Bilionea Richard Branson asitisha mradi wa 1$ Billion na Saudi Arabia Baada ya KUPOTEA kwa Mwandishi wa Washington Post

- Hii ni baada ya kupotea katika hali isiyoyakikawaida kwa Muandishi wa Gazeti la Kimarekani Washinton Post na Mkosoaji wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi.

- Utata wa kupotea kwake bado haijajulikana japo marekani inawatupia lawama Serikali ya Saudia.
-Pia marekani inafikilia kuweka vikwazo ikiwa itathibitika Saudia imehusika.

My Take.
Kwa dunia hii, cheza na vyote ila sio Raia wa US, unaweza kujikuta unanunua kitunguu sokoni kwa shilingi billioni moja wakiamua kukubinya kiuchumi ukiingia anga zao. Inanikumbusha na Movie inaitwa Tears of the Sun, Kikosi cha makomandoo kilichotumwa eneo la hatari kabisa huko West Afrika Kumuokoa Dada wa kimarekani katikati ya Msitu uliojaa waasi mamia na makatili kupita kiasi.

Chanzo.
New York Post
Uongo iran kawekewa vikwazo miaka mingap Korea kazkazin je kwa taarifa yako vikwazo akiviweka kwa saud Arabia havita kua na athar yoyote
 
Marekani inahitaji uhusiano mzuri na Saudi Arabia kuliko ambavyo Saudia ina invyo hitaji ushirikiano na Marekani.

Kuvunja uhusiano na Saudia ni kuvunja nguvu za dola kuwa fedha ya manunuzi ktk soko la dunia. Kumbuka mikataba ya Petro dollar.

Marekani akigomabana na Saudia, Yemeni, Iran na Syria na hao jamaa wote wakajiunga na Russia na China unaweza kukuta matumizi ya dhahabu ktk manunuzi inarudi na kuipiteza dollar au Euro au Rubble(ya Russia) au fedha ya China inashika soko.

Sasa huwezi kununua mafuta bila dollar na hii inatokana na mikataba ya Saudia na Marekani pamoja na nchi zingine chache. Imagine Saudia akisema sasa siuzi mafuta kwa dollar nanunua vitu na kuuza mafuta kwa dhahabu au fedha nyingine itakuwaje?

Fikiria Saudia akizuia kununua silaha toka Marekani kama vile sasa alivyo goma vitu vya Canada itakuwaje viwanda vikubwa vya silaha vya vinavyokuza uchumi wa Marekani?

Kumbuka Saudia inatumika sana kueneza ushawishi wa Marekani eneo la nchi za kiarabu na kiajemi.

Cc: Malcom Lumumba
mkuu kweli
ndio maana Trump anaposhawishiwa asitishe kuwauzia silaha kama hatua ya kukemea tukio hilo, anasita na kusema Kuwauzia silaha Saudia ni Kwa ajili ya Kuisaidia Marekani kiuchumi na kufanya hivyo ni Sawa na Kuinyesha marekani kidonge kichungu sana.
Wachambuzi wengine wanasema tukio hilo ni Crisis kwa mahusiano ya US na Saudia Arabia kama 9/11

mkuu Malcom Lumumba karibu utie baraka zako katika sakata hili.
je ni upepo tu unapita, au kuna kitu cha ziada cha kujifunza.
 
Uongo iran kawekewa vikwazo miaka mingap Korea kazkazin je kwa taarifa yako vikwazo akiviweka kwa saud Arabia havita kua na athar yoyote
hayo yalikuwa maoni ya jumla, hasa sisi masikini huku hao waarabu wanawashirika wengi, china, Russia etc wanaweza kutake over.
Ila vikwazo zimbabwe tu vilitosha kununua mkate kwa shilingi milioni miatatu na ushee.
 
Kwani kati ya Usd na mafuta ya ARABIA kipi kinathamani?kwani Saudi ana US treasury bonds yenye thamani kiasi gani?
 
Hii familia ya kifalme ya Al Saud hata ifanye nini itavumiliwa na Marekani maana utajiri wao wa Mafuta unatosha kuwasafisha na pia ni soko kubwa la silaha kutoka Marekani, soko hili linatengeneza maelfu ya ajira kwa wamarekani na Makampuni ya silaha kujipatia faida kubwa
 
Kwani kati ya Usd na mafuta ya ARABIA kipi kinathamani?kwani Saudi ana US treasury bonds yenye thamani kiasi gani?

Kwa wajuz wa Uchumi wanatambua thamani ya Dola Moja ya determinants yake Ni Uzalishaji wa Mafuta lakin Uzalishaji wa Mafuta hautegemi thamani ya dola

Sina uhakika Kama wote wanaelewa Hii theory
 
Kwa wajuz wa Uchumi wanatambua thamani ya Dola Moja ya determinants yake Ni Uzalishaji wa Mafuta lakin Uzalishaji wa Mafuta hautegemi thamani ya dola

Sina uhakika Kama wote wanaelewa Hii theory
Unamaanisha mafuta yanaweza kuuzwa Kwa pesa yoyote badala ya dola? au kuanguka thamani ya dola haita athiri uzalishaji wa mafuta ila kushuka uzalishaji wa mafuta itaangusha thamani ya dola?
 
Unamaanisha mafuta yanaweza kuuzwa Kwa pesa yoyote badala ya dola? au kuanguka thamani ya dola haita athiri uzalishaji wa mafuta ila kushuka uzalishaji wa mafuta itaangusha thamani ya dola?

Swadakta ndio nimemaanisha hivyo Na umefafanua vizuri zaid

Gadafi alikuwa hauzi Mafuta Kwa Dola , Iran wanatumia Euro Na ndio sababu America Na Ulaya hawana Umoja kwny Suala la kuwekewa Vikwazo Iran Kwa Kuwa Vikwazo dhidi ya Iran maana yake kuangusha thamani ya Euro kimataifa
 
Unamaanisha mafuta yanaweza kuuzwa Kwa pesa yoyote badala ya dola? au kuanguka thamani ya dola haita athiri uzalishaji wa mafuta ila kushuka uzalishaji wa mafuta itaangusha thamani ya dola?
mafuta yasipouzwa kwa dola thamani ya dola itashuka sana.. maana dola ni fiat currency
 
Ni kweli Mwandishi raia wa Saudi aliekua anaishi uhamishon US baada ya kua mwiba nchi mwake kulingana na kuipinga serikal yake na kuajiriwa na Jarida la US....CCTV camera zinaonesha alivoingia ubalozin lakin hazionesh akitoka na zinaonesha wafanyakaz wakiambiwa watoke na baadae waliingia Watu 15 toka Saud waliofika na private jet from Saud 3Hrs later na mmojawapo ni mlinzi wa MBS or Mohammed Bin Salman mrithi wa mfalme Hii habari ni ya Leo toka #Hurriyet news ya Uturuki....Baadhi ya Maseneta wa US wameanza kumshinikiza Trump kuchukua hatua japo hali inavoonekana Trump atasita kutokana na mikataba ya zaidi 100$ Billion ya silaha waliosaini....Pia Uchumi wa US kwa kiasi kikubwa umebebwa na Saudi Arabia kwa #petrodollars hii saga itaichafua US kwa double standard maana sidhan km ataweza pambana na mbabe wa kiuchumi km Saudi kwasasa....
 
sijasema Jamal ni mmarekani, ila nimesema kwa ujumla raia wa US sio wakuchezewa. Kwa sababu na yeye alifanya kazi kwa maslahi ya US, Kwenye gazeti la US .

Tutajuaje raia wa Marekani sio wa kuchezewa kama umetumia hadithi ya mtu ambae sio raia? You're not making much sense.
 
Jamal Khashoggi amefanya kazi ndani ya balozi za Saudi Arabia mjini London na Washington kabla ya kukimbilia Marekani na baadae kuajiriwa na Washington Post kama mwandishi wa makala.

Nyingi za makala hizo zilikuwa ni kuishambulia serikali ya Riyadh khasa mfalme Mohamed bin Salman ambae tokea aingie madarakani ameonyesha ukatili wake na kuwa mtu asie na simile kwa yeyote anaekosoa serikali yake.

Hivyo kwa vyovyote vile mfalme Salman asingeweza kumvumulia mtu kama Khashoggi ambae aliwahi kuwa mtumishi wake kwenye ofisi za ubalozi na mtu ambae alikuwa anafahamu siri nyingi.

Hivyo kilichotokea ni mfululizo wa matukio ya nchi maswahiba wa Marekani ambao wanaweza kufanya mambo kama hayo ya mauaji na baadae yakaishia hivihivi.

Itakumbukwa mwaka 2010 majasusi wa Israeli waliingia Dubai na kwenda kwemye hoteli alofikia mwanamgambo wa Hamas bwana Mahmoud Al-Mabhou na kumuulia mbali!

Majasusi hao wa Israeli waliingia Dubai wakitumia pasi za kusafiria za Ireland, Uingereza, Australia, Ufaransa na Ujerumani.

Picha zao ziliwekwa Interpol na kudaiwa kuwa "wanatafutwa" na hadi leo ni hadithi.
 
Msisahu Trump mwenyewe personally has business interests with Saudis.
Trump Org. has done numerous businesses with Saudi Arabia.
Will be Interesting to see how he's handling this.
 
Back
Top Bottom