Bomu la Arusha: Lichunguzwe na tume huru!

Bomu la Arusha: Lichunguzwe na tume huru!

gayo

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
238
Reaction score
93
Mimi nadhani wakati umefika kwa watawala wetu kuacha siasa kushughulikia matatizo yanoyochochea uvunjifu wa amani. Ktk suala la Arusha jeshi la polisi pamoja na chama tawala ni moja ya watuhumiwa namba 1 according to Mheshimiwa Mbowe hivyo hawana hadhi tena ya kujichunguza. Nafikiri kama kweli mheshimiwa IGP na JK mna nia njema na hii nchi undeni tume huru kuchunguza hili swala na uzuri inaonekana Mhe Mbowe ana ushahidi tosha.

Kila mtu ameshachoka na movie za jinsi haya matukio muhimu yanavyoshughulikiwa na ikumbukwe kuwa wananchi wa sasa ni wachambuzi wazuri na wanaelewa vyema jinsi haya masuala yanavyoshughulikiwa kisiasa.

Kwanini hawa viongozi walikataa pendekezo la CDM kuunda tume huru kuchunguza vifo vyote vilivyotokea kwenye shughuli za kisiasa halafu hao hao chama tawala kupitia kwa Mwigu wanailaumu CDM kwa mauaji??
Hii inaonyesha CDM wanajiamini 100% na inatuaminisha hawahusiki hata kidogo

Mheshimiwa Mwigu tafadhali kama utapita huku jibu suali langu hapo juu

Asante


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kila wakati tume za ulaji! Mianya ya ulaji kwa mwavuli wa mauaji ya kupanga! Upumbavu wa namna hii uko Tanzania tu!
 
Nakuunga mköno, lakini kitendo cha bunge kuendelea na vikao dodoma ilhali sehemu moja ya jamhuri yetu haina usalama wa kutosha ni kudhohofisha umoja,mshikamano na amani kwa taifa letu! Hizi ni dalili za kuweka matabaka ya kimaamuzi kwa jambo moja na maamuzi tofauti kwa taifa! Naunga mkono kwa swala la tume huru ya kuchunguza jambo hilo!
 
Back
Top Bottom