BlackBerry 101: How to Reload the Operating System on a Nuked BlackBerry. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BlackBerry 101: How to Reload the Operating System on a Nuked BlackBerry.

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Gbollin, Apr 1, 2011.

 1. Gbollin

  Gbollin JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 589
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wakuu, Nilikuwa Na-update Blackberry yangu curve 8320, ambayo imetolewa na vodafone, Wakati Na-update nilipata tatizo la simu ku-stack na kushindwa kuendelea na update, Nilijaribu kuichomoa betri na kuirudisha tena lakini ikagoma kabisa kusoma na ikawa haionekani kwenye computer. Nilipoidisconect na kuiwasha haikuwaka bali ilikuwa inawaka taa ya juu nyekundu kwa muda mrefu mpaka nilipoamua kutoa betri na hadi hivi sasa siwezi kuitumia tena, Nimejaribu njia mbalimbali ili kufix tatizo ila nimeshindwa. Naomba msaada wenu nifanyeje mpaka niweze kulitatua tatizo hili.
   
 2. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Duh! Mkuu we kiboko! Ulikuwa una upgrade OS kwa njia ipi? Ya mtandao au kwa kutumia BB Desktop Manager?

  Sasa kama haiwaki ina bidi ukubali kupoteza baadhi ya vitu vyako kama vile applications n'k kama ulikuwa umefanya full backup ndio itakuwa salama yako...


  Nenda kwenye Blackberry desktop manager, then click Applicatins(fanya hivi simu yako ikiwa connected hata kama hionekani kwenye computer) aagh nimekosea (samahani mambo ya weekend yameanza kichwani) haya tuendelee na topic yetu.

  Fanya hivi kama ume install BB DM0 versio 4.5 na kuendelea , ingia my computer/drive c/programs files, tafuta folder lililo andikwa commons file, baada ya hapo utaona folder la Blackberry lifungue, na ndani yake utaona file limeandikwa "vendo" lifute na ubakishe vendol.HTML,

  Baada ya hatua hizo... Kwenye hilo hilo folder kuna ka-application kamaandikwa ''loader'' au ''apploader"kifungua na baada ya kufanya hivyo itakutaka uselect simu yako, fanya hivyo(kwenye hatua hii ni lazima simu yako ionekane kama ilipata matatizo ya software) baada ya kuselect simu yako itakuletea menu ya OS ya bb yako, na chagua vitu unavyotaka kuinstall kwa kuweka tick kwenye vi-box usika, na baada ya kufanya hivyo nende next na subiria kwa mda kidogo imalize kuistall Os kwenye simu yako. Na baada ya mda utaona simu yako ikiwaka...

  Ukifanikiwa hizo step simu yako itakuwa imerudi katika hali yake ya kawaida,japokuwa itakuwa kama vile ndio umetoka kuinunua dukani kwa data ambazo zilikuwa kwenye simu zitafutika(siyo za kwenye memory card) kama ulikuwa umefanya backup hapo nyuma sasa unaweza kuzi rudishia....

  Samahani kama maelezo yangu yana dosari yoyote, hiyo ni kutokana na "ndovu" pia mtake radhi shemejio kwa kumuweka mpweke wakati nikiandika haya...
   
 3. Gbollin

  Gbollin JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 589
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu, Nimefuata maelezo yako na nimefanikiwa. Nilikuwa naaupdate kupitia desktop bb manager.
   
 4. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pamoja sana mkuu... Nafurahi kusikia kuwa umefanikiwa kutatua tazizo lako, pia asante kwa mrejesho wako(maana hii kitu inatupa moyo wa kusaidia na wengine) maana kwenye hili jukwaa watu wanatabia ya kuomba msaada na ukiwasaidia wanakimbia kimoja hawarudi kuja kutujulisha kama walifanikiwa au laa kitu ambacho kina tukatisha tamaa wengi wetu na kubaki kutizama thread zenu tu.
   
Loading...