Bobi Wine apewa kifungo cha nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279

JESHI la Polisi limemweka katika kizuizi cha nyumbani mwanamuziki na Mbunge wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine.

Jeshi lilichukua hatua hiyo saa kadhaa baada ya kutangaza mpango wake wa kuandamana hadi polisi kupinga ukatili dhidi ya matamasha yake ya muziki na wanasiasa wa upinzani.





Aliwataka Waganda wote wenye hasira kuungana naye katika mapambano dhidi ya ukosefu wa haki.

Polisi walisema lengo la uamuzi wao ni kumzuia mwanasiasa huyo wa upinzani kufanya mikutano iliyo kinyume cha sheria.

“Hizo zilikuwa ni hatua zilizochukuliwa chini ya sera ya kuzuia ili kulinda sheria na utulivu wa umma wakati bado anatishia kufanya mikutano kinyume cha sheria.

“Maofisa wetu wa ujasusi watatusaidia kumpata na tutaweza kuona ni nini kitakachofuatia. Hili limekuwa suala la usalama wa taifa,” alisema Msemaji wa Polisi, Fred Enanga.

Awali Bobi Wine alikuwa ametangaza mpango wa kufanya maandamano ya umma kote nchini kupinga hatua ya polisi kuendelea kuzuia matamasha yake ya muziki na ukatili dhidi ya wanasiasa wa upinzani.

Alitangaza hatua yake alipokuwa nyumbani kwake Magere, Kasangati katika Wilaya ya Wakiso muda mfupi baada ya polisi kumzuia asubuhi kufika katika makazi yake ya ufukweni ya One Love Beach yaliyopo eneo la Busabala na kumwingiza katika gari la polisi na kumbwaga nyumbani kwake hapo.
 
Viva mapambano kumbe ndo yameanza ya kudai uhuru? Siyo kwa mabeberu ila kwa wapigania uhuru na haki waliojinasifu kupigania haki ya waganada. Leo ni walinzi wa haki za chama chao na wana Kabale na Mpololo? Bashambo oyeee. Njoo utuchukue na sisi Museveni ingawa wewe siyo ukoo wetu ila unajikomba.
 
Back
Top Bottom