Bilionea wa home shopping centre ashindikana kutibiwa

Bilionea wa home shopping centre ashindikana kutibiwa

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,848
attachment.php



Hakika aliyemmwagia tindikali bilionea Said Mohamed Saad, alifanya kitendo kibaya kupitiliza, kwani athari ambazo amemsababishia ni kubwa kiasi ambacho hata upatikanaji wa tiba mahsusi umekuwa wa kutangatanga.


attachment.php

Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali bilionea Said Mohamed Saad hospitalini.

Gazeti hili linazo taarifa za ndani na zenye uhakika kuwa Said ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping Centre, amekimbizwa Ujerumani kwa matibabu zaidi baada ya kushindikana Afrika Kusini alikopelekwa awali.

Said alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa kwenye moja ya maduka yake yaliyopo kwenye jengo analodaiwa kulimiliki la Msasani Mall.
Ilielezwa kuwa baada ya kumwagiwa tindikali, alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ami Wellness Centre iliyopo Masaki, Dar es Salaam lakini ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60, alichukuliwa na kupandishwa ndege kupelekwa Afrika Kusini.


attachment.php


Said Mohamed Saad akiwa hospitali.


AFRIKA KUSINI MATUMAINI KIDOGO

Ndugu wa Said aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini, alisema kuwa akiwa Afrika Kusini, ilionekana kwamba bilionea huyo anatakiwa kufanyiwa oparesheni ya uso ili kuondoa ngozi iliyoathiriwa na tindikali, vilevile kulifanyia jicho upasuaji.

"Sehemu ya usoni kushuka kifuani upande wa kulia na mkono wenyewe wa kulia ndiyo maeneo katika mwili wa ndugu yetu yaliyoathirika zaidi na tindikali," alisema ndugu huyo wa ndani kabisa kwa sharti la kutotajwa jina na kuongeza:

"Jicho la kulia lenyewe limepata athari kidogo, kwani inaonekana wakati mmwagaji akifanya kile kitendo, yeye alifumba macho kwa hiyo tindikali haikuingia ndani ya jicho, iliishia kwa juu.

"Ila kwa vile tindikali ilimwagika kwa wingi juu kwenye jicho la kulia na kutokana na ukali wa tindikali aliyomwagiwa, imesababisha kutengenezwa kwa mtoto wa jicho kwa hiyo hawezi kuona mbali.

"Uamuzi wa kumpeleka Ujerumani uliafikiwa baada ya kujiridhisha kwamba kule kuna wataalamu kuliko Afrika Kusini. Oparesheni ya uso kubadili ngozi iliyoathirika, vilevile kufanya upasuaji wa jicho na kuliweka sawa ni mambo ambayo tulijiridhisha yanawezekana Ujerumani."

AKATAA KUTAJA JINA LA HOSPITALI
Kwa mujibu wa ndugu huyo, Said aliondolewa Afrika Kusini na kupelekwa Ujerumani, Agosti 3, mwaka huu na tangu hapo taarifa zake zimefanywa siri kubwa ili kulinda usalama wake.
"Hata wakati nazungumza na wewe kama mwandishi wa habari, nilijua tu lazima utaniuliza kuhusu jina la hospitali aliyolazwa Ujerumani. Ukweli ni kwamba siwezi kukwambia. Tunafanya hivyo kwa ajili ya usalama wa ndugu yetu.

"Tukio la kumwagiwa tindikali ni zito sana, imeshajionesha wazi namna ambavyo kuna watu hawampendi, hao maadui wakijua hospitali aliyolazwa, wanaweza kufanya juu chini wamfikie na kumdhuru kwa mara nyingine. Hilo jambo hatutaki kabisa litokee," alisema ndugu huyo.

NDUGU, WATOTO WAKE WAZUIWA KWENDA UJERUMANI
Habari zaidi zinabainisha kuwa ndugu wa Said walipanga kwenda Ujerumani kumtembelea lakini walizuiwa kwa sababu awamu hii, viongozi wa familia yake wamezingatia usiri.
"Kuna watoto wake walikwenda Afrika Kusini na walikuwepo wakati anasafirishwa kwenda Ujerumani lakini waliambiwa warudi Tanzania kwa sababu kule Ujerumani utaratibu umebadilika. Watu wachache wanaohusika na huduma pamoja na usalama wake ndiyo pekee wanaoruhusiwa," alisema, akaongeza:

"Wapo ndugu wengine kutoka Saudi Arabia na Oman, vilevile nao wamezuiwa kwenda Ujerumani kumwona. Ni katika kuhakikisha mambo hayawi kama ilivyokuwa Afrika Kusini, maana kule ilishakuwa hatari, ndugu wengine wanaingia wodini, wanampiga picha na kusambaza mitandaoni. Safari hii mambo hayo hayatakiwi."

APELEKWA UJERUMANI BAADA YA JK
Imeelezwa kwamba Said alipelekwa Ujerumani wiki moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kwenda kumtembelea alipokuwa amelazwa kwenye hospitali moja nchini Afrika Kusini.
Dk. Kikwete, alikuwa kwenye ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini alipokwenda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika (SADC), kuhusu pande tatu za umoja huo (Troika of SADC), hivyo kupata fursa ya kwenda kumjulia hali.


MUNGU AMPONYE SAIDI
Dawati la gazeti hili linamuombea Said apone kwani alionesha moyo wa ukarimu kwa familia 655 zilizokumbwa na mafuriko eneo la Jangwani, Desemba, 2011 kisha kuhamishiwa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.


MTUHUMIWA BADO KUKAMATWA
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura alisema kwamba jeshi la polisi linaendelea kufanya kazi kwa nguvu na umakini mkubwa lakini mpaka sasa halijafanikiwa kumpata mtuhumiwa.


Chanzo.
BILIONEA WA HOME SHOPPING CENTRE ASHINDIKANA KUTIBIWA - Global Publishers
 

Attachments

  • kikwete  homeshopig  cetre.jpg
    kikwete homeshopig cetre.jpg
    37.6 KB · Views: 5,802
  • BILIONEA.jpg
    BILIONEA.jpg
    49.1 KB · Views: 5,829
Very soon wachina watabuni 'anti-acid cloth'; mavazi ya aina yake ambayo mtu utakuwa unavaa tindikali haikuathiri na watapata soko zuri tu Tz
 

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP Camillius Wambura alisema kwamba
jeshi la polisi linaendelea kufanya kazi kwa nguvu na umakini mkubwa lakini mpaka sasa halijafanikiwa kumpata mtuhumiwa.


Mkuu MziziMkavu,
Hii wazungu wanaita "an insult to human intelligence".
 
Last edited by a moderator:
Pesa sio kila kitu, mhimu ni kuishi kwa upendo na amani.

usipende kuwatendea vibaya wenzio.!!

Mkuu una ushahidi aliwatendea vibaya wenzake?
Kwani wanaodhuriwa wote wametenda ubaya?
Hivi unajua biashara yako ikiwa tishio kwenye kuteka wateja wa mfanyabiashara mwingine unaweza ukadhuriwa pia? sasa hapo kosa lako ni lipi?
Tumeshuhudia baadhi ya sehemu TZ wachawi wanahangaika kumroga mtu kisa amejenga nyumba ya tofali kaezeka na vigae wakati nyumba nyingi mtaani ni za udogo, sasa kosa la huyo mtu ni nini?

Kwa kifupi, watu wanaweza kukudhuru hata kama hujafanya kosa. Mifano ipo mingi mno ninauhakika hata wewe ipo unayoifahamu.
 
Ndio tabu ya watu wanaojiita mabilionea..wanadhani ukishamiliki fedha basi ndio umekata kibali cha kumtendea mwenzako lolote baya...kwa sababu ya pesa zake anajua hakuna wakumgusa.....RIP billionea..
 
Mkuu una ushahidi aliwatendea vibaya wenzake?
Kwani wanaodhuriwa wote wametenda ubaya?
Hivi unajua biashara yako ikiwa tishio kwenye kuteka wateja wa mfanyabiashara mwingine unaweza ukadhuriwa pia? sasa hapo kosa lako ni lipi?
Tumeshuhudia baadhi ya sehemu TZ wachawi wanahangaika kumroga mtu kisa amejenga nyumba ya tofali kaezeka na vigae wakati nyumba nyingi mtaani ni za udogo, sasa kosa la huyo mtu ni nini?

Kwa kifupi, watu wanaweza kukudhuru hata kama hujafanya kosa. Mifano ipo mingi mno ninauhakika hata wewe ipo unayoifahamu.

Mkuu kuna uzi humu ndani unaeleza kwa kirefu sana kuhusu tuhuma za ajabu kuhusu huyo ndugu.

watu wameuwawa,kupigwa risasi za miguu,kubakwa, kulawitiwa, madawa ya kulevya dhuluma na mengineyo kupitia mikono yake au kikundi chake cha kihalifu....

utafute uusome.!!!
 
Mkuu kuna uzi humu ndani unaeleza kwa kirefu sana kuhusu tuhuma za ajabu kuhusu huyo ndugu.

watu wameuwawa,kupigwa risasi za miguu,kubakwa, kulawitiwa, madawa ya kulevya dhuluma na mengineyo kupitia mikono yake au kikundi chake cha kihalifu....

utafute uusome.!!!

uzi wenyewe huu hapa



[h=2]Changia Tshs 30,000/= Kwa Mwaka ili kuiwezesha JamiiForums na upate kuwa JF Gold Member, Ujulishwe kinachojiri kwa SMS BURE Mwaka Mzima --> Bofya hapa kwa maelezo zaidi [/h]
















  • [h=2]
    icon1.png
    Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center[/h]
    Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

    Utangulizi

    Mfanyabiashara Said Mohammed Saad anamiliki Kampuni ya Home Shopping Center iliyopo Kariakoo Mtaa wa Swahili na Msimbazi katika Jengo la Ghorofa lenye vioo vilivyochorwa picha za waigizaji wa Kikundi cha Orijino Commedy kinachorusha vipindi vyake Televisheni ya taifa ya TBC1.

    Mfanyabiashara huyu ambaye ana uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Saud Arabia, anafanya uhalifu na kuhujumu uchumi nchi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine wakubwa

    Tuhuma

    Mfanyabiashara Said Mohammed ameshiriki katika matukio mengi ya kihalifu yakiwamo ya kupiga risasi watu na kesi zake zimekuwa zikifunguliwa na baadaye anazizima kwa kutoa rushwa polisi.

    Moja ya matukio hayo ni kumpiga risasi mfanyakazi wake mwaka 2005 wakati akishusha bidhaa za kuuza dukani kutoka katika gari lake, kumpiga risasi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Vingunguti, Deo Vicent Agosti 15, 2006 saa 1:00 usiku Mtaa wa Msimbazi na Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam.

    Mfanyakazi wake alimpiga baada ya kumbishia Said kwamba hawezi kumpiga risasi kwa sababu anajua sheria za nchi haziruhusu kufanya hivyo. Alimpiga kuonyesha kwamba yeye yupo juu ya sheria za nchi. Kesi hiyo nayo aliimaliza kimya kimya kwa kumpa hela mfanyakazi huyo na ndugu zake na polisi.

    Mtoto Vicent yeye baada ya kupigwa risasi aliliripoti Polisi na baadaye alilazwa katika Wodi namba 17 Moi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Alipigwa risasi ya mguuni wakati akipita karibu na duka la Said baada ya mashabiki wa Simba waliokuwa wakisherekea ushindi wa timu yao kupita katika eneo hilo.

    Hata hivyo, alimaliza kesi hiyo nje ya mahakamani kwa kuwapa hela wazazi wa mtoto huyo.

    Pia anamiliki genge la Wahalifu ambalo analitumia kumlinda na kuwaadhibu wapinzani wake au maadui zake akishirikiana na mdogo wake Ghalib Mohammed Saad.

    Kundi hilo linalojulikana kama Ze Popobawa ndilo ambalo Agosti mwaka huu lilitumika kumteka nyara Mlebanoni mfanyabiashara ambaye ana duka la vitu vya ndani Mtaa wa Morogoro karibu na makutano ya barabara za Morogoro na Bibi Titi na baadaye kumwingilia kinyume cha maumbile kisha kumpeleka kwa nguvu Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumrejesha kwao Yemen kinyume cha taratibu.

    Kisa kilichofanya mfanyabiashara huyo ambaye yupo nchini kisheria ni kumpa mimba mdogo wa Said anayeitwa Salha bila ya kuoana kama zilivyotaratibu za mila zao za Yemeni.

    Mfanyabiashra huyo wa Mlebanoni ambaye awali alikuwa rafiki yake mkubwa na Said, amemfanya tangu tukio hilo litokee kuishi kwa kujificha kwa kuhofia kufanyiwa unyama mwingine na Said ambaye anaendelea kumtisha.

    Unyama mwingine

    Baada ya kumfanyia unyama mfanyabiashra Mlebanoni , Said hakuishia hapo bali aliamua kumwadhibu dada yake Salha kwa kumpiga. kumnyoa nywele zake zote na kumnywesha vidonge ambavyo havijulikani aina yake na alimpa kwa sababu zipi?

    Salha baada ya kufanyiwa nyama huo nyumbani kwao Msasani wilaya Kinondoni aliamua kwenda kuripoti polisi kituo cha Osterbay ambako lilifunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/13915 ambayo ilifunguliwa Agosti 5 mwaka huu.

    Hata hivyo, mbali ya polisi kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini wanashangaa tangu Salha aripoti tukio hilo, hajarudi kituoni hapo wala simu yake mkononi ambayo aliicha namba zake kituoni hapo wakati akiandikisha maelezo haipatikani, kitu ambacho kinawapa wasiwasi.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye anasema huenda suala hilo wamelimaliza kifamilia. Ingawa kuna tariafa kuwa msichana huyo amewekwa kizuizini chumbani ambako haruhusiwi kutoka nje. Polisi kituo cha Oysterbay hawajafuatilia suala hilo kutokana na kupozwa kwa kupewa kitu kidogo rushwa na Said ili kuzima suala hilo.

    Ushirika wa kihalifu

    Kutokana na kushirikiana vyema katika shughuli za dawa za kulevya na kutorosha nyara za taifa wakimtumia Mfanyabiashara huyu, Said, Manji ameamua kumpa vijana wake wa Orijino Commedy kuwapa ufadhili wa kutangaza bidhaa zake anazoingiza nchini za mashuka na nguo.

    Hivi karibuni baada ya Manji kushiriki katika kuigiza mchezo wa kikundi cha Orijino Comedy kama mfanyabishara ambaye alikuwa akihitaji msaada wa kupata fedha za kufadhili Klabu ya Yanga na kuwapa wagizaji wa kikundi hicho kutumia ofisi yake kuigiza, Said naye wiki iliyofuatia aliwapa wana kikundi hicho nafasi kuingiza katika ofisi yake na kuwapa gari lake kulitumia.

    Wizi wa makontena bandarini

    1. Mfanyabiashara huyu anamiliki kampuni nyingi za Clearing and Forwarding ambazo hutumika kuiba makontena ya bidhaa anazoziingiza nchini kutoka nje na akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa TRA.

    Hata hivyo, Kampuni hizi zimefungiwa baada ya kubaini kuhusika na wizi huo wa makontena, lakini kila inayofungiwa husajili nyingine Brela akitumia majina feki.

    Kampuni ambazo zimefungiwa na TRA kwa kuhusika na wizi wa makontena zaidi ya 30 kila moja ni Mbasi Clearing and Fowarding, Clinton Clearing and Forwarding, London Freight Forwarding, Exceptional Freight Forwaders na Upland Clearing and Forwarding.

    TRA imethibitisha kuzifungia kampuni hizo kufanya kazi ya Clearing and Fowading, kwa kutumia kifungu 145 (3) cha sheria ya Jumuia ya Afrika Mashariki ya utawala wa Forodha ya mwaka 2004.

    Hata hivyo, wamekataa kutaja majina ya wamiliki wa kampuni hizo wakisema Brela ndio wenye jukumu hilo. Ingawa wamekuwa wakikubali kuendelea kumhudumia mteja huyo huyo ambaye anaiba makontena na kufungiwa kampuni zake kisha anafungua nyingine chap chap kama uyoga.

    Hata hivyo, Brela kuna kumbukumbu ya kampuni mbili tu ambazo ni London Freight Fowarders Ltd yenye usajili namba 39834 iliyosajiliwa Agosti 15, 2000 ikionyesha wamiliki wake ni Angelo Peter mwenye hisa 2000, Richard Mulenga mwenye hisa 1500 na Abdulkarim Zaharan Salim mwenye hisa 1500. Kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

    Kampuni nyingine za kwake zenye kumbukumbu Brela ni Exceptional Freight Fowarders Ltd ambayo wamiliki wake ni Lumba Nguku mwenye hisa 5,000 na Salim Suleiman mwenye hisa 5,000. Kampuni ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

    Dawa za kulevya na kutorosha nyara

    Mfanyabiashara huyu anajihusisha na uingizaji wa dawa za kulevya nchini kwa kushirikiana na mfanyabiashara Manji wakitumia kampuni zake za Clearing and Fowarding ambazo huiba makontena yenye dawa hizo yanapoingia bandarini.

    Mfanyabiashara huyu ni mmoja wa watu waliotajwa katika orodha ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya iliyowasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2006 akitajwa kama Said Abuu mfanyabiashra wa Kariakoo.

    Nyara za taifa

    Mfanyabiashara huyu amekuwa akitumia kampuni zake kusafirisha makontena yenye nyara za taifa kwenda Vietnam, Philipiness na Malaysia akishirikiana Manji na Rostam Aziz ambaye pia ni mmiliki vitalu vya uwindaji. Kampuni ya Rostam ya Uwindaji inaendeshwa na mdogo wake anayeitwa Akram.

    Ili kufanikisha mtandao wao huo wana watu wao katika sehemu nyeti za TRA, bandari, Polisi na usalama wa taifa unaowalinda kwa hali na mali.

    Utajiri wa kutisha

    Kutokana na Said kujihusisha na biashara hizo haramu kwa muda mfupi tangu mwaka 2004 alipoanza hivi sasa ana utajiri wa kutisha. Anamiliki nyumba sita eneo la Kariakoo pekee.

    1. Moja ipo Swahili na Msimbazi, Ghorofa saba ambayo ameamua kuipangisha watu sehemu ya juu, lakini TRA akidaganya kwamba ni hoteli ili kukwepa kulipa kodi. 2. Congo na Agrey ghorofa sita, 3. Uhuru mkabala na shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa bado inajengwa ni ya ghorofa, 4. Livingstone na Uhuru ipo, 5. Mkunguni Kariakoo Sokoni karibu na dula la Azam Ice Cream ghorofa sita, 6. Lumumba karibu na CCM makao makuu limepakana na Hospitali ya Burhan.​




 
Napata tabu kuamini kwamba mtu anaweza kukumwagia acid bila sababu nafikiri kuna dhuluma au kiburi cha pesa kwa huyo tajiri wa kibongo, inasemekana amekuwa akifanya vitendo vya kishenzi na kutofanywa lolote na vyombo vya sheria, Kama hayo yana ukweli basi naomba mungu aendelee kumpa uhai ila makovu aliyonayo apate kukumbuka nobody is untouchable no matter how powerful you're.
 
Mmh! Hivi wote wanaomwagiwa tindikali wamewatendea wenzao vibaya ? Nadhani tusihukumu kwani haya yanaweza kumtokea mtu yeyote. Isitoshe hata kama mtu kamtendea vibaya mwenzie anastahili kufanyiwa hivi? Huyu anyefanya hivi anakuwa tofauti naye? Si nayeye anakuwa amemtendea mwenzie ubaya??? Kwa hiyo wote wanakuwa wabaya!!!
Pesa sio kila kitu, mhimu ni kuishi kwa upendo na amani.

usipende kuwatendea vibaya wenzio.!!
 
Yaan huyu afe kabsa ,mabaunsa wake walikuwa wap akimwagiwa? Yaan ingewezekana aogeshwe kwenye pipa zima la tindkali
 
Back
Top Bottom