Bodi za taalamu kama lengo lao ni kusaidia basi wapunguze gharama

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,060
10,528
Uwepo wa hizi bodi za taalamu ni muendelezo wa kukandamiza juhudi za maskini kujikomboa katika umasikini. Uhalisia ni kuwa gharama za masomo zimekuwa kubwa na bado serikali inashindwa kuweka masharti na vigezo nafuu vitakavyo muwezesha kila mhitimu kujiunga na bodi za taalamu. Recently ajira nyingi zimekuwa zikiwataka wahitimu wawe registered na bodi za taalamu walizosomea lakini sio wahitimu wote wanaweza kumudu gharama hizo na ukizingatia wametoka kutumia gharama kubwa hadi kugratuate.

ushauri.
Serikali ijaribu kuzielekeza bodi zipange gharama ambazo zitakuwa affordable kwa kila mhitimu kwa kuzingatia hali ya maisha awamu hii ya tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…