakuwa balaa
 
Hata upande wa afya mambo siyo mazuri mkuu........... mpaka maaskofu wanakufa unadhani ni mchezo!
 
Mlipeleka Ikulu mcheza ngoma leo mnalialia kama ndama wakiwa tulieni nyie ndomana juzi akawa anawakejeli kwa viswali vya kiingereza ugoko eti "Nani asiyejua Kimaraa hamna maji?Nani hajui hamna reli?"Utadhani alichaguliwe ili aue reli,maji na kufelisha form four....Sasa ndo mtatia akili katika yafuatayo
1.Mtajua kuwa Rais mislamu ni janga
2.Wacheza ngoma huweza kuongoza ngoma tu na sio nchi
3.Kuhongwa kofia na khanga ni tofauti kupata maendeleo
Ila mpaka sasa mmetia adabu vilaza wabongo nyie
 
Ukweli mweupe. Ni afadhali mtu mmoja ajitokeze atuambie ukweli. Watanzania ni wakati sasa tuache mazoea na kufikiri kwa kutumia akili tuliyopewa bure na Mungu. Huyu si rais bali janga kuliko majnga yote yaliyokwisha ikumba Tanzania.
 
Wakati mwingine ninadhani tusimlaumu Rais ,hebu tuangalie na wabunge wetu tuliowachagua wanafanya kazi tulizowatuma?Au ndio wako busy kutafuna pesa na kuona kwa kutengeneza barabara au mabomba ya maji wamemsaidia mtanzania?

Wakiamka wabunge wetu hasa wenye tiketi ya CCM basi wanauwezo wa kumwajibisha waziri mkuu na rais.
 
Wanajua kila kitu, ila ni maandalizi ya kuunda tume za ulaji, 2017 itaundwa kuhusu hili.
 
Its a matter of time!!!!

Unfortunately, hawa watawala wetu wanasema HUU NI UPEPO UTAPITA TU!! Hawafahamu kuwa there is a very high correlation kati ya wanafunzi hawa wanaume waliobalehe na vigori kufeli mitihani na kuongezeka kwa magonjwa hatari ya UKIMWI! Vijana hawa waliofeli hawatakuwa na ajira na wengi wao itabidi kwa ugumu wa maisha wafanye ukahaba na mambo mengine ya kihalifu ili kujipatia mahitaji yao ya muhimu; hivyo this will have a negative impact kwenye bajeti ya wizara ya afya na pia bajeti ya vyombo vya ulinzi na usalama. Serikali will ultimately be forced to levy more taxes from the already overtaxed population hivyo MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA kuwa ni kauli ya kuwahadaa wananchi tu.
 
..very well said.....in fact impact ya matokeo haya mabaya itakuja kujionyesha soon....in 2-3 years to come.....pale ambapo vijana wengi hawa waliofeli watakapokuwa katika pool ya wasioajiriwa.....na madhara yake yataweka mzigo mzito kwa watawala hawa.....hawa ndio vijana watakaoisumbua vilivyo serikali hii kama hawatashughulikiwa ipasavyo....maana wengi wao wataweka negative feelings dhidi ya watawala hawa....na madhara yake yakuwa makubwa kweli kweli....ndio sababu serikali wanahangaika kuunda matume sasa....wakati matatizo wanayajua...yote hii ni kuzima upepo tu..kama kawaida yao....

Kuhusu madhara ya ku neglect sekta ya afya(kama walivyofanya sekta ya elimu)....hakika nina uhakika kuwa ikifanyika survey kule afya...kuangalia mortality rates......tangu walipoanza kuwasumbua madaktari.....hali kule lazima ni mbaya sana.....ni kwasababu watanzania wamezoezwa kuwa kifo ni mapenzi ya Mungu......lakini hali halisi afya ni mbaya for sure.....wajaribu kufanya survey waone...watalia.......nchi hii imeoza......
 
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa uamuzi wa Kikwete wa kuwafukuza wale madaktari athari zake ni kubwa sana ingawa sio za wazi wazi na kupimika kama hizi za walimu kwa wanafunzi kufeli!! Watawala watafukia vichwa vyao kwenye mchanga lakini hawataepuka madhara ya vifo ambavyo vingeepukika kama busara juu ya madai ya madaktari kama yalivyokuwa ya walimu yangeshuhulikiwa badara ya kutumia fedha hizo kuongeza malupulupu ya wabunge!!
 
This is the result of playing with education many play and games have been passed like
clash program aka voda faster, joining of chemistry and physics and so so so so !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Acheni tu tuendelee kugharamia SIASA. Kupanga ni kuchagua. Tumechagua kugharamia siasa. RUZUKU kwa vyama vya siasa haikosekani kila mwezi; Fedha za kuliendesha Bunge zipo; fedha za chaguzi ndogo zipo; fedha za kuongeza majimbo, halmashauri, wilaya na mikoa zipo; hata tukitaka kuongeza serikali kuu ziwe mbili fedha zipo!

Elimu na Afya tumeacha zijiendeshe zenyewe. Tumeziweka sokoni kama nyanya. Tumeunda TCRA iangalie bei ya vocha; tumeunda SUMATRA iangalie nauli; tumeunda EWURA iangalie mafuta na maji, bidhaa muhimu na nyeti kwa wakubwa;

Haya mambo hayafanyika kwa bahati mbaya au kwa upeo mdogo wa VIONGOZI wetu. Yanafanyika kwa makusudi kabisa
 
Back
Top Bottom