Bingwa wa EPL

Bingwa wa EPL

reginahope

Senior Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
163
Reaction score
30
Wadau sipo kiushabiki zaidi ila mtizamo wangu kuhusu bingwa wa EPL. Nimezichunguza timu 4 za juu katika epl na binafsi naona kombe litaenda Chelsea au Liverpool.

Manchester City nimewatoa kwasababu naamini ana game nyingi ngumu za away. Najua mechi na Liverpool,Arsenal pamoja na Manchester united hawezi kushinda.

Pia Arsenal nawatoa sababu fixture yake ya march ni ngumu sana, game kama 5 mfululizo zote ngumu.

Liverpool wapo vizuri kwa sasa na gap kati yake na Chelsea ni point 4 tu, Chelsea pia wapo vizuri na bahati kwao game ngumu ya away ni ya Liverpool tu.

So binafsi nawapa nafasi kubwa Chelsea au Liverpool kubeba ndoo.

Chelsea ana game 6 za home na 6 away, so nadhan anahitaji pointi km 30 awe bingwa.
 
Nakuunga mkono sio kwa sababu ni shabiki wa Liverpool ila kwa sababu umefanya scientific analysis. Mwishoni wa Januari nilifikiri Man City anaweza kuchukua bila tatizo lakini kiwango chao sikuza karibuni dhidi ya Norwich, Chelsea na hata walipcheza jana na Chelsea nimeanza kuwa na shaka na uwezo wao baada ya kukosekana kwa wachezaji muhimu kama Sergio Aguero na Fernandinho
Kuhusu timu yangu ya Liverpool nilifikiri tunwania nafasi ya 4 lakini kwa kiwango cha mwaka 2014 na kutetereka kwa timu nyingine nashawishika kuamini kwamba Liverpool ikirekebisha matatizo kidogo ya defence (Sakho,Enrique na Agger wanarudi) ubingwa ni nje nje.Kumbuka Liver ndio timu yenye safu kali zaidi ya ushambuliaji baada ya Man City (goli 66).
 
Mimi ni shabiki wa Chelsea na nipo hapo si kiushabiki bali nina maoni yaliyo si ya kialshabiki....

1.Arsenal ana nafasi ngumu ya kubeba taji ifikapo mwezi Mei..Hii ni kutokana na ratiba ngumu iliyo mbele yake!..Pia kukosekana kwa Ramsey ambaye alikuwa mfunguji na mchezeshaj mzuri ni pengo kubwa sana..Pia mchezaji kama Walcott ambaye pia ni majeruhi kuna waathiri sana na kutokuwa na kikosi kigumu ambacho kitaweza kupambana hadi mwisho..

2.Man City sio wabaya sana na pia wanaweza kulitwaa taji hili pale tu watakapoweza kupata points muhimu za game zao za ugenini..Pia kukosekana kwa Aguero na Fernandinho ni pengo kubwa kwao sasa...

3.Liverpool wameuanza mwaka vizuri na wameweza kuchukua alama muhimu katika mechi zao mpaka sasa..Hivyo wakiendelea na kasi hii basi si ajabu kama wakitwaa taji...

4.Chelsea ambao ni kinara pale EPL pia wana nafasi ya kuwa bingwa msimu huu..Ila tu ni pale watakapoweza kuwa makini kwa game zao za karibuni na kupata points zao muhimu..Safu ya ushambuliaji imekuwa haifanyi vizuri na tumekuwa tukipata magoli mengi kupitia kwa Oscar au Hazard...Tukiweza kuliona lango vizuri basi Kombe litaenda Stamford Bridge kirahisi kabisaa..

#ni hayo tu kwa leo....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom