Binadamu akichoka,ni kiumbe hatari sana!

Binadamu akichoka,ni kiumbe hatari sana!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,198
Reaction score
162,735
Kweli binadamu akisema sasa basi nimechoka,hata ufanye nini huwezi kumbadilisha hata kama atakabiliwa na hatari kubwa mbele ya safari.

Cyber law ilianza tangu tarehe 01/09/2015 lakini nikiangalia lugha na yanayoendelea katika mitandao ya kijamii hasa kuhusiana na maswala ya uchaguzi mkuu,watu wanafunguka na kujiachi utazani hakuna sheria iliyotungwa.

Kuna wataokuja na hoja kwamba labda mpaka baadhi yao watolewe mfano ndio watu wataogopa,lakini sidhani kama watu watanyamaza kwa jinsi walivyochoka na kuishiwa uvumilivu.

Hata hivyo,tatizo kubwa ni wanasiasa wetu kutumia vibaya vyombo vya habari na majukwaa ya kisiasa kwa maslahi yao binafsi ili hali wananchi wamechoka na hawana pa kusemea(kujibu) zaidi ya kutumia mitandao hii ya kijamii.

Matumizi mabovu ya mitandao kwa kiasi fulani ni matokeo ya matumizi mabovu ya vyombo vya habari.

Mwanasiasa akitumia lugha chafu au propaganda majukwaani mwananchi wa kawaida atamjibu wapi zaidi ya kutumia hii mitandao?

It is a challenge; a real big challenge!

The law should be suspended otherwise we are heading for troube-a very seriuos one-as a nation.
 
Matumizi mabaga ikiwemo ya vyombo vya habari ikiwemo ipendeleo, hii imechangia kiasi kikubwa watu kutoa mawazo mbadala kwa njia hii. Mawazo hao yanaweza kuwa na mihemko lakini ujumbe unakuwa umefika.
 
Ni kweli nyuzi kibao hazina udadavuzi kama pale awali
 
Ni kweli nyuzi kibao hazina udadavuzi kama pale awali

Watanzania wamechukia.Kukatwa rasimu ya Katiba mpya ndio funga kazi, watanzania kwa pamoja wamekata shauri uvumilivu basi mabadiliko lazima.
 
Matumizi mabaga ikiwemo ya vyombo vya habari ikiwemo ipendeleo, hii imechangia kiasi kikubwa watu kutoa mawazo mbadala kwa njia hii. Mawazo hao yanaweza kuwa na mihemko lakini ujumbe unakuwa umefika.

Matumizi mabaya yakiwemo ya vyombo vya habari ukiwemo upendeleo, hii imechangia kiasi kikubwa watu kutoa mawazo mbadala kwa njia hii. Mawazo hayo yanaweza kuwa na mihemuko lakini ujumbe unakuwa umefika.
 
Na Ndiomaana Kila Siku Tunawaambia Ccm Kwamba Wametufanyia Mambo Mengi Mabaya, Maonezi Mengi, Lakini Uzalendo Ukitushinda, Nasema Uzalendo Ukitushinda, Tutafia Miguuni Mwao, Mwaka Huu Tumepanga Kufanya Siasa Za Kistaarabu Ila Wasituibie Kura Zetu
 
Watu wamepiga pesa mzee hapo, katika mchakato wa kuundwa hiyo sheria.... Tanzania hatuna wataalamu wala Teknolojia inayoweza kukabiliana na maswala ya kimtandano 100%.. yaani ni maneno bila vitendo na vitisho kwa wananchi ili kuwanyima uhuru wa kutumia teknolojia ya habari mawasiliano.
 
Matumizi mabaga ikiwemo ya vyombo vya habari ikiwemo ipendeleo, hii imechangia kiasi kikubwa watu kutoa mawazo mbadala kwa njia hii. Mawazo hao yanaweza kuwa na mihemko lakini ujumbe unakuwa umefika.

watanzania watapata wapi nafasi ya kujibu matusi kama "MALOFA" "WAPUMBAVU" zaidi ya mtandaoni? Magazeti ya kawaida wana edit mno NA wana nafasi ndogo,
 
Malofa na wapumbafu tunajipanga kweli hapa kukabiliana na oct 25.
 
Back
Top Bottom