Binadamu lazima ujiulize maswali haya kabla siku haijaisha

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
52,470
70,590
1.Je, leo nina nafuu yoyote kuliko jana? Kama ipo ni ipi?

2. Ni Kitu gani kipya nimejifunza leo?kama hakuna basi soma hata kitabu ukurasa mmoja.

3. Kuna maamuzi yapi mapya au chaguzi zipi nimefanya kuboresha maisha yangu?

4.Kuna chochote nimefanya kwa ajili ya mtu mwingine au dunia kwa ujumla. Kumbuka sio kila zuri unalofanya lazima likufaidishe wewe au ndugu yako moja kwa moja, bali mazuri yaw engine ndiyo yatakayokunufaisha wewe na jamii yako.

5. Je, nimemuudhi nani leo? Au pengine
nimekwaruzana na nani? Na je nini hatma yake?

6. Je, nini umekifanya kwa ajili ya kesho?

7.Umetimiza kiasi gani mipango uliyojiwekea hapo kabla?

8. Nitafanya nini Kesho ili Kurekebisha nilipokosea leo?

9. Je , nimeonesha upendo kiasi gani kwa familia yangu kwa ujumla? mzazi, mke, mume, watoto au hata mpenzi wako.

10. Ni lipi limekuudhi zaidi na ni lipi limekufurahisha pia?
 
Shukrani sana ndugu kwa uzi huu maana ni adimu sana kwa nyakati hizi, ila hofu ni aina na idadi ya wachangiaji yaweza kuwa si kama ilivyotarajiwa.
 
1.Je, leo nina nafuu yoyote kuliko jana? Kama ipo ni ipi?

2. Ni Kitu gani kipya nimejifunza leo?kama hakuna basi soma hata kitabu ukurasa mmoja.

3. Kuna maamuzi yapi mapya au chaguzi zipi nimefanya kuboresha maisha yangu?

4.Kuna chochote nimefanya kwa ajili ya mtu mwingine au dunia kwa ujumla. Kumbuka sio kila zuri unalofanya lazima likufaidishe wewe au ndugu yako moja kwa moja, bali mazuri yaw engine ndiyo yatakayokunufaisha wewe na jamii yako.

5. Je, nimemuudhi nani leo? Au pengine
nimekwaruzana na nani? Na je nini hatma yake?

6. Je, nini umekifanya kwa ajili ya kesho?

7.Umetimiza kiasi gani mipango uliyojiwekea hapo kabla?

8. Nitafanya nini Kesho ili Kurekebisha nilipokosea leo?

9. Je , nimeonesha upendo kiasi gani kwa familia yangu kwa ujumla? mzazi, mke, mume, watoto au hata mpenzi wako.

10. Ni lipi limekuudhi zaidi na ni lipi limekufurahisha pia?
Anayesema anajiuliza maswali haya yote kila siku ama ni muongo ama hajui kupanga mipango ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu.

Siku nyingine nasahau hata kujiuliza kama nimekula lunch, nitapata wapi muda wa kujiuliza maswali yote hayo kila siku kama mtawa wa Delphi?
 
Back
Top Bottom