Kuna wazo limenijia baada ya kupeleka gari yangu garage. Kama ilivyo tunavyotibiwa miili yetu katika hospitali kwa kutumia bima ya afya, ifike mahali sasa kuwe na bima ya afya ya magari na vyombo vingine vya moto na kama ilivyo kuna bima ya vyombo vya moto vinapopata ajali basi kuwe kuna bima special ambazo hu-cover na matengenezo ya gari na vipimo. Pia kuwe kuna garage ambazo zinapokea bima kama ilivyo kwenye hospitali.
Wataalam wa mambo ya bima tupeni mawazo yenu hili limekaaje kiuchumi, na pia watu mliozunguka sehemu mbali mbali duniani je hili lipo huko nchi zingine?
Ni wazo zuri sana, ila kimbembe kitakuja kwenye gharama,
Nahisi gharama yake kwa mwaka inaweza kukaribia gharama ya gari mpya au nusu.
Ikiwa chini ya hapo basi tutegemee kufungiwa spea feki.
Ni wazo zuri sana, ila kimbembe kitakuja kwenye gharama,
Nahisi gharama yake kwa mwaka inaweza kukaribia gharama ya gari mpya au nusu.
Ikiwa chini ya hapo basi tutegemee kufungiwa spea feki.
Alafu pia magari almost kila baada ya miezi miwili yanahitaji service, hiyo ni mandatory iwe nzima au mbovu. tofauti na mwili wa binadamu. kwahyo hapo bima lazima zile hasara.