Billionea rizi 1 nae kubambikiwa cheki feki?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Billionea rizi 1 nae kubambikiwa cheki feki??

Discussion in 'Jamii Photos' started by Pdidy, May 9, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Mmhhh unajua mtoto anaweza mambikiwa vitu feki labda kwa tamaa ya pesa lakini ukikuta familia ya vigogo kama rais anapigwa mchanga wa macho basi naomba msishangae kuona bilionea riz 1 nae kupewa cheki feki very soon maana kwa pesa aliokuwa nayo kwa kweli niliposoma niliomba kwenda haja

  polen familia ya kikwete ama ni mara ya kwanza kupokea cheki kwa style hiyo ama mkiona hela mnapigwa upofu hata fgr amsomi
  polen tena watoto watarajiwa maana yalipo mbele yenu ni makubwa kuliko haya
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  ALIANZA BABA


  <TABLE id=Table_01 border=0 cellSpacing=0 cellPadding=0 width=879 height=956><TBODY><TR><TD id=Top_Mid_Column bgColor=#ffffff><TABLE id=tp_F4 border=0 cellSpacing=0 cellPadding=0 width=599><TBODY><TR><TD vAlign=top>
  Mkuu wa mkoa umemfedhehesha Rais
  [​IMG]


  Mobini Sarya

  </TD></TR></TBODY></TABLE></TD><TD style="BACKGROUND-REPEAT: repeat-x" id=Right_Column bgColor=#ffffff vAlign=top background=images/grad2.gif rowSpan=2 width=140 align=middle>[​IMG] </TD></TR><TR><TD id=Mid_Column><TABLE id=F4 border=0 cellSpacing=0 cellPadding=0 width=599 bgColor=#ffffff height=696><TBODY><TR vAlign=top><TD style="PADDING-LEFT: 45px; PADDING-RIGHT: 45px" vAlign=top>
  KAMA ningekuwa Mkuu wa Mkoa (RC) wa Arusha, ningejiuzulu haraka pamoja na Katibu Tawala wangu (RAS), kwa kumfedhehesha kiongozi wangu na kushindwa kuonyesha umakini kwenye kazi yangu.
  Ningefanya hivyo si kwa kumuogopa kiongozi wangu, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali ni kwa kuonyesha uwajibikaji, kwa kitendo cha kumfedhehesha mkuu wangu.
  Kauli yangu hii inatokana na kitendo cha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kumtuma Mkurugenzi wa Wilaya ya Ngorongoro, Kayange Jacob, kwenda Ikulu, Dar es Salaam, kukabidhiwa gari la wagonjwa na rais, ambapo haikumpasa.
  Ingawa Rais Kikwete mwenyewe alibaini kuwa mkurugenzi huyo hakuwa mhusika na hivyo kuahirisha shughuli nzima ya kukabidhi magari ya wagonjwa kwa halmashauri za wilaya za Mbozi na Longido.
  Kwa hilo sina budi kumpongeza Rais kwa umakini aliouonyesha ilhali akiwa anakabiliwa na mambo mengi ya shughuli za kiserikali.
  Ingawa kuna taarifa nyingine zinadai kuwa baadaye jioni Kikwete alimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi, Levison Jeremiah Chilewa, kwa ajili ya wakazi wa eneo la Kamsamba, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya, lakini Longido walikabidhiwa gari hilo siku iliyofuata baada ya mkurugenzi husika kufika katika eneo hilo.
  Watu wa Ngorongoro hawakulipata gari hilo kwa sababu rais alikuwa amekusudia kulitoa kwa wakazi wa Wilaya ya Longido, kwani walikuwa wameliomba wakati alipofanya ziara katika Kijiji cha Engalinaibo.
  Licha ya rais kuagiza katibu wa Ikulu amuarifu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ili amtume Mkurugenzi wa Longido na madereva wawili ambao wangepatiwa mafunzo ya kuendesha gari hilo, lakini akapelekwa mkurugenzi mwingine ambaye hahusiki na sehemu aliyokusudia rais kuipatia gari.
  Kitendo hicho kimeonekana kumuudhi mkuu wa nchi hadi akatamka maneno makali. “Hii ni kashfa kubwa, nakumbuka vizuri msaada huu niliahidi kuwapa wananchi wa Wilaya ya Longido wakati nilipofanya ziara katika Kijiji cha Engalinaibo, kipindi cha ukame, ambapo nilifika katika kituo cha afya,” alisema rais.
  “Wewe bwana unatoka wapi?” alihoji Rais Kikwete kwa jazba.
  Kisha akaongeza: “Hapa umefikaje? Umekuja kufanya nini na nani kakualika?”
  Hizi kauli mbili zinaonyesha jinsi rais alivyokerwa na kuhuzunishwa na kitendo cha wasaidizi wake kumchomekea.
  Siwezi kuendelea kunukuu kila jambo ambalo rais alilisema wakati akifoka lakini ni dhahiri kwamba rais sasa amechoka kudanganywa na watu anaowaamini, ambao ni wasaidizi wake.
  Hii si mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kudanganywa, itakumbukwa kuwa miezi michache tu baada ya kuingia madarakani alikutanishwa na kampuni za kuchimba madini, kisha tukatangaziwa kuwa rais amefanikiwa kuwashawishi wachimba madini kuongeza kodi.
  Haikupita muda kabla wanasheria, akiwamo Tundu Lisu kutamka wazi kuwa ‘Rais amedanganywa’, kwa sababu kiasi cha kodi alichokuwa ameambiwa na wachimbaji hao ni kidogo ikilinganishwa na kile ambacho mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, alikuwa amewapangia.
  Mwaka mmoja baadaye wasaidizi wa rais Ikulu walishindwa kubaini hundi feki aliyokuwa anakabidhiwa rais na benki moja ya hapa nchini, ambapo kiasi cha fedha kwa tarakimu kilikuwa tofauti na kwa maneno.
  Baadhi ya watu waliozungumzia tukio lile walisema kuwa kama ungekuwa ni mkataba, tayari ulikuwa umekwishasainiwa kiuzembe na taifa lingeingia hasara kubwa.
  Baada ya dosari hiyo, leo mkuu wa mkoa anamtuma mtumishi ambaye hakupaswa kwenda Ikulu na wasaidizi wa rais waliohusika kutoa mwaliko wakashindwa kumtambua hadi Rais Kikwete mwenyewe alipomuumbua.
  Wakati rais anang’amua uzembe huo, tayari mkurugenzi huyo alishatumia gharama za serikali kuja Dar es Salaam na kulipwa posho. Kibaya zaidi, madereva wawili wasiohusika wamekwishapewa mafunzo kwa muda wa wiki nzima ili wawe wanaendesha gari lile.
  Kutokana na uzembe huu, hatujui ni nani atalipa gharama hizo, ambazo zimesababishwa na wazembe waliomo serikalini, kuanzia Arusha hadi Ikulu.
  Rais Kikwete anayo kazi moja tu ya kuwafukuza kazi wazembe wote waliohusika katika tukio hilo, kuanzia wasaidizi wake wa Ikulu hadi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kwa tukio hilo la kufedhehesha.
  Pia namshauri Rais Kikwete ampandishe cheo mkurugenzi wa Ngorongoro aliyekuwa ametumwa Ikulu kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha ili aweze kufarijika kutokana na mfadhaiko aliokutana nao Ikulu.
  Ni wazi kuwa pamoja na Rais Kikwete kukasirishwa na tukio hilo la aibu, pia mkurugenzi yule atakuwa amefedheheka na kuogopa, baada ya kufukuzwa Ikulu. Pia namshauri Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati akijiandaa kukabidhi ofisi amuombe radhi mkurugenzi yule kwa kitendo chake cha kumtuma Ikulu wakati yeye hakuwa mhusika aliyekusudiwa. Rais wangu Kikwete, wameshindwa kujiuzulu, wafukuze leo kabla jua halijazama, kwa sababu kwa uzembe huu ipo siku watauza nchi.


  </TD></TR></TBODY></TABLE></TD></TR></TBODY></TABLE>
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu siku zote uwa sikuelewi maana unaandika huku unakimbia:israel::israel:
   
 4. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  riz unaruhusiwa kuoa wake 4,chagua naona wengi wanalipenda jina lako kaka hop c unajua wengine hawawez kusema mpaka wapitie lugha ya cheki
   
Loading...