singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SERIKALI imetangaza uwezekano wa kufuta bodi zote za mazao ya biashara zitakazoshindwa kuainisha uhalali wa uwepo wake na kuanzisha bodi moja itakayosimamiwa na watendaji pekee, baada ya kubainika kuwa bodi hizo nyingi zimejaa wizi na ufisadi.
Aidha, imetangaza kuondoa rasmi ushuru wa magetini kutokana na kutoa mianya ya rushwa pasipo na tija, huku ikitangaza kupitia makato yote wanayotozwa wakulima pamoja na wavuvi ili kuondoa yale yanayotumika kama kichaka cha kunufaisha wachache.
Pia imeitaka mikoa yote nchini, kuwasilisha waraka utakaobainisha vyanzo vya migogoro ya ardhi katika mikoa husika ili itafutiwe ufumbuzi wa haraka.
Akihitimisha hoja ya mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya mwaka wa fedha wa 2016/17, Waziri Mwigulu Nchemba alisema kuna utitiri wa bodi na vyama vya ushirika vya mazao, visivyo na tija zaidi ya kusababisha malalamiko.
Alizitaka kujitathmini na kujitambua zenyewe uhalali wa uwepo wake.
“Nilikuwa na nafanya tathmini ya bodi hizi ndio maana sijatoa mapendekezo ya majina mpaka sasa kwa sababu kumekuwa na malalamiko mengi dhidi ya bodi hizi... “...Hivi mbona kuna mazao ambayo hayana bodi lakini huwezi kusikia suala la wizi, makato, ufisadi na madeni, tena yanafanya vizuri tu, tofauti na mazao yenye bodi,” alisema Mwigulu.
Alisema mazao hayo yasiyo na bodi wakulima wake wanazalisha kila siku na huwezi kusikia malalamiko ya kesi za wizi, makato, madeni ya mikopo wala unyonyaji na kutolea mfano wa zao la mpunga ambalo kwa sasa Tanzania ni ya pili kwa uzalishaji lakini halina bodi.
Alitoa fursa ya mwisho kwa bodi na vyama hivyo vya ushirika kuwasilisha kwake sababu na uhalali wa kuendelea kuwepo, vinginevyo atafuta taasisi zote zinazotumika kama vichaka vya kujinufaisha na majasho ya wakulima.
Alisema ni bora kuwa na bodi ya mchanganyiko na bodi ya mazao ya biashara na wasimamizi watakuwa watendaji.
“Hatuwezi kuwa na taasisi zinazotumika kuwanyonya wengine,” alieleza. Kuhusu kufuta ushuru magetini, alisema nia ya serikali ni njema na imelenga kuwaondolea usumbufu wakulima na wafanyabiashara. “Nasikia wengine wanadai eti halmashauri zitakosa mapato, nawaambia kwa nia njema katika mazingira tuliyonayo kupitia haya mageti tunatoza ushuru wa zao au bidhaa moja zaidi ya mara mbili hii si sahihi,” alisema.
Alisema kupitia mageti hayo, wafanyabiashara na wakulima wamekuwa wakisumbuliwa na kutozwa fedha ambazo nyingine zinapotelea kwenye rushwa na wala hazina mchango wowote kwa halmashauri.
“Tumesikia wengine wanapata hadi ajali kwa sababu ya kuwakimbia hawa watoza ushuru wa mageti. Ni lazima tuweke utaratibu unaotambulika na kuondoa mianya hii ya rushwa, lakini pia kumpunguzia usumbufu huyu mkulima au mfanyabiashara,” alisisitiza.
Alisema serikali imeamua kuwa kuanzia sasa fedha zitakazotozwa kama ushuru wa mazao, itozwe eneo moja la sokoni na risiti itakayotolewa ndio itakayotumika katika maeneo yote bidhaa hiyo itakapoenda.
Aidha, alisema hata bidhaa za minadani ushuru unaotozwa kwenye leseni ya mfanyabiashara na mkulima risiti yake ndio itumike katika minada yote na si mtu huyo mmoja kutozwa tena kila anapoenda mnadani.
Akizungumzia makato, alisema tayari serikali imepitia makato yote yakiwemo ya leseni na mazao na tayari wamefanya uamuzi na kinachosubiriwa ni mawasiliano ya serikali na huenda yakatolewa uamuzi kwenye Bajeti ya Serikali.
Alikiri kubaini kuwepo kwa utitiri wa makato yasiyo na tija hata kwa serikali zaidi ya kuwa mzigo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi huku akitolea mfano eneo la uvuvi ambalo linatozwa hadi makato ya ushuru wa zimamoto ambayo kiuhalisia hayamsaidii mvuvi.
Kuhusu tatizo la migogoro ya ardhi, alisema wizara yake imetoa kipaumbele katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo kwa kuwa lisipochukuliwa hatua linaweza kutishia amani ya nchi.
Alisema kwa kuwa suala hilo ni mtambuka, tayari wamewasiliana na wizara zote husika ambazo zote zitakaa kwa pamoja na kujadili kwa kina namna ya kumaliza tatizo hilo ambalo linazidi kukua katika baadhi ya maeneo.
Hata hivyo, alisema Wizara ya Kilimo imeshandaa mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo namna ya kutafuta ardhi itakayotosheleza wafugaji, kulinda ardhi ya wafugaji kwa kuitangaza kwenye Gazeti la Serikali na kutenga ardhi kwenye mikoa kwa ajili ya kilimo na ufugaji.
Aidha, alisema kwa upande wa wafugaji wenye mifugo mingine, wizara hiyo inafikiria kuwafanya wawekezaji wakubwa kwenye mifugo kwa kuwapatia maeneo yanayokodishwa kwa ajili ya ufugaji na baadaye kuwaunganisha na wenye viwanda kwa faida ya wote.
Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, alisema kwa kuwa suala la migogoro ya ardhi ni mtambuka, anaamini kupitia vikao vitakavyojumuisha wizara zote husika, watapatia ufumbuzi tatizo hilo baada ya kubaini chanzo cha mgogoro kwa kila mkoa.
Alisema wanatambua kuwa kuna vyanzo vingi vya migogoro hivyo wameagiza kila mkoa kuwasilisha waraka unaoinisha vyanzo vya migogoro hiyo katika mkoa husika ili kuweza kutafutia ufumbuzi wa haraka.
Wakati huo huo, Mwanasheria Mkuu George Masaju ametangaza rasmi kuwa hati ya mgawanyo wa madaraka ya mawaziri tayari imeshatolewa na Rais John Magufuli kupitia Tangazo la Serikali Namba 144, lililochapishwa Aprili 22, mwaka huu.
Alisema suala hilo limekuwa likipotoshwa kuwa hati hiyo ni mwongozo wa mawaziri wakati kiukweli hati hiyo inatamka majukumu ya wizara pekee na wala haihusiani na utendaji wa waziri.