Bima mkoani Kagera mnakwama wapi?

uncle regy

New Member
Joined
May 16, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Imekuwa ni kero ya muda mrefu kwa watumishi ambao tunafatilia vitambulisho vyetu vya bima mkoani kagera.

Kila ukienda wanakwambia vitambulisho havijakamilika kwa kisingizio cha kuharibika kwa mashine ya kutengenezea vitambulisho hivyo.

Hali hii imekuwa ya muda mrefu ilihali tunaendelea kukatwa kwenye mishahara yetu na kukosa huduma za kiafya pindi tunapozihitaji.

Nashauri Rais Magufuli autumbue uongozi mzima wa Bima Kagera kwa kushindwa kutoa huduma stahiki kwa wateja wake.

Naomba kuwasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…