Biteko afanya mazungumzo na Kampuni kutoka Marekani

Biteko afanya mazungumzo na Kampuni kutoka Marekani

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
1553677204183.png


Waziri wa Madini, Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya PRNG Minerals Ltd, ya Marekani, Rocky Smith na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni hiyo Lucas Stanfield ofisini kwake Jijini Dodoma.

Watendaji hao wapo nchini kwa ziara ya kawaida ya kikazi ya siku tano ambapo waliomba kukutana na Waziri wa Madini.

Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo inakusudia kuwasilisha taarifa juu ya hali na Maendeleo ya soko la dunia kwa Madini ya Rare Earth Elements na kuzungumzia hatua iliyofikiwa kwa ombi la leseni ya uchimbaji Mkubwa wa madini hayo.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amesema wizara iko tayari kuipokea kampuni husika nchini baada ya kukamilika kwa taratibu kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu Rocky Smith, amesema kuwa, amefurahishwa na ushirikiano unaooneshwa na wizara na kuahidi kuanza shughuli za uchimbaji mara baada ya kukamilika kwa taratibu.
 
Back
Top Bottom