Bilionea Richard Branson asitisha mradi wa 1$ Billion na Saudi Arabia Baada ya KUPOTEA kwa Mwandishi wa Washington Post

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
- Hii ni baada ya kupotea katika hali isiyoyakikawaida kwa Muandishi wa Gazeti la Kimarekani Washinton Post na Mkosoaji wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi.

- Utata wa kupotea kwake bado haijajulikana japo marekani inawatupia lawama Serikali ya Saudia.
-Pia marekani inafikilia kuweka vikwazo ikiwa itathibitika Saudia imehusika.

My Take.
Kwa dunia hii, cheza na vyote ila sio Raia wa US, unaweza kujikuta unanunua kitunguu sokoni kwa shilingi billioni moja wakiamua kukubinya kiuchumi ukiingia anga zao. Inanikumbusha na Movie inaitwa Tears of the Sun, Kikosi cha makomandoo kilichotumwa eneo la hatari kabisa huko West Afrika Kumuokoa Dada wa kimarekani katikati ya Msitu uliojaa waasi mamia na makatili kupita kiasi.

Chanzo.
New York Post
 
Acha kuwafagilia usa kiasi hicho kijana mdogo, jamaa ni wajanja na waongo wa kukubuu walahi
Saudi na usa ni pete na kidole walahi
Changa la macho kwa katoto hilo, kuwa uyaone kijana mdogo walahi
 
naona hapo kuna mgongano wa mavibaraka.
ila mkuu mtu mwenye maslahi na marekani ukimzingua lazima upate tabu sana.
Tafuta Habari ya Kibaraka Mkongwe wa America anaitwa Abdallah Ocalan aliekuwa Mkuu wa Waasi wa Wakurdi Wanaopigania kujitenga Toka Turkey

Alikuja kukamatwa Ubalozi wa Greece Nchini Kenya Na CIA Na kukabidhiwa Kwa Turkey ili Turkey itoe Anga lake kumchakazia Saddam Hussein wakati Ni America ndio ilikuwa imemficha huko Kwa Miaka yote
 
Acha kuwafagilia usa kiasi hicho kijana mdogo, jamaa ni wajanja na waongo wa kukubuu walahi
Saudi na usa ni pete na kidole walahi
Changa la macho kwa katoto hilo, kuwa uyaone kijana mdogo walahi
hii ni habari mkuu sio ufagio.
kuhusu ukibaraka hiyo nayo ni habari nyingine
 
Tafuta Habari ya Kibaraka Mkongwe wa America anaitwa Abdallah Ocalan aliekuwa Mkuu wa Waasi wa Wakurdi Wanaopigania kujitenga Toka Turkey

Alikuja kukamatwa Ubalozi wa Greece Nchini Kenya Na CIA Na kukabidhiwa Kwa Turkey ili Turkey itoe Anga lake kumchakazia Saddam Hussein wakati Ni America ndio ilikuwa imemficha huko Kwa Miaka yote
habari ni mwandishi wa gazei kupotea.
habari ni matokeo ya kupotea kwa mwandishi huyo na kampuni la mzee Branson, Virgin kusitisha mradi wake na Saudia hadi ufafanuzi uwe wazi.
hayo maelezo mengine mkuu yanaweza kuwa sahihi lakini ni Tangential to the thread on table.
 
hakuna watu wanafiki kama USA
 
naona hapo kuna mgongano wa mavibaraka.
ila mkuu mtu mwenye maslahi na marekani ukimzingua lazima upate tabu sana.
Marekani inahitaji uhusiano mzuri na Saudi Arabia kuliko ambavyo Saudia ina inavyo hitaji ushirikiano na Marekani.

Kuvunja uhusiano na Saudia ni kuvunja nguvu za dola kuwa fedha ya manunuzi ktk soko la dunia. Kumbuka mikataba ya Petro dollar.

Marekani akigomabana na Saudia, Yemeni, Iran na Syria na hao jamaa wote wakajiunga na Russia na China unaweza kukuta matumizi ya dhahabu ktk manunuzi inarudi na kuipoteza dollar kisha Euro au Rubble(ya Russia) au fedha ya China inashika soko.

Sasa huwezi kununua mafuta bila dollar na hii inatokana na mikataba ya Saudia na Marekani pamoja na nchi zingine chache. Imagine Saudia akisema sasa siuzi mafuta kwa dollar nanunua vitu na kuuza mafuta kwa dhahabu au fedha nyingine itakuwaje?

Fikiria Saudia akizuia kununua silaha toka Marekani kama vile sasa alivyo goma vitu vya Canada itakuwaje viwanda vikubwa vya silaha vya Marekani ambavyo vinavyokuza uchumi wa Marekani?

Kumbuka Saudia inatumika sana kueneza ushawishi wa Marekani eneo la nchi za kiarabu na kiajemi.

Cc: Malcom Lumumba
 
habari ni mwandishi wa gazei kupotea.
habari ni matokeo ya kupotea kwa mwandishi huyo na kampuni la mzee Branson, Virgin kusitisha mradi wake na Saudia hadi ufafanuzi uwe wazi.
hayo maelezo mengine mkuu yanaweza kuwa sahihi lakini ni Tangential to the thread on table.
Lengo ka kuandika haya niliyoandika sio kukutoa nje ya Mada Au kuharibu uzi, lengo Ni kukumbusha undumilakuwili wa America inapokuja kwny Maslahi yake

America haiwezi kugombana Na Saudia ili kumtetea Mwandishi ambae tayari amekufa

Kama umekwazika niwie radhi!
 
Marekani anawayanyasa waarabu na sehemu kubwa ya dunia sababu ya unafiki wa wafalme wa Saudi Arabia na viongozi wengine wa nchi hizo za mashariki ya kati.

Siku wakiamka na dunia itakombolewa mikononi mwa ubabe wa Marekani kiuchumi na kijeshi.
 
CNN wanasema Upo ushahidi usiotia Shaka kuwa mwandishi huyo aliuwawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia Uturuki.
 
Lengo ka kuandika haya niliyoandika sio kukutoa nje ya Mada Au kuharibu uzi, lengo Ni kukumbusha undumilakuwili wa America inapokuja kwny Maslahi yake

America haiwezi kugombana Na Saudia ili kumtetea Mwandishi ambae tayari amekufa

Kama umekwazika niwie radhi!
sawa mkuu. sijawahi kukwazwa humu jf maana kigezo cha kuandika chochote humu ni utayari wa kupata jibu lolote bila kujali kama zuri au baya au la pembeni.
namkumbuka rais mmoja wa US aliwahi kusema wao wanaangalia America haina urafiki wa Kudumu bali maslahi ya kudumu.
hivyo hata hilo suala kama maslahi yatakuwa kwa huyo muandishi Saudia itapata changamoto kidogo. Ila kama ni kote hii itabaki kuwa danganya toto na mfano ulioutoa utakuwa na mashiko.

karibu.
 
Unahahika ni raia wa Marekani?

Halafu New York Post is a known tabloid, huwa halitumiwi kama quotable source
sijasema Jamal ni mmarekani, ila nimesema kwa ujumla raia wa US sio wakuchezewa. Kwa sababu na yeye alifanya kazi kwa maslahi ya US, Kwenye gazeti la US ndio maana hata Maseneta wa US wanampressure trump na serikali yake wafanye investigation ya tukio hilo.
Hiyo habari haijaandikwa na NYP tu. magazeti mengi lkn pia hata huyo dingi mwenyewe billionea twitter ametoa tamko kwa ufalme wa saudia arabia mkuu, huwa namfuatilia article zake twitter na linkedin.

maoni lkn.
 
Back
Top Bottom