Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,473
- 757
kwani ni kosa gani alilofanya Boban hadi mseme kuwa amekosa nidhamu? Au kwakuwa Maximo amesema hivyo? Tatizo la ukosefu wa nidhamu ni endelevu, kama ni hivyo mbona Phil kila kukicha amekuwa akim miss Boban katika kikosi chake toka alipoenda kufanya majaribio Sweden?Ni kweli, matarajio yetu kwake ni kuwa asituangushe kwa mambo ya kukosa nidhamu. Hata kama ni mchezaji mzuri kiasi gani, kama hana nidhamu hataweza kufika popote maana dunia hii inatabia ya kuwakimbia watu wenye kukosa adabu kwenye shughuli wanazofanya.
huko ataacha tu maana hakuna cha arusha wala monduli wala temeke wala wapi,na akijitia jeuri kukitafuta mitaani siku si nyingi mtamuona bongo na story kibaao za kulaumu watu,huko mambo hayo aache hata kufikiria polisi huko wanafatilia mambo hayo kinoma hasa kwake yeye yatamuharibia tu,usikute washampima na wameona kama anakula jani asa akiendelea watajua tu na hiyo ndio itakua imeharibu future yake vibaya,achana na ndumu bwa mdogoSura yenyewe tu inaoneka anakula CHA ARUSHA/TARIME huyu
wewe umenena,ndumu kweli sio nzuri.BOBAN uwe na nidhamu ndio siri ya mafanikio ndumu haitakufikisha popote
vp tena?uchawisimba yamsajili haruna moshi caf
kiungo haruna moshi aliyefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya gefle if ya nchini sweden ni miongoni mwa wachezaji 27 waliosajiliwa na simba ya dar es salaam kwa ajili ya michuano ya kimataifa mwakani.
Haruna, ilielezwa hivi karibuni kuwa amefuzu majaribio kwenye klabu hiyo na anatarajiwa kwenda tena sweden mapema mwezi ujao kujiunga na timu hiyo, lakini klabu ya simba imeorodhesha jina lake kwenye orodha yake iliyowasilishwa shirikisho la soka tanzania (tff) jana kwa ajili ya kutumwa makao makuu ya shirikisho la soka afrika (caf).
Akizungumza jana, msemaji wa klabu ya simba, clifford ndimbo, alisema ni wachezaji watatu hawapo kwenye orodha ya simba kwa ajili ya michuano ya kombe la shirikisho ambao ni adam kingwande, george nyanda na meshack abel wanaocheza kwa mkopo klabu ya africa lyon.
Katika kikosi hicho lipo jina la mshambuliaji mkenya aliyesajiliwa akitokea yanga, mike barasa pamoja na nyota mwingine mkenya jerry santo ambao wote wamesajiliwa kwenye dirisha dogo novemba mwaka huu.
Orodha kamili ya wachezaji wa simba kwa michuano hiyo ni juma kaseja, ally mustapha, deogratius munishi, haruna shamte, haruna moshi, salum kanoni, kelvin yondan, salim aziz, danny mrwanda, nico nyagawa, antony matangalu, mussa mgosi, hilary echesa na ulimboka mwakingwe.
Wengine ni uhuru seleman, mohamed banka, ramadhan chombo, joseph owino, jabir aziz, juma jabu, juma nyoso, emmanuel okwi, mohamed kijuso, david naftal na amri kiemba.
Kuhusiana na hofu ya simba kuchelewesha kutuma majina hayo tff huku siku ya mwisho ya majina kutumwa caf ikiwa ni leo, ndimbo alisema, hawana hofu na hilo na jana walitarajiwa kuyawasilisha tff.
Mwisho wa caf kupokea majina ya wachezaji kwa ajili ya michuano ya kimataifa bila faini ni leo, ambapo baada ya hapo klabu italazimika kutuma majina hayo pamoja na faini hali ambayo juzi ilimfanya katibu mkuu wa tff, fredrick mwakalebela kuihimiza simba kufanya hivyo.
Akizungumza jana, mwakalebela alisema ana matumaini kwamba simba ingewapa mapema usajili wao, hivyo wao watautuma caf kama taratibu zinavyotaka bila kuiathiri klabu hiyo.
Source: Gazeti la habari leo
vp tena?uchawi
ndio nashangaa mambo ya bongo yanaumiza kichwaUchawi kivipi mjomba?,hizi taarifa za Boba hazieleweki hata kidogo,mara kapata timu Ulaya,mara kasajiliwa na Simba!!,ina maana atachezea timu mbili kwa wakati mmoja???.Haya soma habari nyingine hii hapa chini
SIMBA ya Dar es Salaam imewasilisha majina ya wachezaji 27 watakaoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani akiwemo kiungo wake mahiri Haruna Moshi Shaaban "Boban".
Majina hayo yamewasilishwa jana kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), siku moja baada ya shirikisho hilo kudai juzi kuwa klabu hiyo imeshindwa kufanya hivyo.
Afisa habari wa klabu hiyo, Cilfford Ndimbo alisema jana kuwa wamewasilisha majina hayo 27 TFF , isipokuwa watatu ambao wameuzwa kwa mkopo kwenye ya klabu ya African Lyon.
"Tumewasilisha majina ya wachezaji wote, ispokuwa Meshack Abel, George Nyanda na Adam Kingwande, hao wapo Lyon kwa mkopo.
"Ni mataumanini yetu kuwa majina hayo tumeyawasilisha kwa muda muafaka kwa sababu kesho (leo) ndiyo mwisho ya kufanya hivyo.
"Kwa kuzingatia muda huo ni matumaini yetu kuwa TFF itayawasilisha CAFjijini Cairo, Misri bila ya matatizo," alisema Ndimbo.
"Kutokana na usajili imara tulioufanya msimu huu, hatuihofii timu yoyote ambayo tutakutana nayo," alisema.
Kikosi hicho cha wachezaji 27 ambao walikuwa wameweka kambi visiwani Zanzibari kwa ajili ya michuano ya Tusker kiliwasili jijini Dar es Salaam jana kwa michuano hiyo.
Hata hivyo taarifa za kupelekwa kwa jina la Boban katika CUF kwa ajili ya michuano ya kimataifa kumeibua maswali mengi kutoka kwa mashabiki kuwa je ni vp kiungo huyo asajiliwe na simba katika michuano ya kimataifa hali ikiwa ameripotiwa kushinda majaribio katika timu ya daraja la kwanza nchini Sweden?
Itawezekanaje mchezaji mmoja akachezea timu mbili kwa msimu mmoja?ikizingatiwa kule Sweden atakwenda kusaini mkataba wa takriban msimu mmoja kuanzia mapema mwakani wakati ambapo pia simba itakuwa mashindanoni wanahoji wachambuzi wa masuala ya kispoti kupitia Bongo Ndiyo home!
Wadadafuaji hao wa kispoti wamewataka viongozi wa simba,wakara wa mchezaji huyo na Haruna Moshi Mwenyewe kuwaeleza watanzania ukweli ni upi?alishindwa majaribio au alishinda? na kama alishinda iweje akimbilie kisamvu nyumbani kwao akaacha nyama ya kutosha kwa jirani asiye na mizengwe katika masuala ya misosi? au ale tu kisamvu kwa kuwa kimepikwa home?
Wamesema wanalazimika kuhoji hivyo kwa kuwa hakuna uwiano wa ubora wa soka kati ya Tanzania km sio simba na sweden katika kikosi cha daraja la kwanza ambacho boban anatakiwa.
Naomba kuwasilisha Je Haruna Moshi aliyekwishaichezea stars michezo 24 alishindwa majaribio Sweden?
Source Dullonet