Bilion 2 za content creators ningefanya nini?

gabylovestech

Member
Joined
Jul 13, 2025
Posts
20
Reaction score
50

“You don’t change youths by giving them money

You change them by giving them access.”

Nitatoa uchambuzi na ushauri wangu kwa uzoefu wangu ONLINE, je hiki kitu kina manufaa?.

Faida na hasara zake ni nini?
Tufanyeje?

Taarifa ya TCRA inasema watumiaji wa intaneti (ama subscribers) wameongezeka kutoka milioni 90 – Machi 2025 hadi milioni 106 – Desemba 2025.

Lakini Imagine ni 2026 na watu 30% tu wanaweza kufikia 5G.

Nitaongea kama kijana ambaye amezunguka mikoa 25+ ya Tanzania. Nimejaribu kufanya EVENTS 10 za Kidigitali mwenyewe na washkaji zangu, na yote yalikuwa na watu 50-100.

Kwenye maisha yangu, siku zote nimekuwa na falsafa ya kuamini kwamba watu wanaweza kuanza kutoka sifuri na kuwa watu fulani kwenye MITANDAO.

❯ Ndio maana pages zangu zimejaa sana resources, Tips na tutorials za bure.

Kuna vitu vingi, hiyo 2B itatumika na havitaleta chochote kwenye nchi wala maisha ya vijana. Zitaishia mikononi mwa WAJANJA wachache.

Najua mawazo yatapuuziliwa mbali kama ilivyo kawaida, lakini je, ITANISIKITISHA? Hapana.

Sasa tuanzeje?
tunahitaji kizazi kipya cha vijana ambao watafundishwa kuvua, si kupewa samaki.

Skills zote za kidigitali, iwe ni Coding, AI, Digital Marketing, Content Creation, YouTubing nk, zinafundishwa bure na hizi taasisi kubwa duniani.

Wanafundisha bure maana wanahitaji watu kwenye platforms zao, wanahitaji taasisi na watumiaji wa platforms zao ila wao wapate pesa na watumiaji pia wapate VALUE wanayotarajia

Maana ya kuwa na Serikali ni kwamba unapata ufikiaji leo na taasisi zote ndani na nchi zote.

Sasa hizi skills vijana wanasimamiwa kupitia portal fulani ya serikali, tuseme inaitwa fanisiprojekti.com.

➙ Hapo kila kijana aliehitimu elimu ya form 4 na kuendelea anajiandikisha na kuanza kujifunza hizo skills. (Huwezi enda na kila mtu PROJEKTI itakufa tu)

Mfumo unafuatilia:

*Amejisajili? (anaweka NIN na contacts basi)
  • Amefanya assignment?
  • Skills zake zikitestiwa ndani na nje ya nchi anafaa?
  • Anakwama wapi?

*Kwa skills zake anatakiwa kuwa Linked na nani (Sio unamchukua @allyjape creator wa utalii unampeleka wizara ya
Viwanda)

Nitatoa mfano halisi. Make.com ni platform kubwa ya kufanya automation. Inayo Make Academy (ni bure).

➤ Mnachukua mtu kama Gaby ama yeyote anayeweza Automation.

❯ Mnawasiliana na Make ili atafsiri au aRecreate hizo kozi kwa Kiswahili ama hata kwa

Kizungu ziwe kwenye platform yao, lakini ziwe linked kwa project ya serikali kulingana na Mazingira yetu ya wananchi wa Tanzania.

Unaweza kufanya hivi kwa YouTube , @OpenAI , meta , @freeCodeCamp , GOOGLE , Binance nk.

Hawa wote wana Academy za BURE kabisa

Zitasaidia kututoa kwenye hatua ya kwanza ya “KUJIFUNZA KUVUA SAMAKI”

➙ Vijana wanaenda kujifunza hapo kwa portal ya serikali (fanisiprojekti.com kwa mfano), na system inafuatilia maendeleo yao polepole hadi wanapohitimu.

Changamoto inakuwa ni vijana kutumia skills zao kuboresha maisha ya maeneo wanayotoka. Kwenye taasisi zao, kuanzia mashinani, kwenye biashara zao na za ndugu zao kuanzia chini.

Wanafanyaje kujikwamua kiFIKRA, kitaaluma na kiuchumi?

Kazi ya Serikali ni kuwatengenezea mazingira,
➤Acheni ushamba wa kuzuia watu kupiga hata picha kwa Mwendokasi
➤waambie TTCL weka intaneti bure.

➤ Wadau kama halmashauri wana majengo kibao hayatumiki, ziwe ICT centers au Digital Economy hubs ambazo vijana watazitumia kujifunza na kujikwamua kiakili, kitabia, na kiuchumi.

Kama halmashauri hazina majengo, taasisi zipo tayari kama mashule nk, ambazo hazitumiki, vijana watumie.

➙ TAASISI za Serikali zisomane na hawa vijana.

Namaanisha, baada ya kuwasaidia hawa vijana, sasa ni vipi taasisi zitawapa fursa vijana.

Tunataka sasa mama mboga kule mtaani kwetu Simike Mbeya, aliekopeshwa pesa na Halmashauri, awe na link na kijana atakayemsaidia kujitangaza biashara yake mtandaoni.

Hii itamsaidia kulipa deni kwa wakati na wengine wakopeshwe, kijana apate kitu kidogo.

sasa kata zote ziachane na makaratasi kwa sababu tuna vijana waliojifunza coding na wanaweza kutengeneza mifumo na kuendesha wao wenyewe. Kila kata sasa ina database na taarifa za kila kitu kuhusu hiyo kata online.

hapo sasa kuna na taarifa ya kutosha kuhusu nchi yetu ONLINE.

❯ Leo nikifika Manyoni, nisianze kutafuta wapi napata lodge, mgahawa, club nk maana kuna vijana washaweka hizo taarifa kwenye encyclopedia yetu ya Kitanzania kwenye mtandao. Hapo, umeinua biashara ndogo ndogo, uchumi mpaka mashinani.

Mimi sihitaji 2B, ningefanya hivi.

➙ Najua kuwa biashara nyingi, kama sio zote zinazofanyika online, pia zipo physical. Nisingewahi kumdai mwananchi kodi ama content creator tozo kwa kupost content yake YouTube ama tangazo la biashara yake (ya mteja wake).
Sahizi YouTube, Serikali inataka youtubers wapewe kibali na TCRA na walipie 50-100k. Hii ningefuta na kuhakikisha vijana wanapata skills za YouTube bure kabisa kutoka YouTube wenyewe.

Kitu ambacho kinaExist ni kuwaonesha tu VIJANA.

Mimi sihitaji 2B, ningefanya hivi.

* Ningehakikisha ni LAZIMA hawa Creators na Influencers wanapewa kazi na mashirika, maduka, taasisi nk ambazo zinaexist kwa mujibu wa sheria na zinalipa kodi.

Mimi sihitaji 2B, ningefanya hivi.

* Ningehakikisha influencers na content creators ambao malipo yao si pesa, siwalipishi kodi wala tozo.

➙ I mean, kuna mtu anatangaza hotel fulani inayolipa kodi kwa mujibu wa sheria, malipo yake ni kwenda kula bure.

Mimi sihitaji 2B, ningefanya hivi.

* Ningetengeneza mazingira kwa creators, mfano MC ana kampuni ameajiri vijana, analipa kodi na ameDeclare, basi akipost content yake au biashara yake Instagram, au YouTube, asilipe tena kodi.

Mimi sihitaji 2B, ningefanya hivi.

* Ningetaka kukamua ng’ombe maziwa, basi lazima ningemlisha majani: JPM aliwapa machinga viparata kwa 20,000/-, value aliyotoa ni Machinga wasisumbuliwe na mgambo. Hawa creators ningewatengenezea Creators Bundle kwa TTCL bei nusu ya watu wengine, hasa wale waliopita kwenye academy yetu.
*Mtu yeyote atakae ZUIA content creator kuFilm kwa maeneo ya public yasipkuwa ya vyombo vya ulinzi na usalama plus Ikulu nk angekiona cha moto

Mimi sihitaji 2B, ningefanya hivi.

* Nisingewahi fungia mtandao wowote, maana najua wazi kwa teknolojia ilipofika, watu watatafuta namna tu ya kuAccess mitandao. Ningeachana na uzamani na ubabe maana ni kazi bure.

Unaweza IGNORE haya kama lengo lako ni:

1. Kupiga pesa za walipa kodi.
2. Huna nia ya dhati ya kuendeleza vijana.
3. Kutaka kutumia kama strategy ya kuzima hasira za vijana tarehe 29.
4. Kusambaza mabango nchi nzima kuwa CONTENT CREATORS wamesaidika (of which ni pesa zao wamelipa kodi).
5. Kufanya PR isiyo na kichwa wala miguu.

Wasalaam kutoka USAWA wa chini Mbali na MEZA zenu,

Written by:
Gabriel M. Patson (Gaby Loves Tech)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…