BODI YA MIKOPO-HESLB

BODI YA MIKOPO-HESLB

DOFFA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
425
Reaction score
233
upload_2016-11-20_14-31-19.png


Ni tumie fursa hii ya leo kumshukuru mungu kwa uzima anaotujalia katika maisha na shughuli zetu za kila siku.Niwape pole nyingi serikali yetu na taasisi zetu kwa kazi wanazofanya kukiwa na changamoto za hapa na pale na kwa namna wanavyo kabiliana.
Katika kukabiliana na changamoto kwenye mifumo ya serikali wataalamu wetu wapo na serikali inatakiwa kuweka kipaumbele suala la utafiti ili kupima athari za mabadiliko kama yataleta unafuu kwa maisha ya watu na afya nchi.
Mosi,Suala la mikopo;Serikali pamoja na vipaumbele ilivyo navyo inapaswa kuangalia namna bora zaidi ya kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu yao kwenye mazingira rafiki bila makwazo yeyote.
Pili,vigezo;Kazi kubwa ya vigezo na masharti ni kuchuja waombaji wapya wa mikopo kila mwaka kuendana na mipango iliyopo na vigezo huwa vinabadilika mwaka hadi mwaka,ktk hili serikali ingefanya makosa makubwa kuingiza vigezo hivyo kwa wanafunzi wetu wanaoendelea.Hapa naipongeza SERIKALI yetu kwa kuona mbele zaidi.
Tatu,wadaiwa;Nitumie fursa hii vilevile kwa wanufaika waliowezesha kusoma kwa mikopo hii na wamehitimu wajitahidi kurudisha mikopo hiyo kwa wakati ili wengine waweze kusoma kama wao walivyosoma.HII NI MUHIMU SANA SANA.
Nne,wanufaika;Wale wote wanaonufaika na mikopo wanapaswa kutumia kwa umakini mkubwa na kusoma kwa bidii ili wawe msaada kwa jamii na taifa kwa ujumla.Watazame nyuma-mbele-na pembeni kuona ni wangapi wamekosa wakashindwa kuendelea na masomo?
Naendelea kusisitiza ombi kwa HESLB na SERIKALI kuwa watulivu zaidi wakati wa kutatua changamoto mbalimbali ili kuongeza ufanisi zaidi bila kusababisha majeraha na vidonda.
NIMTAKIE AFYA NJEMA NA ULINZI WA MUNGU MH.RAIS WETU NA WATUMISHI WOTE WA SERIKALI NA WA UMMA KATIKA MAJUKUMU YAO YA KUHUDUMIA TAIFA.
MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
DOFFA
 
Back
Top Bottom