Bomani: Gamba litapasua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomani: Gamba litapasua CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 21, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 20 November 2011 21:01[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [​IMG]


  Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, Jaji Mark Bomani

  Mwandishi wetu

  WAKATI mfululizo wa vikao vya CCM vya Kamati ya Maadili, Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), vinaanza leo Mjini Dodoma, Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, Jaji Mark Bomani amekitaka chama hicho kuachana na mpango wa kujivua gamba akisema utakipasua.

  Moja ya agenda kubwa na ambayo imekuwa ikiwasumbua makada, wafuasi na hata wapinzani wa chama hicho ni hiyo ya kujivua gamba yenye lengo la kukisafisha kwa kuwaweka kando wanachama na viongozi wake wanaosadikiwa kukumbatia vitendo vya ufisadi na kukipaka matope mbele ya jamii.

  Jaji Bomani akionekana kuguswa na utekelezaji wa mpango huo, ametoa waraka alioupa kichwa cha habari: "Majibu juu ya Hali ya Nchi." Katika suala la kujivua gamba alisema: "Chama Cha Mapinduzi kimejiingiza kwenye mtego mkubwa wa kujivua gamba. Kwa maoni yangu, CCM ingeachana na dhana ya kujivua gamba ambayo hatima yake ni mpasuko na mfarakano mkubwa usio wa lazima ndani ya chama hicho."

  Jaji Bomani alishauri kwamba kwa kuwa CCM kitafanya uchaguzi wa ngazi zake zote mwakani, ingekuwa nafasi nzuri kwake kujisafisha.Tayari kikao cha Nec cha Agosti, mwaka huu kilikwishaamua kwamba watuhumiwa wote wa ufisadi wakiwemo wa Richmond, kashfa ya rada na Kagoda wawajibike wenyewe au wasubiri kufukuzwa katika nyadhifa zao katika kipindi cha siku 90 ambazo zimekwishapita.

  Hadi sasa CCM inaonekana kuchelewa kuwachukulia hatua watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakitajwa kukipotezea chama hicho mvuto kutokana na wananchi kuchukia ufisadi na mafisadi, hali ambayo inadaiwa kuwa ilichangia kukipa matokeo mabaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

  Lakini, kada huyo ambaye aliwahi kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 1995, alisisitiza kwamba kwa sasa hivi kingeweza kuteua kamati, jopo teule au kikosi kazi (task force), kupitia upya mwenendo wote wa kupata uongozi.

  "Utaratibu huo ungekipa chama sura au gamba jipya kwa kutumia maadili mazuri ya kukipatia viongozi bora bila ya vurugu zozote."

  Jaji Bomani alisema jopo la namna hiyo linaweza kufanya kazi hiyo na kuikamilisha ndani ya miezi michache, kabla ya uchaguzi wa mwakani.Mpango wa chama kujivua gamba ulitangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwake ambayo aliyatumia pamoja na mambo mengine, kueleza umuhimu wa chama kujihuisha kwa kujivua gamba ili kuwaacha njiani watu wote wachafu wenye tuhuma za ufisadi.

  Watu hao ni wale ambao hawaendani wala kushabihiana na historia ya chama hicho ambacho kilirithi miiko na maadili ya viongozi kutoka TANU ambayo, uadilifu ilikuwa ni kigezo kikuu kwa mwanachama.

  Serikali iachane na ATCL
  Jaji Bomani akigusia uchumi, aliitaka Serikali kuachane na suala la kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) akitaka iachie watu na makampuni binafsi kutoa huduma hiyo ya usafiri wa ndege akisema: "Serikali sasa hivi haina uwezo wa kutoa huduma hiyo."

  "Huwezi kutoa huduma ya usafiri wa ndege kwa ndege moja au mbili! Wenzetu Emirates hivi majuzi wameagiza ndege mpya 50 kwa mpigo! Wacha hao wenye uwezo wa usafiri wa ndege wahudumiwe na kampuni au mashirika ya binafsi."

  Bomani alisema kitu ambacho kinatakiwa kupewa kipaumbele nchini ni huduma ya reli na barabara... "Huu ndiyo wa wananchi walio wengi na wenye nafuu. Juhudi za Serikali zielekezwe kwenye kufufua na kuendeleza usafiri wa reli ili mizigo isafirishwe kwa gharama nafuu ya reli, barabara na maji."
  Ataka nishati mbadala

  Akizungumzia huduma ya nishati alisema ahadi zilizotolewa na Wizara ya Nishati na Madini mara kawa mara hazionekani kutekelezwa kwa kiwango kinachoridhisha hivyo kupunguza imani ya wananchi.

  "Nishati ambayo haijapewa msukumo wa kutosha ni nishati ya jua (solar power) na nishati upepo (wind power). Hizi ndizo nishati ambazo zinaweza kupatikana mahali kwingi nchini na kuwakomboa wananchi vijijini," aliongeza.

  "Mfano hai ni maendeleo ya nishati ya jua India. Nishati za jua na upepo licha ya kuwa za nafuu ni nishati ambazo haziathiri mazingira. Mbona hazichangamkiwi?"

  Kuhusu madini, alisema sekta hiyo nayo haijashughulikiwa vya kutosha akitoa mfano wa Waziri wa Nishati na Madini (William Ngeleja), ambaye aliliahidi Bunge kwenye mkutano wa bajeti kwamba ifikapo mwanzoni mwa Septemba, mwaka huu kampuni za madini hasa dhahabu zingekuwa zinatozwa mrabaha wa asilimia nne ya jumla ya mapato yake (gross revenue) lakini hadi sasa haijafanyika.

  "Kitu hiki kingeleta manufaa makubwa. Lakini, leo hii ni Novemba! Hili nalo limefikia wapi?," alihoji.

  Aliipongeza Kampuni ya Barrick African Gold kwa uamuzi wake wa kuuza baadhi ya hisa kwa Watanzania kupitia Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kuanzia mwezi ujao.

  Uamuzi huo wa Barrick ulikuwa moja ya pendekezo muhimu la Kamati ya Bomani iliyoundwa na Rais Kikwete, ambayo pamoja na mambo mengine ilipewa kazi ya kudurusu mikataba ya madini na kuishauri Serikali kuona namna ambavyo nchi ingenufaika.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mzee ameongea vizuri lakini tunatakiwa kuyapima kwa uzito unaostahili aliyoyasema,tusiingie kichwa kichwa maana siku hizi kwenye hii nchi hakuna anayeaminika moja kwa moja;watanzania tunatumika kirahisi sana siku hizi kufanikisha ajenda mbalimbali za makundi fulani fulani!namuheshimu sana mzee bomani lakini aliyoyasema nayapima kwanza!ila amenifurahisha kwenye mabadiliko ya jinsi ya kuwapata viongozi,hiyo ccm wanaweza kuifanyia kazi kabla ya uchaguzi wao kama mwenyekiti ataacha uoga!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red: Magamba hayataondoka kwani yatatumia hela walizokuwa nazo kurudi katika uongozi wa chama na JK hawezi kuwa na ubavu wa kuzuia hilokutokea kwa kuwa ni dhaifu kupindukia.
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzee Bomani ni beneficiary wa ufisadi na hawa anaowatetea ndio ambao wamekuwa wakimtumia katika kupiga madili mbalimbali. Ni vigumu sana kwa yeye kutoa maoni tofauti na haya kwa sababu yeye amekuwa kielelezo cha wazi cah ufisadi, kuanzia kwenye EPA iliyozaa Serengeti Breweries na mengine mengi. Mzee huyu amepoteza moral authority ya kutoa maoni yoyote kuhusu mustakabali wa nchi hii kwa sababu ya kutumbukia kwake kwenye dimbwi la uporaji wa rasilimali na mapato ya nchi hii.
   
 5. M

  Mzee Kipara Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15
  Hivi ni kiongozi wa namna gani anaetetea kwamba watu wanaohujumu taifa wasichukuliwe hatua? Kweli pesa mwanaharamu.
   
 6. d

  dotto JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyu mzee kwa ushauri huu alio utoa hauna tija kwa watanzania maana lichama hilo ndo mzigo kwetu sisi. Ni uchaguzi gani wa cCM ambao si wa kuhongana pesa kubwa kubwa?. Manake ni kuwa kwa mtindo huo wa pesa huwezi pata kiongozi bora bali kiongozi tamaa masilahi.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hawa ndo wale akina Kingunge waliojifanya wakomunisti huku wakiibia watanzania. Angekuwa na akili angefunga mdomo maana tunajua mengi yanayomhusu.
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Chama cha Mafisadi -- wanateteana ili wao wote waendelee kula...

  Umeona katibu mkuu wa Zamani wa CCM na yeye ana gari Mpya - aliitoa wapi?
   
 9. f

  fat faza Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli ndugu yangu ebu fikiria yan huyu mzee ndio tunamuita mzee wa busara yuko tayari nchi iangamie lakini GAMBA libaki!!!! beta die than living in dis dark country
   
Loading...