Binadamu kuanza kuchimba madini Angani

Binadamu kuanza kuchimba madini Angani

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
Fursa kwa watafuta ajira 😃 Angani watu wataanza kuchimba madini..!!!

1_20250328_112741_0000.png


💭 Miaka 30 iliyopita kwenye jalida la BBC Tomorrow iliweza kutabiri ifikapo mwaka 2025, binadamu wangeweza kuanza kuchimba madini kutoka kwenye miamba ya Angani (asteroids), japo Bado mpango huu ujakamilika kikamilifu lakini Tayari baadhi ya makampuni yameanza kazi.

4_20250328_112741_0003.png


💭 Kampuni ya Astro forge inakua kampuni ya kwanza yenye Makazi jiji la California kuweza kufanikisha uchimbaji wa madini Angani. Ilikua February 17 kampuni hiyo iliweza kuzindua chombo cha uchunguzi Odin kupitia Roketi ya SpaceX falcon 9.

🔅 Lengo lake kuu ni kufika kwenye kwenye miamba (OB5), umbali wa kilomita milioni 8 kutoka Dunia, ili kuchunguza madini yaliyoko huko. Safari hii inatarajiwa kuchukua miezi tisa.

2_20250328_112741_0001.png


💭 Hata hivyo, chombo cha Odin kilipata changamoto ya mawasiliano, hali inayofanya iwe vigumu kufuatilia mahali kilipo na harakati zake. Bado wataalamu wa AstroForge wanajitahidi kurejesha mawasiliano, wakitumaini kuwa chombo hicho kinaendelea na safari yake kama ilivyopangwa.

3_20250328_112741_0002.png


Credit to: #astronauts #bbclondon #bbcswahili #bongotech255
 
Back
Top Bottom