Bodi ya Ligi na TFF ndani ya bifu zito

Bodi ya Ligi na TFF ndani ya bifu zito

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,393
Taarifa za uhakika ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kuna hali ya kutoelewana kati ya TFF na bodi ya ligi. Chanzo cha kutokuwepo kwa
maelewano mazuri baina ya uongozi wa bodi na TFF ni kutokana na viongozi wa bodi ya ligi kukataa kukaguliwa mahesabu ya matumizi yao ya fedha.

Inasemekana kwamba uongozi wa Jamal Malinzi ulivyoingia madarakani uliwasaliana na bodi ya ligi ukiwaeleza kwamba ungewatumia mkaguzi wa
mahesabu bodi ya ligi kwa ajili ya kukagua matumizi yao.

Lakini katika hali ya kushangaza bila sababu ya msingi na yenye mashiko uongozi wa bodi ya ligi ulikataa kumpokea mkaguzi wa mahesabu, hali iliyopelekea kutokuelewana baina ya TFF na bodi hiyo.

Source: Shaffih Dauda
 
Back
Top Bottom