Bollen Ngetti: Dk. Bashiru, Membe si size yako, kaa kimya

Naona umeweka wosifu wa mh Membe..sio tatizo..
Lakini haibadilishi lolote..kila zama zina watu wake na yeye kashakuq zilipendwa hatakama mkilia vipi ndio ukweli mchungu..

Ccm ya sasa ni kazi tuu sio maneno matupu mliokua nayo kwenye the previous regime

Mkia ushakatwa subirini uote kama kunahiyo miujiza.
 
Dr Bashiru Ally alipoteuliwa alisema kazi yake kubwa itakuwa kuleta umoja ndani ya ccm. Tatizo ni kutofautisha kati ya kusema na kutenda. Sasa badala ya kukiunganishachama na yeye ameamua kukigawa. Inawezekana kazi ya kukiunganisha ni ngumu kuliko kukigawa. Hiyo ndiyo sababu ameingia 18 za Membe. Membe alisema yeye na Rostam wamekatwa mikia bila kuelezwa maana ya kukatwa Mikia. Labda alikuwa na maana kuwa, pamoja na Rostam kujipendekeza kwa Magufuli, ukweli unabaki palepale kwamba Rostam na Membe walimpinga Magufuli tangu mwanzo hadi mwisho. Ndiyo maana ya kuwa wote kwa Magufuli ni watoto wa kambo. Pamoja na kwamba hiyo ni tafasli yangu tu,lakini ina ukweli mwingi. Dr Bashiru badala ya kutafakali maana ya maneno ya Membe, ameamua kumshambulia Membe kwa kugawa wanachama kwa makundi na kutotumia vikao kukosoa bila kushauri namna ya kutatua tatizo. Alichokosea ni pamoja na kutohoji Rostam alitumia kikao gani kumsema Membe kuwa anataka Urais wa mwaka 2020. Pia lawama zake kwa Membe kuwa anagawa wanachama kwa madaraja, na yeye ameanzisha msamiati wa wanachama halisi na wanachama nyemelezi. Labda kuna wakati ataeleza Kati ya Membe, Rostam na yeye Bashiru Nani halisi na nani Nyemelezi? Dr Bashiru lazima ajitahidi kuwa sehemu ya majawabu ndani ya ccm badala ya kuwa chanzo cha migogoro. Mwisho dr Bashiru apunguze hasira anapojenga hola, kwa vile hasira ni sehemu ya wazimu ambayo hufanya binadamu apoteze mwelekeo.
 
Mkuu nakupa hai. Hilo jina linafanana na la babu yangu. Sifa moja tu ya Membe hukuitaja, nayo ni kuwa mtu mwongo anayesema asoyaamini.
 
Bollen tumbo likijaa huwa network za juu zinakata na kuhamia tumboni
 

Ujumbe murua kabisa, ila hofu yangu mtu akishaingia lumumba tu, anaanza kufikiri kwa masaburi, kukuelewa hapo ni kumpigia mbuzi gitaaa
 
Hmm..
Bonge moja la thread.mkuu bigup ujumbe utakua ushamfikia mlengwa.
Na binafsi naongezea nje ya mada, wale wanaopenda kupost thread na kujikuta wako perfect kumbe bogus wapitie hii thread,uandishi murua haichoshi unavutia kusoma hadi mwisho.
Hakuna vimaneno vya hovyo wala kejeli ni straight and clear article.
Kidumu CCM[emoji41]
 
Sema Tumbo na Ubinafsi ni kitu kingine ushauri safi kbs lkn cha Ajabu na ww ukipewa nafasi utafanya hayo hayo anayofanya Kaka yngu Dk Bushir embu turudi kwa Dk Rioba yule TBC vp khs Prof Mkumbo...
Akifanya na yy atakumbushwa kama alivyo mkumbusha bashiru
 
Team Membe mtararuana mwaka huu.
 
Leo ndiyo nimemwelewa membe kumbe ni mtu wamaana si agombee2
 
Kwa jinsi nijuwavyo Bashiru anapaswa kuwa katikati ya akina Membe ili kusiwepo na mpasuko!
Wote wanapaswa kuheshimiana - lkn niendelee kumpongeza membe kwa hekima na busara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…