mediy dullah
Member
- Jan 9, 2014
- 35
- 12
Habari za wakati huu home of great thinker .Najua humu wapo wadau wengi tu wa elimu ya juu. Nataka niwakumbushe kitu bodi ya mikopo kuhusu chuo cha Bahari DMI.
Chuo cha DMI ni moja kati ya vyuo vikubwa katika kutoa maritime education africa mashariki na kati.Kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara vyuo kama hivi vipo vinne tu.Chuo kinatoa kozi kubwa mbili marine engeneering na maritime transport.
Graduate wa chuo cha DMI na ujuzi wanaoupata wanaweza kufanya kazi viwandani, kwenye vituo vya kufua umeme(power plant), baharini kwenye vyombo vya majini, kwenye meli za kuchimba mafuta na gesi, kwenye migodi na sehemi nyingine nyingi zinazuhusu matumizi ya mitambo. Kwa maana hiyo kozi zinazotolewa ni moja kati ya vipaumbele vya mh Rais.
Lakini cha ajabu bodi ya mikopo mmekuwa mkisuasua kutoa mikopo kwa wanafunzi wa hiki chuo inamaana mnakaidi agizo la mh rais la kuifanya tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Mkiulizwa wenyewe mnakiri kuna tatizo kwenye database ya majina ya wanafunzi wa DMI swali ni JE! kwa tatizo hilo uzembe ni wa wanafunzi au nyie.Na kama uzembe upo kwenu kwa nini wanafunzi ndo wawe wahanga wa uzembe wenu. Kiukweli nyie ndio mnaochangia kurudisha nyuma juhudi za mh raisi hasa ukizingatia nchi ya viwanda inategemea sana uchumi wa bahari. Vijana wamejitolea kwa sababu kazi za ubaharia ni za wito na kuhatarisha maisha lakini bado mnawakatisha tamaa.Chuo kimefunguliwa tar 31 october mpaka leo mmetoa mkopo kwa wanafunzi wawili.
Mtoto wa maskini ambae amesoma shule ya kata ada elfu 20 kwa mwaka kwa miaka minne ni 80000 Tsh akasoma a level miaka miwili ada sh 140000 Tsh halafu unategemea ataweza kulipa 1.6 milioni per one year bado na yeye hajala hajapanda gari ukizingatia chuo hakina hostels.Acheni ubabaishaji na kumpamba mh rais kwamba mmefanya kazi aliyowaagiza kwa ufanisi.Mnataka kuua taaluma ya ubaharia wakati mpaka sasa dunia ina upungufu wa 82% ya wataalamu wa fani za ubaharia.Halafu serikali inawalipa takriban walimu 55 wakiwemo doctors ,engeneers na ma captain pesa nyingi tu kwa ajili ya kuwafundisha vijana katika fani hii ya ubaharia.
Halafu kila tarehe 25 june mnaungana nao kusherehekea siku ya mabaharia duniani kwa yapi mliowafanyia.Angalieni upya mjue tatizo lipo wapi mtoe hizo allocation kwa vijana waliojitolea kwa fani hii adimu kabisa yenye changamoto nyingi idadi yenyewe ni ndogo tu watu 70Ujumbe umefika labda mjidai hamjaelewa.