Bila Umwagiliaji hatutaepuka njaa

MTENDAHAKI

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,013
1,443
Pembejeo ya kwanza ya kilimo ni maji!mwaka ambao mvua zimenyesha wakulima hawapatwi na njaa hata kama serikali haitapeleka pembejeo yoyote! Kwa sasa mvua hazina uhakika na wala hazitabiriki!hii ina madhara makubwa sana kwa kilimo na usalama wa chakula! Hata mtama,ulezi,mihogo ama viazi vinahitaji maji ya kutosha!Ni aibu kwa watu wa kanda ya ziwa kupatwa na njaa ilhali wamezungukwa na ziwa lenye maji bora kabisa kwa umwagiliaji.Kama tunataka kufanya mapinduzi ya viwanda ni lazima tuwekeze kwenye umwagiliaji! Viwanda vitawezekana tu pale tutakapozalisha kwa ziada,kilimo kinaweza kusaidia Taifa kujenga uchumi wa kati kwa usawa na kuchagiza ukuaji wa sekta zingine kama ujenzi,afya, elimu nk.
Namshauri Rais Magufuli, kama anataka kufanikiwa katika uongozi wake aweke nguvu kubwa kwenye sekta ya umwagiliaji!
IMG_20170123_044655.jpg
 
nimekuelewa vyema mkuu.
hakika ni aibu na fedheha kwa mikoa ya kanda ya ziwa kulia njaa na wakati imepakana na ziwa kubwa Africa.
 
Ipo siku njaa itatusaidia kujua vipaumbele vya kufuta umaskini!Katika maisha maji ndio uhai,hata mwili wa binadaam 70% ni maji tu
 
Back
Top Bottom