VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Kuna taarifa kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA,baada ya Mzee Edwin Mtei,Mohamed Makani(Bob Makani) amelazwa katika Hospitali ya Aghakan.Mwenye taarifa juu ya kinachomsibu Kamanda huyu atujuze.Nitakwenda pale kesho kumtakia pole Mzee wetu huyu.Get well soon Kamanda!
Ni hivi Mkuu: mimi najua kuwa Kamanda amelazwa Aghakan ila bado sijui anasumbuliwa na tatizo gani.Lazima niwe mkweli.Kuhusu Mohamed na Bob ni kuwa Kamanda alibadili jina kisheria na kuitwa Bob kutoka Mohamed.Ni hayo tu Mkuu.Sasa mbona hueleweki kama Ngiri?? Mana meno yamekutoka, ukicheka hatujui ukilia hatujui...inaonekana una info halafu unataka sisi tutoe taarifa..*sigh* kwanza nieleze KUNA uhusiano gani kati ya Mohammed makani na Bob maana sikuwahi kujua kama anaitwa Mudy..
Umesema kuna taarifa..ukaomba mwenye, taarifa halafu uka conclude as if una uhakika na chanzo chako cha habari...
Mzee Bob Nyanga Makani ni mpambanaji kweli huyu. Nakumbuka siku moja ambapo nilishiriki maandamano naye wakati ndio kwanza vyama vingi vimeanzishwa hapa nchini, mzee alikuwa na munkari na alikuwa mhamasishaji mzuri. Mungu amjaalie apate nafuu mapema.Ni hivi Mkuu: mimi najua kuwa Kamanda amelazwa Aghakan ila bado sijui anasumbuliwa na tatizo gani.Lazima niwe mkweli.Kuhusu Mohamed na Bob ni kuwa Kamanda alibadili jina kisheria na kuitwa Bob kutoka Mohamed.Ni hayo tu Mkuu.
Umri umekwenda Mzee Makani, nakumbuka mwaka 1992 ulinipatia kadi ya CHADEMA mjini shinyanga. Ugua pole Mungu akuponye haraka