Katika jamii iliyostaarabika, ukiona hujaridhika na jambo unafuata taratibu za kisheria, kijamii au kisiasa kutafuta utatuzi.
Uchaguzi ulikuwa huru na umefanyika kwa amani.
Kama kuna mgombea hajaridhika. Anatakiwa akashitaki mahakamani. Kama anaona mlango wa mahakama hauingiliki, basi afanye maongezi na upande wa pili kutafuta kile kinachoweza kumridhisha.
Ukiandamana tu bila kufanya jitihada za maongezi, hakuna mstaarabu yeyote duniani atakayekuunga mkono. Swali la kwanza utaulizwa, je ulifanya hatua gani kabla ya kuandamana? Ukisema hajafanya hatua nyingine yoyote, unaonekana mshari.
Kwahiyo, ushauri wangu, hawa ambao hawajaridhika wawasiliane na Humphrey Polepole wapange kufanya maongezi. Au wanaweza kumtafuta mzee kama Butiku akawasaidia kufikisha ujumbe wao kwa Bashiru.
Tanzania ni nchi ya amani. Tuilinde.