BMT yaitaka Yanga kufanya Uchaguzi ndani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Baraza la Michezo Tanzania limeitaka timu ya Yanga kufanya uchaguzi

Kaimu katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema, walishatoa maelekezo kwamba ndani ya siku saba wafanye utaratibu au wafanye uchaguzi kwani yote yanawezekana licha ya katiba yao kueleza kuwa uchaguzi ni ndani ya siku 60.

Kiganja amesema, Klabu hiyo inatakiwa kuanza kuchukua hatua kwa kila walichoambiwa kama ni kuanza mchakato wa uchaguzi lakini wawe wametimiza kwa muda walioambiwa.

Tayari barua ya kutakiwa kufanya uchaguzi imeshawafikia viongozi wa Yanga na wamekiri kuanza mchakato wa kuitisha uchaguzi hivi karibuni, Yanga inatakiwa kufanya uchaguzi kabla hawajarudiana na Al Ahly huko Cairo Misri.

Yanga sasa ipo chini ya uongozi ulioingia madarakani Julai 15 mwaka 2012 ambao uliingia mara baada ya kufanyika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za viongozi waliojiuzulu ambapo uongozi huo pia umemaliza muda wake.
 
...wafanye uchaguzi ndani ya siku saba?,mbona balaa hilo,hata hivyo nahisi watawarudisha viongozi walewale!
 
Hivi ni kitu gani kinakwamisha uchaguzi wa Yanga? Mbona nao unakuwa jipu? Diwani wa Mbagala itisha uchaguzi mapema!!
 
Back
Top Bottom