Scorpion_004
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 204
- 125
"umasikini umegawanyika sehemu mbili,yaani umasikini wa mawazo na pesa.Ndani ya umasikini wa elimu kuna umasikini wa mawazo.
Hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa mawazo kwa maana kwamba, hakuna kitu kibaya kama kuikabidhi akili yako kwa mtu mwingine(mhisani wa kimasomo binafsi)huku ukisumbuliwa na njaa.
Inasikitisha sana kuona bodi ya mikopo ya elimu ya juu kutoa mikopo kwa kubagua yaani mtoto wa masikini ambaye familia yake inaishi kwa kutegemea TASAF ananyimwa mkopo.Mnapo sema mnatoa mikopo kwa walemavu, wenye mzazi mmoja na waliosoma sayansi ni sahihi lakini angalieni na kundi lingine ambalo kiukweli familia anayotoka kiuchumi hali ni mbaya.
Embu jiulize, ada ya mafunzo, chakula na malazi, vitabu na viandikwa, mafunzo ya vitendo pia gharama za mahitaji maalumu ya vitio na gharama za tafiti atapata wapi huyu mtoto wa masikini mwenye ndoto ya kupata elimu lakini anaishia mtaani kwa msongo wa mawazo ambao mnamsababishia mwisho wa siku vijana wengi wanajikuta wakiangukia katika janga la matumizi ya madawa ya kulevya, kuuza miili yao na kupatwa utapiamlo kwa kupata chakula mara moja kutwa.
Ndugu mkurugenzi wa bodi ya mikopo elimu ya juu jaribu kungalia rufaa za wanafunzi kwa jicho la tatu. Tunapata taabu sana mwisho wa siku ufaulu unapungua (njaa+masomo)GPA itakuwa sio nzuri.
Bila shaka serikali ya awamu ya tano naomba mtimizie moja ya ahadi Yenu kuhusu mikopo hali ni ngumu. Kwa wale wana JF ambao wamepita vyuo vikuu mnaelewa maisha yalivyo bila mkopo huku unatoka familia ya chini kiuchumi.
Ama kweli NGO'MBE WA MASIKINI HAZAI